Tatizo unasikiliza maneno ya wanasiasa na kuyaaamini na hapa namaanisha wote wa Ug, Ke na kwetu pia! Hawo wanasiasa wote hakuna kitu wanajua wao wanaongea tu kwa kufuata kile watu kama ninyi mnapenda kusikia na maamuzi wanayoyafanya ndiyo yanayokuja kuzigharimu nchi zetu!
Uganda hawawezi kutumia Bandari ya Tanga kwa ajili ya ku-export mafuta yao ni rahisi kihivyo tu!
Pili Tanzania hatuna fedha ya kuwekeza kwenye Ujenzi wa Reli mpya ya ktk Tanga mpka Uganda pmj na Bandari ili kukidhi soko la Uganda, hayo maneno yote unayosikia ya Bandari ya Bagamoyo hizo siyo fedha zetu ni fedha za ktk Uchina na mtoa fedha ndiyo anaamua ni wapi aweke fedha yake sasa kama wamechagua B'moyowana sababu ingawaje sizijui sababu zenyewe!
Tatu kama ukiniuliza mimi Tanzania kwa sasa hatuhitaji reli mpya ya ktk Tanga kwenda Uganda bali tunahitaji kwanza kuzijenga upya Reli zetu tulizonazo ili zifanye kazi kwa full capacity kama Reli ya kati iende sambamba na kufufua Bandari ya Kigoma ambayo ilikuwa inashusha mizigo ktk kwenye treni na kuipakia kwenye Meli kwenda Zambia, Kongo na Burundi, kufufua na kuijenga upya reli ya ktk Dar kupitia Ruvu na nyingine ktk Tanga mpaka Arusha, hivyo tunapaswa kuanzia hapo kwanza kabla ya kufikiria kujenga Reli ambayo haipo kabisa sijui mpka Uganda!