Elections 2015 Lowassa: Serikali yangu itaangalia jinsi ya kuvunja mkataba wa bandari ya Bagamoyo

Kwa hiyo pale Bagamoyo hiyo bandari inatakiwa kuserve nini cha ziada anbacho hakiwezekani kufanywa na bandari za Mtwara, Dar na Tanga zikiwekwa vema.

Kikwete anataka kila kitu kihamie Bagamoyo. Kuna ule mradi wa maendeleo pia aliurushia huko. Ikajengwa bara bara ya haraka ya Msata pia na kuacha bara bara kuu ya Dar morogoro ikijitengeneza matuta. Angeendelea kuwa Rais angetaka hata uwanja wa ndege wa KIA uhamishiwe Bagamoyo. Naunga mkono hoja ya Lowassa ya kuistopisha na kuwekeza zaidi Mtwara na Tanga.
 
The same kwa Chuo cha Nelson Mandela kilikuwa kijengwe Mbeya,Lowasa akakihamishia Arusha

Mie naona ahamishe Bahari monduli na wajenge bandari patakuwa karibu zaidi na Uganda.
 
Kama bandari ta Bagamoyo inajengwa kwa fedha za BMW hiyo sawa... Lakini kama ni kodi na jasho la watanzania basi asahau...
Tanga, Mtwara kuna potential kubwa sana kuliko Bagamoyo....
 
Nahisi kichefukichefu kuwa mtanzania hasa pale unapoona mtu asiyejua chochote anaongea jambo akiwa kama analijua. Unaweza ukapinga terms za mkataba lakini si kupinga umuhimu wa bandari hii; economically, politically and strategically.

Tumesema vya kutosha juu ya sababu za bandari hii kujengwa Bagamoyo, ikumbukwe mradi huu utahusisha ujenzi wa barabara ya hadi mlandizi na km za reli hadi reli ya kati na TAZARA ambapo umbali ni kati ya km 35-65 kufikia barabara ya morogoro na reli hizo. Bila shaka mradi utaleta decongestion ya jiji la Dar es Salaam ambapo location yake inafanya ugumu kupanua bandari ya Dar kufikia hiyo TEU milion 20.

Tumesema tena, strategic location ya Dar, same as Bagamoyo ni conducive kuwa na mradi wa ukubwa wa namna hiyo kwani utaweza kuunganisha nchi tarajiwa za kiafrika bila kuhitaji miundombinu mipya mingi kujengwa tofauti na Tanga ambako ni relatively mbali na nchi hizo.

Huwezi kujenga MEGA port ya Teu 20milion kwa kulenga nchi ya Uganda yenye import and export value ya $4b na 3b$ huku ukijua kuwa Uganda sio centrally located na ni lazima ujenge na bandari nyingine. Huu ni uwendawazimu wa hali ya juu.

Tumesema sana, politically, bandari ya Dar (same as Bagamoyo ) ni good application ya Game theory katika kuwania lango kuu la bandari katika ukanda wa afrika Mashariki (Gateway), jambo ambalo hata kenya analiogopa kwani hii maana yake hata biashara ya bandari yake ya Mombasa ni mashakani. Whats a strategic move like that? Habari ya Kikwete kutoka pwani eti ndio sababu za kujenga bandari hiyo ni sababu mfu za waliozoea kufanya hivyo wsnadhani watu wote wako interested na mambo hayo.

Huwezi kuzungumzia nchi ya kipato cha kati ikiwa si landlocked conuntry na ni gateway huku bandari yako uwezo wake kwa mwaka ni Teu 800000, huu ni mzaha ambao labda ukawa ni kawaida yao kufanya sanaa hata kwenye mambo ya msingi.

Mradi huu maana yake na faida yake, unquestionably; watanganyika acheni blanlaa nyiiiingi. Kama watu hamjui mkae kimya au muilaumu serikali yenu kwa kutowaelimisha wananchi wake ikiwa pamoja na masharti/terms za mradi husika ambapo bila shakamna haki kujua. Mengine yote ni upungufu wa elimu, maarifa na reasoning capacity ya watanzania.
 
