Lowassa, Msabaha hapatoshi

Lowassa, Msabaha hapatoshi

mkuu Kanda2, samahani naomba nikuulize swali moja tu. Wewe unamaanisha nini juu ya mafisadi? Kwani hapa JF akiongelewa fisadi Rostam, Msabaha, JK unawatetea kwa nguvu zote. Akiongelewa fisadi Lowasa, Mkapa, Sumaye... unapiga nyundo za nguvu?
 
[

- Tizama, kule US Mr. Kerik alitaka kuwa waziri wa Homeland Security, akatuma CV yake kwa ofisi ya rais, ambapo hakusema ukweli ofisi ya rais ilipogundua kuwa hakuwa mkweli, ikamuweka pembeni na kumtosa, lakini FBI automatically wakaingilia kati na kutaka kujua ukweli aliouficha wakagundua kwamba ana matatizo ya kushirkiana na Mafia, wao hawakusubiri bunge lichunguze, au katibu wa rais amuandikie katibu wa bunge, au kuanza kuwapigia simu Kerik na Mafia, wao walichofanya ni kumburuza Kerik mara moja kwenye sheria kwa kuidanganya ofisi ya rais wa US, Full Stop.

- Ndugu zangu hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa kwenye utawala unaoheshimu sheria, Takukuru walitakiwa kuwa wameshawaburuza wote waliotajwa kuhusika na Richmond pale tu ripoti ya kamati ya bunge ilipopitishwa na bunge, lakini kwa sababu ni Banana Republic tizama tulipo na hii ishu, mara Hosea amesema hawana makosa, mara kikao cha NEC kimewasafisha, mara kuna habari zingine hazikutolewa kuinusuru serikali, mara sasa Msabaha ndiye ana ukweli wote, foolishness!

Hivi hili taifa tumelogwa na nani? wakati hizi ishu zingine ziko so open huhitaji hata kuwa mwanasheria au mwanasiasa kuzielewa, kwamba hawa mafisadi wanazidi kutuchezea akili tu!

Ahsanteni.

William.

[/QUOTE]
Haya maneno mazito sana. Kila mtu anashangaa strategists wetu wananini ndani ya bongo zao maana wanajaribu kufanya the impossibles all the time. It is high time now to start respecting the rule of law.Vinginevyo hakuna haja ya kuendelea kuwafunga watu magerezani.Tuwaachie huru
 
mkuu kanda2, samahani naomba nikuulize swali moja tu. Wewe unamaanisha nini juu ya mafisadi? Kwani hapa jf akiongelewa fisadi rostam, msabaha, jk unawatetea kwa nguvu zote. Akiongelewa fisadi lowasa, mkapa, sumaye... Unapiga nyundo za nguvu?
wapi nimepiga nyundo kwa sumaye na lowassa plz thibitisha.
 
Masatu punguza uongo ndugu yangu ... kama hizo kazi zote anazifanya yeye, wakati ule alipoenda India Gazeti la MwanaHalisi nalo lilienda India?

Hayo majina ya waandishi wa habari ambayo yanawekwa kwenye Gazeti la MwanaHalisi ina maana ni ya kubuni?

Ndimara Tegambwage alipomwagiwa tindikali alikuwa wapi na anafanya nini? Alipohojiwa alisema yeye ni mshauri wa kuhariri habari za gazeti la MwanaHalisi.

Tatizo lako ni kwamba mapenzi yako kwa CCM na kwa watu fulani ndani ya CCM yamekufanya uwe kipofu na kiziwi. Ikiguswa CCM kidogo tu tayari unakuja na hoja zisizo na mashiko, zimejaa uzushi na uongo.

Wakati ule Sitta anakaangwa na NEC kule Dodoma ulishangilia sana, yalipoanza kurushwa mawe baada ya NEC ukawa kimya kabisa. Wewe, Makamba akina Chiligati hamna tofauti kabisa, agenda yenu ni kutetea mafisadi kwa nguvu zote.

