View attachment 394510
Baada ya kuona mwaliko wa Edward Lowassa kwenye Uzinduzi wa chama kipya nchini Kenya cha Jubilee Party hapo jumamosi tarehe 9 September nimejiuliza maswali mengi sana bila kupata majipu!!
1: Hivi ni nchi gani Dunia ambayo ilishawai kufanya kitendo ambacho Kenya wanakifanya cha Kutengeneza chama ndani ya chama wakati hivyo vyama unavyovivunja ndivyo unavitumia kutawala?
2: Rais aliyepo madarakani kuanzisha chama kipya cha siasa ambacho atakitumia katika uchaguzi ujao hiki nacho ni kituko kingine ambacho nakiona!
3: Lowassa anaalikwa kwenda kwenye uzinduzi huo kama nani hasa
Mimi ninavyojua waalikwa uwa ni Mwenyekiti wa chama ,Karibu wa chama, Au kiongozi mkuu wa chama ( Chifu)
3: Sasa huyu ndugu yetu Lowassa anaenda kama nani huko ni mjumbe tu wa Kamati kuu anaenda kukiwakilisha chama tena nje ya nchi?
4: Sasa kwa nini tusiamini Maneno kwamba Lowassa aliinunua chadema?