Tetesi: Lowassa nchini Kenya tena

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Baada ya kuona mwaliko wa Edward Lowassa kwenye Uzinduzi wa chama kipya nchini Kenya cha Jubilee Party hapo jumamosi tarehe 9 September nimejiuliza maswali mengi sana bila kupata majipu!!

1: Hivi ni nchi gani Dunia ambayo ilishawai kufanya kitendo ambacho Kenya wanakifanya cha Kutengeneza chama ndani ya chama wakati hivyo vyama unavyovivunja ndivyo unavitumia kutawala?

2: Rais aliyepo madarakani kuanzisha chama kipya cha siasa ambacho atakitumia katika uchaguzi ujao hiki nacho ni kituko kingine ambacho nakiona!


3: Lowassa anaalikwa kwenda kwenye uzinduzi huo kama nani hasa
Mimi ninavyojua waalikwa uwa ni Mwenyekiti wa chama ,Katibu wa chama, Au kiongozi mkuu wa chama ( Chifu)

3: Sasa huyu ndugu yetu Lowassa anaenda kama nani huko ni mjumbe tu wa Kamati kuu anaenda kukiwakilisha chama tena nje ya nchi?

4: Sasa kwa nini tusiamini Maneno kwamba Lowassa aliinunua chadema?
 
Hicho cheo walichomtambulisha nacho ndicho alichokwenda nacho.

Kwanini usifikiri zaidi ya box?
Kuna kumuakilisha mwenyekiti,kuna kwenda kama rafiki wa waanzilishi wa chama,kuna kwenda kama mzoefu wa siasa za chini chini,kuna kwenda kama mwanasiasa wa upinzani n.k n.k
Ishu ya kununua chama ni akili ya maiti
 
Utaratibu mzuri kuwa na muungano wa vyama vingi . Sheria zao zinaruhusu na ni utaratibu mzuri kuunganisha watu wenye ukabila mbele.
Hata hapa kwetu inatakiwa sheria zibadilishwe ili vyama viweze kuungana official kwa ajili ya uchaguzi
 
Mtoa mada fuatilia historia ya siasa za Tanzania. Jishughilishe wacha kuuliza maswali yenye majibu
 
Hakika mkuu.
 
Ninakushauri hayo maswali yako yapeleke Jubilee Party kwani sisi wengine hatujui kinachoendelea Kenya na wala hatuifahamu katiba yao.
 
Unahisi wakenya wote hawana akili na kwamba hawakuwahi kujiuliza maswali rahisi kama haya na kuyapatia majibu kabla ya kufanya hayo wanayotegemea kuyafanya.......??? Jielimishe juu ya jambo unalotaka kuwasilisha mbele ya umma kama hoja vinginevyo waweza kugeuka kituko, kwa taarifa yako ndogo sana, kinachotegemewa kufanywa tar 09 ni kuzindua coalition na si political party......
 
Hivi Mutharika kule Malawi si alinini?
Na kule Israel huwa kunatokea nini?
Ninakushauri hayo maswali yako yapeleke Jubilee Party kwani sisi wengine hatujui kinachoendelea Kenya na wala hatuifahamu katiba yao.[/QUOT
 
Wewe mtoa mada lini wamekukata mkia na kukuingiza kwenye zizi la ng'ombe?, mimi nakujua wewe ni ukawa, au kuna mtu anachezea akaunti yako
 
Mtoa mada unaakili za kushikiwa, kama kusoma hujui hata picha huoni pia? [emoji13]
 
Anaenda kwa cheo cha "aliyekuwa mgombea mwenye mvuto lakini akashindwa vibaya"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…