Baada ya kikao cha NEC wenzako (Makamba, Chiligati + all pro ufisadi) walitoka wanashangilia, mawe yalipoanza kurushwa wakakaa kimya, mara mjomba wako Makamba akaenda Urambo kujikomba kwa kuwa alishajua kwamba alichemsha. Chiligati alikaa kimya wala hakutaka kuongelea tena kwa mbwembwe swala la maamuzi ya NEC.

Last time ulidanganya hapa kwamba JKT ilikuwepo mpaka zama za Mkapa, wakati hakuna ukweli wowote na wewe mwenyewe ukasema kwamba ulienda JKT zama za Mkapa, uongo mkubwa! Nilikuomba uthibitishe ukaingia mitini. Tuache kupakaza.

Je, unataka na leo tuamini huo uongo wako kwamba Kubenea ni kila kitu? Kwamba ni mwandishi, mhariri, msambazi, dereva, mhasibu, etc?

Kaazi kweli kweli!

Sitajibu hizo blah blah zako nyingine hazina mashiko.

Hilo highlighted haliwezi pita bila kutolewa ufafanuzi. Yes nilikwenda jeshini Rais akiwa Mkapa uthibitisho gani unaoutaka? Uthibitisho ni mimi mwenyewe nilikuwa huko.
 
Sina nia ya ligi, lakini uongo ukiwekwa inabidi kuukanusha. Sasa sijui wewe ulienda JKT gani iwapo wenye Jeshi wanasema kipindi hicho hakukuwa na waliojiunga na JKT.

Hatimaye Julai 10, 1963 JKT ilianzishwa kwa kutumia sheria ya Jeshi namba 16 ya kifungu cha 353 ya mwaka 1963. Dhamira kuu ikiwa ni kuunganisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini na kuwapatia mafunzo bila kujali tofauti zao za elimu, dini, rangi, kabila au jinsia.

Azma ya jeshi hilo ilikuwa ni kuwaandaa vijana kijeshi na kuwapatia malezi ya kitaifa yanayozingatia nidhamu, utaifa na uzalendo, ili kuweza kujenga taifa lililo bora. Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, Jeshi hilo lilianza na vijana wa kujitolea wenye elimu ya chini, baadaye mwaka 1966 serikali ilitunga sheria ya kuwataka vijana wasomi wajiunge na JKT. Kutokana na serikali kukosa uwezo wa kumudu gharama za uendeshaji wa mafunzo hayo, mwaka 1994 ilisitisha kuchukua vijana wa kujitolea kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, kuwepo kwa ongezeko la mmomonyoko wa maadili, vitendo vya utumiaji dawa za kulevya na maovu mengineyo ndani ya jamii, mwaka 2001 serikali iliamua kurejesha JKT kwa utaratibu wa kuchukua vijana wa kujitolea kwa miaka miwili, na sasa wahitimu wote wa kidato cha sita kwa mujibu wa sheria watalazimika kupitia jeshi hilo kabla ya kuingia vyuoni kuanzia mwakani.

Imeshauriwa kuwa taasisi, idara, kampuni, na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuajiri vijana wenye sifa kutoka JKT, waliopata mafunzo ya kijeshi na malezi yenye nidhamu na uzalendo kwa nchi yao. Pia wanapokuwa vikosini, hufuatiliwa tabia na nyendo zao, tofauti na vijana ambao hawajapitia JKT.

“Naipongeza serikali kupitia Bunge lake tukufu kwa kurejesha mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ifikapo 2010, kwani taifa lipo katika wakati mgumu kutokana na kumomonyoka kwa maadili sehemu mbalimbali za kazi, shuleni na vyuoni, hali inayosababisha kuwepo kwa migomo ikiwa ni ukosefu wa maadili na uzalendo kwa nchi yao,” anasema Mkuu wa Idara ya Utumishi JKT, Luteni Kanali Eslom Lubinga.

Hicho ni kipande cha habari kutoka gazeti la HabariLeo, gazeti la serikali ambalo unaamini linaandika habari za kweli.

http://www.habarileo.co.tz/makala/?n=3077&cat=makala

Labda nikukumbushe kwamba Mkapa alikuwa madarakani kuanzia mwishoni mwa 1995 mpaka mwishoni mwa 2005, by then hakukuwa na mtu anakwenda JKT kwa mujibu wa sheria.

