Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kama kichwa cha huu uzi kinavyojieleza, ndugu Lucas Mwashambwa, Sio bure kazi unazozifanya za kukichafua Chama Cha Demokrasia na Maendeleo zinaonyesha kabisa wewe ni mtu ambaye umetumwa na unalipwa hatufanyi kutoka rohoni, nikirejea uzi wako wa jana kuhusu Makamu Mwenyekiti wa Chadema ndugu Tundu Lissu kutumia majukwaa yasiyo kuwa imara ule uzi niliu copy na ku paste WhatsApp ili ni usome mstari kwa mstari nimesoma zaidi ya mara tatu nikagundua una tatizo sehemu maana una chuki ambazo hazina maana yoyote. Tundu Lissu anachokifanya ni kutoa elimu ya uraia kwa Wananchi na haijalishi anatumia Jukwaa la aina gani as long as elimu imewafikia Wananchi. Sasa ndugu Lucas Mwashambwa unapoonyesha chuki kwa mtu ambaye hakusaidii chochote hiyo ni matumizi mabaya ya chuki. Wewe hata hakujui na inawezekana huwa anakusoma tu humu Jamiiforums. Hilo liangalie CHUKI NI UCHAFU MOYO kosoa kwa kujenga hoja zenye tija Mkuu. Lengo la Lissu ni kutoa elimu sio kusimama kwenye majukwaa kama yanayotumiwa na Katibu Mkuu wa Chama Tawala na anachokizungumza hakina tija wala manufaa kwa ustawi wa maisha ya Mwananchi wa Kawaida.
Na mwisho wa ule uzi wako unakisifia Chama cha Mapinduzi na Raisi kwa hoja nyepesi kama tissue yaani unachokifanya kusifia Chama Tawala ni sawa na kuisifia na kuishukuru ATM Machine kukupa hela pale unapoenda ku withdraw na wakati hizo ni hela ni za kwako. Hata kama unalipwa hebu jaribu kuwa unaandika hoja zenye mashiko maana umekuwa ni mtu mwenye kuandika vitu visivyo kuwa na tija katika ulimwengu wa watu wenye access ya taarifa mbalimbali hapa duniani.
Nawasilisha