Kuna siku hawa waheshimiwa watadai mtanganyika asioe mzanzibar kwa sababu wao ni wachache bali waoane wao kwa wao.
Mimi siamini kama kuna watanzania wengi kihivyo wanaotaka ardhi zenji. Personally nisingependa kuishi sehemu ninayobaguliwa kila siku na ukikaribia uchaguzi ndio scape-goat wa kila baya! Nadhani umefika wkt sasa watanganyika walioko zenj warudi nyumbani mara moja na wazenj tulionao huku pack n go. Kama watapenda 'nchi yao' iombe uanachama East Africa Community. Ilikuwa ni makosa sana kuungana wa watu wenye historia ya machafuko, chuki and all evils.
Juzi juzi waganda wamegundua mafuta na Museveni ametoa wito wa kuona East Africa inanufaika na mafuta hayo.
Watanganyika tumenunua mafuta miaka nenda rudi, tusitishwe na "mafuta" ya kufikirika. Then tuangalie namna tunavyo weza kutumia umeme wetu kujibu mapigo kama Russia wanavyoitumia gesi yao "kikamilifu".
Zanzibars should be treated just like any foreigner. There should be no let up!
Mimi kwa sasa ninaishi na kufanya kazi hapa Zanzibar; ninaomba ku share experience niliyoipata juu ya mambo haya yahusuyo Muungano.
Kwanza ningeanza na historia fupi ya kufika kwangu hapa Zanzibar. Nimekuja hapa Kisiwani mwishoni mwa mwaka 2003. Baada ya kumaliza Diploma Course ya Computer Science. Nilikutana na rafiki yangu ambae alinieleza juu ya nafasi ya kazi iliyopo hapa Zanzibar. Ilikuwa kufundisha computer katika private institute, nilikuwa tayari kuja Zanzibar kwani niliona hiyo kuwa ni Oppurtunity. Nilipofika na kuripoti kwa mwajiri wangu; nilikuta Computer 3 ndani ya chumba kidogo sana na nikaelezwa hilo ndilo darasa la Computer (Computer Lab).
Kwa kuwa nilijifunza kutumia fursa vizuri niliona kwangu hiyo ni FURSA. Nilianza kazi na baada ya mwezi mmoja tulikuwa na wanafunzi wengi na kufanikiwa kuwa na computer Lab yenye 8 computers.
Lakini kwa sasa nafanya kazi katika field nyingine.
Hivyo basi kwa sisi tuliopo hapa Zanzibar kutoka Tanganyika tuliona fursa zilizopo na kuamua kuzichangamkia. Ukienda stone town vijana wanajihusisha na shughuli za kuuza vinyago na bidhaa nyinginezo kwa watalii, asilimia kumbwa ni kutoka Arusha. Vijana wengi kutoka Tanganyika wanakuja hapa kufanya field katika hotel na wanaona fursa zilizopo na wanaamua kuomba ajira katika hoteli hizi.
Ni kweli kuna mazingira ya kutokutazamwa vyema kwa watu tunaotoka Tangayika katika maeneo ya kazi hata makazi. Tunaonekana kama wageni tuliokuja kuchukua nafasi za watu tena kimabavu.
Haya nimeyashuhudia katika kipindi nilichokuwepo hapa Zanzibar; kwani kuna wakati wazanzibari hawa hueleza kile kilichopo ndani ya mioyo yao tena kwa hasira na uchungu.
Lakini jambo nililogundua katikati ya Wazanzibari ni UBINAFSI na UVIVU, kwa sababu hiyo wanashindwa kuchangamkia fursa zilizopo hapa kisiwani na hata zile zinazopatikana katika Muungano. Badala yake wamekuwa ni watu wa kulaumu wakati wote.
Ni Wanzanzibari wachache sana walioziona fursa zilizopo katika Muungano na hawa ndiyo wale wanaofanya biashara kariakoo na sehemu nyingine za Tanganyika. Bakhresa ameona fursa hiii na ndiyo maana amejikita Tanganyika.
Wazanzibari wengi wenye shida na Muungano ni wale ambao hawajawahi kutoka Zanzibar tokea wazaliwe na inawezekana kundi hili kuwa ni kubwa.
Nashauri politician kuwaelimisha zaidi wazanzibari juu ya fursa zilizopo katika Muungano. Ningeshauri wizara ya Elimu iwe ya Muungano ili kutoa fursa ya vijana kuchaguliwa na kwenda kusoma Tanganyika na wa Tanganyika kuja kusoma Zanzibar, hii itasaidia kwa Wanzaibari kupanua ufahamu wao na kujua kwamba Mungu aliumba Dunia ili tuweze kuitawala. Maana wazanzibari wengine wanafikiri kama Unguja na Pemba iliumbwa na Mungu kwa ajili yao tu.
Hapa Zanzibar shida sio siasa bali ni Mindset ya Wazanzibari yenyewe ambayo inatakiwa kubadilika.
Natamani Muungano kuvungika na nikimuona BAKHERSA na viwanda vyake waki - pack na kurudi Zanzibar na magorofa mengi yaliyopo Kariakoo yakihamishwa na kuletwa Pemba.