Watanzania tufahamu kuwa utafiti uliofanyika na wataalamu kutoka Japan na ambao ulikwishawakilishwa wizara ya viwanda umeonyesha kuwa Bagamoyo hapafai kujenga bandari. Sababu kubwa ni kuwa Bagamoyo ni shallow waters (kina kidogo sana). Ili kujenga bandari ni lazima ichimbwe sana kuongeza kina. Kwa bahati mbaya sana huwezi kuchimba kirahisi sababu Bahari ya Bagamoyo ina mwamba mgumu sana unaonekana hata kwa macho tu. Hivyo gharama ya kuvunja mwamba ili kuongeza kina ni kubwa mno. Ni sawa na kujenga Bandari mbili. Wajapani walipendekeza kupanuliwa kwa bandari ya Tanga ambayo Mungu alikwishaijenga ikiwa na kina kirefu. Huhitaji kuchimba. Isitoshe, Hayati mwalimu Nyerere alishajenga reli kuunganisha Bandari hii na mtandao wa reli nchini. Kwanini tujenge Bagamoyo? Hii tabia ya kujipendelea nyumbani kwa gharama kubwa ya taifa haikubaliki kamwe. Watanzania tukatae upuuzi huu. Lowassa upo sahihi sana kufikiria kuvunja mkataba huu wa kipuuzi. Waambie wachina wakapanue bandari za Tanga na Mtwara.
 

Wakulipe kwa somo unalolitoa hapa
 
Mkuu tuna shukuru kwa maelezo yako . Unachoongea hapa wengi wetu tunakijua kama wewe ujuavyo au pia tunajua zaidi mradi huu kuliko wewe. Gharama ya mradi huu hapo Bagamoyo ni kubwa mara mbili ya kuweza kujenga bandari mbili kama hizo Mkoani Tanga na Mtwara na kutengeneza miundo mbinu mipya na mizuri kuliko hii ya sasa unayo zungumza wewe hapa. Watu walisha fanya tafiti na tathmini katika hilo kwahiyo unapozungumzia kwamba ni Elimu ndogo ya watanzania ndio yenye kuleta ukinzani ktk hili mimi binafsi sikubaliani na wewe.
 
Haya ndiyo mabishano kutoka kwa watanganyika ambayo huwa siyapendi. Kwa ulivyosoma comments za wadau tatizo lao ni gharama au Hakuna haja ya kujenga bandari kama hiyo Bsgamoyo badala yake waendeleze Bandari za Tanga na Mtwara? Ndio yale niliyosema why watanzania mnapenda kukomaa na kitu msichokijua na kujifanya mnajua? Kwani huu mradi unajengwa fedha zenu? Ni mou kati ya China-/Oman na Tanzania. Hivyo kila pande ina nafasi ya kujua wapi aweke fedha zake? Ukumbuke pia Bagamoyo port ni kwa wachina kupitisha bidhaa za viwanda vyao kwa ajili ya masoko ya nchi kadhaa za kiafrika. Utamwambiaje akaendeleze mtwara au Tanga kama haiko katika strategic zones zake?

Kujua mradi unajengwa kwa gharama kubwa kiasi gani kwa fedha za mikopo au msaada kuna vigezo vingi vya kuangalia. Ni budi ujue huo mkopo ni wa interest kiasi gani? Ni wa miaka mingapi nk? Hata hivyo, hayo ni sehemu yenu ninyi watanzania sio kosa la mradi. Je hujui kwamba wako wafadhili wanatumia zero - interest loan lakini wanakuwa na hidden interest kupitia kwenye vipuri, teknolojia na wataalam wa mradi husika? Ndio hasara za kuwa maskini huko, ni lazima ukubali kutokuwa kwa elimu kunachangia. Na mradi wa Bagamoyo port bila shaka hautaepuka hayo.

Anyway, kwaheri ndugu nchi yenu maamuzi yenu.

Ms
 
kula tano mkuu ,
halafu wakati wanaitumia bandari bure na kukomba maliasili, sisi tutakuwa bize tunalipa riba za madeni waliotukopesha kwa benki zao...mikataba mingine bana!wana himiza mradi wa bandari ambayo hata hatuihitaji kwa sababu wanataka kucontrol bandari kwa kusafirisha bidhaa zao na wanataka kutuweka kwenye madeni na nchi zao ili wachukue riba zetu vizazi na vizazi vijavyo! yale yale wanayofanya World bank.
Lowasa kasema tutaanza kujitegemea wenyewe bila kutegemea misaada a.k.a mikopo kutoka nchi za nje, huo ni mkakati mzuri sana, tujiunge na nchi nyingine za africa mashariki na Africa kwa ujumla kuendeleza uchumi wetu, tusaini mikataba ya gesi na madini yenye faida kwa nchi, tushughulikie wakwepa kodi kubwa kubwa, tuondoe misamaha ya kodi asiyekubali aondoke....tutafika tu, sio haya magumashi ya kuuza kila kitu na kugawa maliasili kama karanga halafu kwenda kuomba omba misaada na mikopo kwa hao hao tunaowapa maliasili zetu kwa bei za bure.
 