Nimefunga mabishano na wewe, maana nikiendelea nitakuwa sawa na kichaa anaefukuza upepo.
 
mkuu kanda2, samahani naomba nikuulize swali moja tu. Wewe unamaanisha nini juu ya mafisadi? Kwani hapa jf akiongelewa fisadi rostam, msabaha, jk unawatetea kwa nguvu zote. Akiongelewa fisadi lowasa, mkapa, sumaye... Unapiga nyundo za nguvu?
hujajibu swali langu vipi?
 
I said it: Theory behind vita dhidi ya Ufisadi ni "mwaga mboga, nimwage ugali!" Kama kweli Msabaha alikuwa na vielelezo kwa nini hakuvitoa na anavitoa sasa hivi? Ama kweli masteringi (mafisadi) hawauawi, wanapata vijeraha vidogovidogo (kujiuzulu, nk) tu! Mchezo huu unafanana na movie ya kizungu yenye jina la LOST! Yule unayemwona mzuri sana kwa tabia anageuka baadaye na kuwa mbaya sana na mbaya sana anageuka kuwa mzuri sana kitabia! Kadri unavyoiangalia wewe mwenyewe unakuwa LOST! Kaazi kwelikweli!
 
Nilishawahi kuhoji wa heading za mwanahalisi since day 1 ni lowasa-rostam-mkapa.....,

sidhani kama yale mashaka yangu ayameondolewa na haya yanayoandikwa leo, niwe mkarimu kwa kumshukuru bill kwa analysis nzuri na yenye maono kwetu wana jf na watz.
 
Itabidi nilifanyie kazi sana hili, ili kujua uwezo na uafanyaji kazi wa vyombo vya habari ni kupasha habari yoyote tu, au vinaweza vikawa chachu ya mabadiliko muhimu sana.

Kama kweli hili gazeti linataka mambo yawe 'uchi' nafikiri wangeibana hii taarifa hili Msabaha aanike 'huo ukweli' ambao ungesaidia sana.

Otherwise I am getting confused, SUPPOSE kesho Msabaha akakanusha!

Kwa taarifa yako MwanaHALISI ndilo lilikuwa gazeti la kwanza kuandika list ya mafisadi kama ilivyotolewa na Dr W. Slaa. Mafisadi hao walimtishia Dr Slaa kwamba afute kauli yake hiyo kwamba wao ni mafisadi na pia awaombe radhi kwa kuwachafulia reputation yao au watamfungulia mashtaka. Dr Slaa hakufuta kauli yake na hadi hii leo hakuna hata mmoja wa wale mafisadi waliotajwa na Dr Slaa aliyethubutu kufungua kesi mahakamani dhidi yake.

Wakati mwingine tuwape credit waandishi wetu wa habari katika vita hii dhidi ya mafisadi wamejitahidi sana kutuhabarisha Watanzania juu ya maovu mbali mbali yanayofanywa na mafisadi dhidi ya nchi yetu. Kuhusu huyu Msabaha kukanusha hii habari labda anaweza kufanya hivyo, lakini ukiangalia trends tangu vita dhidi ya mafisadi sidhani Msabaha kama atakuwa na ubavu wa kukanusha kuhusu habari hii, tusubiri.
 
Ni kweli mkuu, maana ukipenda huwezi kuona. Kubenea nimemuuliza ana kwa ana uhusiono wa gazeti lake na JK na hawezi kujibu hili.

Atawasema mafisadi woote hii ndio plan ya JK, atawasema woote lakini sio JK! piga ua garagaza.

Kutuhabarisha habari za ufisadi kwa masada wa JK ni habari njema kwa JK ili Tz ionekane kuna uhuru wa habari, Pasi kuona hatua zozote kwa mafisadi!

lakini kumuacha JK katika tuhuma zote za ufisadi ni sarakasi ya ajabu,\

Sitakusaidia katika hili mkuu, labda kama unataka analysis zaidi.

