Ndugu inabidi kwanza uelewe Historia ya haya mambo kabla ya kuandika tu kwa ushabiki wa kisiasa! Sababu ya nchi ya Uganda kutumia Bandari Mombasa haina uhusiano wowote ule na Tanga, TanZania!
Uganda wanatumia Bandari ya Mombasa kwa sababu za Kihistoria, Wazungu walijenga Reli ya kutoka Mombasa mpaka Uganda kupitia Industrial area ya Uganda, Jinja mpaka Z.Viktoria na ndio maana inaitwa Uganda Railway hivyo kuwafanya Waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa na kutumia ya kwetu siyo rahisi na kujenga Bandari ya Tanga tu peke yake haitoshi ni lazima pia tujenge Reli mpya ya kuunganisha Tanga na Uganda mpaka Jinja sasa hiyo siyo kazi rahisi kwani hai make economic sense yaani kutumia mabilioni ya Dola za Kimarekani kwa ajili tu ya soko la Uganda? usisahau pia kujenga Bandri mpya Ziwa Victoria n.k sasa uwekezaji wote huu kwa mizigo gani ya gani Uganda inayo import na kuexport?
Import Volume ya Uganda ni kiasi gani mpaka iweze kutufanya kufanya uwekezaji mkubwa kiasi hicho?
Jaribuni kujishuhghulisha kidogo kabla ya kulaumu kila kitu, hauwezi kuwafanya waganda waache kutumia Bandari ya Mombasa na kutumia ya kwetu kwani hakulipi kiuchumi!
mbona magari yao yanapitia tanga? pia ni historia?