NgerukeAbra
JF-Expert Member
- Sep 5, 2022
- 4,253
- 5,789
Habari za ndani zina sema mwezi wa sita mwishoni ujumbe wa CCM ukiongizwa na watajwa hapo juu utaelekea Marekani ili kuitetea serikali ya CCM kwa mauaji yaliyotokea October 29 30 na 31 pamoja, uminywaji wa demokrasia na uhuru wa kujieleza, utekaji, kuuwawa na kupotezwa kwa watu kwa kipindi kisichopungua miaka kumi.
Kwanini Lucas Mshamba?
Taarifa zinadai huyu ni mwanachama mwaminifu na ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja kiasi cha kulishawishi bunge la seneti kuacha kupitisha mswada ambao utaiwekea vikwazo Tanzania ikiwa utasainiwa na Raisi wa Marekani.
Kwanini Lucy Mikael?
Huyu ni mkatoliki safi na mcha Mungu anaaminika ataweza kutetea hoja ya serikali kuwa inafanyakazi pamoja na kanisa katoliki na kuna maelewano makubwa sana.
Pia serikali inaruhusu maandano kwani wakatoliki waliandaa maandano kwenda ubalozi wa Vatican bila kuzuiwa au kupigwa mabomu ya machizi na jeshi la polisi.
Kwanini BAKWATA?
Ujumbe wa BAKWATA ni kuonyesha kuwa hakuna tofauti kati ya taasisi za kidini na serikali.
Hapo wataliaminisha bunge la seneti kuwa taasisi zote za kidini zinafanya kazi pamoja na serikali ya CCM.
Kwanini Mwalimu?
Huyu ataelezea uwepo wa demokrasia nchini Tanzania na uchaguzi huru kwa kuwa yeye aligombea uraisi katika uchaguzi ulioshirikisha vyama vya siasa takribani kumi na saba.
Kwanini Yona wa Chalinze?
Huyu anaenda kama mwananchi wa kawaida na inaaminika atalishawishi bunge la seneti la Marekani kuwa Tanzania kuna uhuru wa kutoa maoni na wananchi asilimia 98 wanampenda Raisi na ndio maana walimpigia kura.