Abel Ndundulu
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 846
- 388
Nampa HEKO LOWASSA!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo unasikiliza maneno ya wanasiasa na kuyaaamini na hapa namaanisha wote wa Ug, Ke na kwetu pia! Hawo wanasiasa wote hakuna kitu wanajua wao wanaongea tu kwa kufuata kile watu kama ninyi mnapenda kusikia na maamuzi wanayoyafanya ndiyo yanayokuja kuzigharimu nchi zetu!
Uganda hawawezi kutumia Bandari ya Tanga kwa ajili ya ku-export mafuta yao ni rahisi kihivyo tu!
Pili Tanzania hatuna fedha ya kuwekeza kwenye Ujenzi wa Reli mpya ya ktk Tanga mpka Uganda pmj na Bandari ili kukidhi soko la Uganda, hayo maneno yote unayosikia ya Bandari ya Bagamoyo hizo siyo fedha zetu ni fedha za ktk Uchina na mtoa fedha ndiyo anaamua ni wapi aweke fedha yake sasa kama wamechagua B'moyowana sababu ingawaje sizijui sababu zenyewe!
Tatu kama ukiniuliza mimi Tanzania kwa sasa hatuhitaji reli mpya ya ktk Tanga kwenda Uganda bali tunahitaji kwanza kuzijenga upya Reli zetu tulizonazo ili zifanye kazi kwa full capacity kama Reli ya kati iende sambamba na kufufua Bandari ya Kigoma ambayo ilikuwa inashusha mizigo ktk kwenye treni na kuipakia kwenye Meli kwenda Zambia, Kongo na Burundi, kufufua na kuijenga upya reli ya ktk Dar kupitia Ruvu na nyingine ktk Tanga mpaka Arusha, hivyo tunapaswa kuanzia hapo kwanza kabla ya kufikiria kujenga Reli ambayo haipo kabisa sijui mpka Uganda!
Ingekuwa vyema kama ungesemea kidogo hiyo ya bagamoyo na umuhimu wake. Si lazima mizigo kwenda Uganda tu, tuna viwanda kaskazini mwa Tanzania. Ambako vipuli vya kuviendesha vinahitajika. Kwa swala la mtwara, kuna nchi jirani kama Zambia, mikoa yetu ya mbeya na kwingineko nazo zingefaidi. Iweje bagamoyo? Tafadhali fafanua ndugu, nasi tujue dhana halisi ya hiyo bandari ya Bagamoyo.
Hizi contract za bagamoyo ni za deal deal tu , jamaa wanasubir big man aondoke ofisin then wapige chini mradi mzima
Nimeona bora muwekezaji mzungu kuliko mchina.
Leo katika taarifa ya habari ya Channel Ten nimemsikia Rais mtarajiwa wa awamu ya tano Ngoyai Lowassa akisema kwamba Serikali yake itaangalia jinsi ya kuuvunja mkataba wa bandari ya Wachina Bagamoyo.
Amesema haoni mantiki ya kutumia mabilioni kujenga bandari moja Bagamoyo wakati bandari za Tanga na Mtwara ziko ovyo.
Kama kawaida wananchi wa Tanga wamesema kura zao zote ni kwa UKAWA na adui CCM lazima asome namba mwaka huu.
VIVA UKAWA!
NOTE: Kwa msio fahamu kuna umbali wa kilomita 1200 kutoka Tanga mpaka Kampala (Uganda) ukilinganisha na kilomita 1500 kutoka Mombasa (Kenya) mpaka Kampala.
Lakini Waganda wanatumia bandari ya Mombasa sana kwa sababu Tanga hamna kitu.
Lowassa hamuwezi na hata muweza mtoto wa mjini Jakaya Kikwete,wacha ajifurahishe tu,mtoto wa mjini ni wamjini na wa shamba ni washamba tu.Kesha mtangulia milele.
Ndugu inabidi kwanza uelewe Historia ya haya mambo kabla ya kuandika tu kwa ushabiki wa kisiasa! Sababu ya nchi ya Uganda kutumia Bandari Mombasa haina uhusiano wowote ule na Tanga, TanZania!
Uganda wanatumia Bandari ya Mombasa kwa sababu za Kihistoria, Wazungu walijenga Reli ya kutoka Mombasa mpaka Uganda kupitia Industrial area ya Uganda, Jinja mpaka Z.Viktoria na ndio maana inaitwa Uganda Railway hivyo kuwafanya Waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa na kutumia ya kwetu siyo rahisi na kujenga Bandari ya Tanga tu peke yake haitoshi ni lazima pia tujenge Reli mpya ya kuunganisha Tanga na Uganda mpaka Jinja sasa hiyo siyo kazi rahisi kwani hai make economic sense yaani kutumia mabilioni ya Dola za Kimarekani kwa ajili tu ya soko la Uganda? usisahau pia kujenga Bandri mpya Ziwa Victoria n.k sasa uwekezaji wote huu kwa mizigo gani ya gani Uganda inayo import na kuexport?
Import Volume ya Uganda ni kiasi gani mpaka iweze kutufanya kufanya uwekezaji mkubwa kiasi hicho?
Jaribuni kujishuhghulisha kidogo kabla ya kulaumu kila kitu, hauwezi kuwafanya waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa na kutumia ya kwetu kwani hakulipi kiuchumi!
Barbarosa tatizo lipo iv.bandari ya dar inatumika hadi kwa mizigo ya kaskazin yaani ni kama bandari ya tanga imekufa.vivo ivyo na ya mtwara kwa kusin wanatumia bandari ya dar.sasa matokeo take tunagawana watumiaji wa kaskazin mwa Tanzania Mombasa na dar kitu ambacho ni kosa.kumbuka kaskazin kuna uwekezaji mikubwa tuu na kuna miji mikubwa.na ukiwa arusha bandari ya Mombasa ni karibu kuliko dar na bagamoyo.sasa kwanini tusiendelee kuboresha tanga kwa ajili ya kaskazin mwa Tanzania na mtwara kusin mwa Tanzania? maana faida ni nyingi kuliko hasara.moja umbali mfupi pili garama ya ujenz mpya wa bandari unakuwa hamna.Hapa tunaongelea Bandari ambayo inasafirisha Mizigo in bulk ya Uganda, kuwafanya Waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa badala yake watumie yetu ni kama haiwezekani kwa maana hatuwezi kufanya huwo uwekezaji, elewa viwanda vikubwa Uganda viko Mji wa Jinja na hapo katikati ambapo ndipo Uganda Railway ilikopita ikitokea Mombasa na inakwenda mpaka Ziwa Viktoria ambako pia kuna Bandari inayoshusha mizigo na kusafirishwa kwa meli, sasa ili kuwafanya watumie Bandari yetu nilazima tufanye uwekezaji wote huwo, sasa kwa mizigo ipi ya maana ya ambayo Uganda wanayo?