Unachosema ni historia ya akina RAI.

Sijasema Msabaha atakanusha, je hao walengwa wakipata taarifa hii,si watafanya lolote kumzuia asiseme, je lengo lake Kubenea ni nini? aseme au asiseme?

PIGA UA FANYA ASSIGNMENT ZAKO VIZURI, GAZETI LAMWANAHALISI LINAMNYENYUA SANA JK, KAMA HUNA TAARIFA HII, BASI UMEPITWA NA YANAYOONGELEWA!

Credit nampa, ila nimeshamweleza habari zake ziwe na mantiki, kwanza zisifiche kitu, pili zisilenge kumpa kuddos Kikwete au kumkwepesha JK na ishu za ufisadi nchi hii hayo tu!

Pia aeleze ile tindikali ni siasa au ishu zingine, mtetee katika hili pia,
 
Nilishawahi kuhoji wa heading za mwanahalisi since day 1 ni lowasa-rostam-mkapa.....,

sidhani kama yale mashaka yangu ayameondolewa na haya yanayoandikwa leo, niwe mkarimu kwa kumshukuru bill kwa analysis nzuri na yenye maono kwetu wana jf na watz.

Afadhali umeliona, hakuna seriousness, Mwanahalisi linatakiwa liwe tofauti kabisa na Alasiri jamani au magazeti ya Shigongo.Haiwezekani taarifa za rushwa zikawa kidakudaku tu
 
Sitajibu hizo blah blah zako nyingine hazina mashiko.

Hilo highlighted haliwezi pita bila kutolewa ufafanuzi. Yes nilikwenda jeshini Rais akiwa Mkapa uthibitisho gani unaoutaka? Uthibitisho ni mimi mwenyewe nilikuwa huko.

Acha kukomaa wewe na blah blah zako ...JKT ilifungwa rasmi kabla ya Mkapa kuwa raisi
 
Ni kweli mkuu, maana ukipenda huwezi kuona. Kubenea nimemuuliza ana kwa ana uhusiono wa gazeti lake na JK na hawezi kujibu hili.

Atawasema mafisadi woote hii ndio plan ya JK, atawasema woote lakini sio JK! piga ua garagaza.

Kutuhabarisha habari za ufisadi kwa masada wa JK ni habari njema kwa JK ili Tz ionekane kuna uhuru wa habari, Pasi kuona hatua zozote kwa mafisadi!

lakini kumuacha JK katika tuhuma zote za ufisadi ni sarakasi ya ajabu,\

Sitakusaidia katika hili mkuu, labda kama unataka analysis zaidi.

Unachosema ni historia ya akina RAI.

Sijasema Msabaha atakanusha, je hao walengwa wakipata taarifa hii,si watafanya lolote kumzuia asiseme, je lengo lake Kubenea ni nini? aseme au asiseme?

PIGA UA FANYA ASSIGNMENT ZAKO VIZURI, GAZETI LAMWANAHALISI LINAMNYENYUA SANA JK, KAMA HUNA TAARIFA HII, BASI UMEPITWA NA YANAYOONGELEWA!

Credit nampa, ila nimeshamweleza habari zake ziwe na mantiki, kwanza zisifiche kitu, pili zisilenge kumpa kuddos Kikwete au kumkwepesha JK na ishu za ufisadi nchi hii hayo tu!

Pia aeleze ile tindikali ni siasa au ishu zingine, mtetee katika hili pia,

Naona umeshaleta jingine kabisa ambalo halihusiani na thread hii. Mwambie msabaha akanushe habari hii. Kama ushahidi wa kutosha dhidi yaliyofanywa na Mtandao mwaka 2005 ili Kikwete awe madarakani haukuwezeshi kumuweka Kikwete katika kundi lipi mpaka gazeti la MwanaHALISI liandike hivyo basi una safari ndefu. Wengi tunaofuatilia siasa za Tanzania tunajua Kikwete ni wa kundi lipi wala hatuna haja ya kusubiri MwanaHALISI liandike ili tuelewe hivyo.
 
Back
Top Bottom