reli ya kutoka tanga kwenda uganda ipo ni kuikarabati tuu
 
Kweli mkuu haiingi akilini kutumia gharama ya bandari mpya ilhali mtwara na tanga ziko ovyo..ccm tumewachoka sn
 

Nimejifunza kitu kikubwa sana siku ya leo,,, watanzania siasa zimetujaa hata kwenye mambo ya kimaendeleo.. JK tunapomlaumu pia tuangalie upande wa pili kwa watangulizi wake,, kuna watu walijenga barabara na kupeleka umeme milimani just kwa sababu ni nyumbani, kuna mtu alihamishia mradi wa maji kwao na kuwanyang'anya watanzania wenzie, kuna mtu kaongeza mipaka ya kwao kwa kuiba eneo la
mji mwingine... JK kashindwa kuvumilia kuwaacha hivihivi ndugu zake huku wenzie wamefanya kitu kule makwao...
Kwa namna moja au nyingine ilitakiwa tuwe na akili kama za waindonesia lakini kwa bahati mbaya hizo akili hakuna afrika aka kwa watu weusi... Maisha ya mtu mweusi huwa ni ya kishabiki zaidi na si uzalendo kwa taifa.. hakuna kiongozi mzalendo africa,,TICS kapewa karamagi na lowassa alikuwepo hakupinga hili,, buzwagi imesainiwa pale churchill hotel london lowassa alikuwepo hakupinga nalo....
 
Me nafikiri tatizo sio eneo la kujenga hiyo bandari kwani hata bagamoyo sio shida na bado faida itapatikana tu,, tatizo hiyo bandari tunaijengaje?? Kwa gharama zipi na wapi zinatoka?? Kuna mdau ameandika hapo juu uzi mrefu na ukiusoma vizuri utaona makosa ya angola na wakenya ambapo ujenzi unafanywa na mikopo kutoka china na namna ya kulipa ni mateso makubwa,,, je kwetu ikoje?? tuna akili za waindonesia??? kwa maana ya technology transfer? au ndio upopoma!! Kama bond ni wao wajenge waoperate 50yrs wajilipe then wasepe na mengine tunacharge kama kawa na watu wetu watakodisha mayard na population inaijenga pwani kiuchumi sio mbaya acha wajenge..
Kama tunategemea wajenge halafu tulipe hapo hapana...
 
Mtu kujenga na kuoperate miaka 50 ni ujinga maana miaka 50 wengi hawatakuwepo kabisa
 
Mnashabikia ujinga huuu sio, visas vyake apeleke kaburin huko, nmezid mchukia huyu kunya kunya
 
Wajuzi mnahitajika mtoe elimu kidogo ili watu waelewe ni aina gani ya mkataba tumeingia hapa maana inawezekana tunabishana humu kumbe mkataba unatufavor hata kwa miaka 50 bado tutagain...
maana kama bond ni wao wajenge waoperate 50yrs then wasepe watuachie bandari sioni tatizo maana bado tutakuwa na faida.
1. Wachina wataitumia kama central hub ya
mizigo yao yote kwa kenya,uganda,malawi,
zambia,sudani,tanzania nk maana ikumbukwe wachina wanabiashara nyingi sana ukanda huu.
2. Mkoa wa pwani utanyanyuka kiuchumi.
3. Msongamano dar utapungua kama si kwisha.
4. Wachina wanaweza kutujengea railway line
bure kufika sehemu mbalimbali kwenye
border ili biashara zao ziende haraka na
wapate faida ya haraka na kubwa.
5. Wanawake wengi wapwani watachanganya damu kwa kutuzalia watoto wa kichina wengi maana hawa jamaa watakaa sana hivyo basi angalau tutakuwa tumeleta akili mpya kwenye hiki kizazi.
6. ajira nyingi zitatengenezwa hapa.
7. Bado makusanyo ya kodi yataongezeka maana kwa namna moja nyingine hii bandari itakuja na investment nyinginezo nje ya bandari yenyewe..
8. Tunaweza kuwabana 60% wafanyakazi wawe wazawa na kiwango cha mishahara kiwe kizuri.
9. Tunaweza kupata bajeti ya kukarabati bandari ya tanga pia na tukawashawishi wakizidiwa tanga port ikawa backup yao...

Faida ziko nyingi sana na nyingine zitategemea aina ya mkataba... Mwenye mkataba auweke tuujadiri pia..
 
Mtu kujenga na kuoperate miaka 50 ni ujinga maana miaka 50 wengi hawatakuwepo kabisa

Sio lazima wewe uwepo kwani hata wao hawatakuwepo... Hasara au faida ni kwa kizazi kijacho kwani bado wakiona ni hasara wanaweza kuihujumu vilevile mpaka wenyewe wakaikimbia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…