Kongamano la Fursa za TEHAMA kati ya Tanzania na DRC kuanza Kesho Lubumbashi
Na Innocent Mungy, Lubumbashi.
Kongamano la Fursa za Kibiashara na Uwekezaji katika sekta ya TEHAMA linafanyika kuanzia kesho tarehe 18 na 19 Oktoba 2022, jijini Lubumbashi DRC likiwa na kauli mbiu ya “Kukuza Fursa za Mashirikiano, Biashara na Uwekezaji katika sekta ya TEHAMA”.
Wageni Rasmi katika Kongamano hilo ni Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Augustin Kibassa Maliba, Waziri wa Posta, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Washiriki zaidi ya 300 wanatarajiwa kushiriki Kongamano hilo la siku mbili. Taasisi za Tanzania zinazoshiriki ni pamoja na TAnTRADE, TTCL, Shirika la Posta, Mamlaka ya Serikali Mtandao.
Tanzania, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki na TPSF.