Lowassa umekuja CHADEMA kwa nia ya Urais au uliipenda CHADEMA kabla?

Lowassa umekuja CHADEMA kwa nia ya Urais au uliipenda CHADEMA kabla?

lowasa atafaa kuwa makamu wa rais au waziri mkuu!, na sio urais

maamuzi yake magumu na rafiki zake ndio uleta mashaka..
 
Objectives za CDM zinamatch na za LOWASSA
So shut up and keep quiet

Objectives hizi unazozisema/kutaka kutuaminisha zimeanza kuwepo toka lini? Let me put this way, Hizi "objective za CHADEMA zinazo match na za Lowassa" zilianza wakati Lowassa anatangaza nia au wa Lowassa 'anakatwa' jina/kabla au baada?

Wakati Lowassa akisema "Hatahama CCM, na ambaye anaona hafai ahame yeye" alikuwa tayari ana objectives hizo?
 
Tafakarini hii scenario

Dr. Slaa alikuwa ni kada mzuri tu wa CCM na alikuwa na wapenzi wengi tu jimboni kwake Karatu waliokuwa na imani naye hadi akashawishika kuchukua fomu ya kugombea Ubunge katika uchaguzi wa mwaka 1995. Pamoja na kushinda kwa asilimia kubwa kwenye kura ya maoni na kuchukua nafasi ya kwanza jina lake lilikatwa kwa hila na vyombo vya juu vya CCM. Kwa sababu hakuridhika na uamuzi wa jina lake kukatwa aliamua kuhama na kujiunga na Chadema na wao wakampokea bila maswali akawa mgombea wao. Swali la tofauti ya itikadi hata halikuzuka, hakuna aliyehoji kama anaipenda Chadema na hakuna aliyetilia shaka lengo lake la kujiunga na Chadema. Kwa kujiunga Chadema na kugombea ubunge, aliiwezesha Chadema kupata mbunge mahiri aliyekuja kuichachafya serikali hadi kila mtu ndani ya Chadema akawa na imani naye. Leo hii Dr. Slaa ndiye Katibu Mkuu wa Chadema.

Dupe, mpaka hapo tofauti kati ya kitendo cha Dr. Slaa na Lowassa ni nini? Je wakati huo kama ungekuwepo ungemuuliza Dr. Slaa alichofuata Chadema. Kila binadamu anakuwa na malengo anayotaka kuyatimiza; kwa nini kwa Lowassa iwe ni uroho lakini kwa mwingine isiwe? Kama mtu anaamini ana ndoto ya kuwa Raisi wa nchi hii, kwa nini awekewe mipaka? Mimi ni moja katika watu waliokuwa mstari wa mbele kumpiga Lowassa vita, lakini maadam katubu na kuamua kwa hiari yake kuungana na UKAWA, ambao lengo lao kubwa ni kumuondoa huyo mkoloni mweusi, zimwi lililotutafuna toka tupate uhuru, genge linaloamini lina hatimiliki ya utawala ndani ya nchi hii...kama kuja kwa Lowassa kutaongeza hamasa kwa wana mageuzi kuviondoa hivi ving'ang'anizi, mbaya iko wapi? Pamoja na hilo kuna hili la tofauti ndogo ndogo kuibuka UKAWA, kama ujio wa Lowassa umepoza hali hiyo machozi ya nini?

Mimi Mag3, na declare, sikumpenda Lowassa lakini siipendi CCM zaidi. Lakini hebu tujiulie baada ya Lowassa kuachia ngazi, ni tofauti gani tunaweza kujivunia? Je ufisadi umepungua? Tumeshuhudia tangu aondoke Raisi wetu akishindwa kutulia nyumbani na kila siku ni kiguu na njia ughaibuni, nani ndani ya CCM ameweza kukemea huo utapanyaji wa kodi zetu? Sana sana naona kuondoka kwa Lowassa serikalini kuliwapa mwanya zaidi mafisadi walioiteka CCM na hivyo taifa kuingia kwenye kashfa baada ya kashfa, mikataba mibovu kushika kasi zaidi, vijana kuzidi kukosa adabu na kudhalilisha wazee kwa sababu tu baba zao wako madarakani. Hapana Dupe, kama hurudhiki na yanayotendeka UKAWA, funga virago. Ujio wa Lowassa kwa sasa umefunika anga ya siasa, umezidi kuitangaza UKAWA lakini kubwa kuliko yote umezima kabisa moto waliotoka nao mafisadi Dodoma, macho na masikio yote ya Watanzania ni UKAWA!
 
Mag3,

..nakubaliana na hoja zako 90%.

..10% nisiyokubaliana nayo ni pale wzna ukawa wanaposema asiyekubaliana na ujio wa lowassa afunge virago aende zake.

..ukawa inahitaji ku-retain watu wake, na kuongeza walioko nje.

..hoja ni kwamba Lowassa amejiunga na ukawa. Siyo ukawa imejiunga na lowassa.

..ndani ya ukawa lowassa ataendana na miiko na maadili ya ukawa.

Tumaini Makene, Chademakwanza
 
Last edited by a moderator:
Mag3,

..nakubaliana na hoja zako 90%.

..10% nisiyokubaliana nayo ni pale wzna ukawa wanaposema asiyekubaliana na ujio wa lowassa afunge virago aende zake.

..ukawa inahitaji ku-retain watu wake, na kuongeza walioko nje.

..hoja ni kwamba Lowassa amejiunga na ukawa. Siyo ukawa imejiunga na lowassa.

..ndani ya ukawa lowassa ataendana na miiko na maadili ya ukawa.

Tumaini Makene, Chademakwanza
JokaKuu, asante kwa angalizo na nakubaliana na wewe 100%.
 
Last edited by a moderator:
.......
-Lowasa ulietuhumiwa katika kashfa za uuzwaji wa lanch ya taifa…!!, Mvua za Thailand na Richmond pia leo kirahisi tu unatujibu watanzania mwenye ushahidi apeleke mahakaman…?? .......

...
Mag3, EL kafafanua kidogo ishu ya Richmond, lakini hajafafanua hizo hapo mbili (Redbolded), kuhusu ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana ambalo UVCCM walilalamika EL kuingilia mchakato, kitendo cha kusumbuliwa mwanafunzi aliyemuuliza juu ya kuwa na vyeo vingi...alipokuwa kanda ya Ziwa na mambo mengine makubwa makubwa na madogo madogo. Dupe anaweza kuwa na hoja ila kaileta kwa stahili ya 'kinyongo kinyongo'....

Mimi si mkatahi Lowassa kuingia CDM/UKAWA ila sikubaliani na yeye kupewa jukumu la kuiwakilisha UKAWA kwenye uchaguzi kwanza kwa uadilifu wake usiyoridhisha na pamoja na yeye kutotambua malengo hasa ya UKAWA na sera ,katiba na kanuni za Chadema. Waweza kulidhibitisha hili kwa kuchambua maelezo ya EL tangu ajiunge na UKAWA/CDM pale alipopewa nafasi, hakuna sehemu ametumia ama maelezo ya jumla juu ya nukuu ama vifungu vya malengo ya UKAWA ama vya Katiba ya Chadema kama kumbukumbu yangu iko sahihi. Hii si sahihi....!
 
Back
Top Bottom