Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
we jamaa unautani nasisi kabisa ahahahahah aika ruaaaa eti meku bon to safa mbeeee ila all in all moshi wanijua rege kuliko bongo fleva
Mkuu ukisoma haya mashairi utagundua kitu
Lucky Dube Lyrics
"Good Things"
There will be a time in your life
When you'll need me the most
But I won't be there
There will be a time in your life
When you won't need me at all
I won't be there
But while I've got the chance
I'm gonna tell you what I know
About this world we're living in
It may seem so beautiful
From where you are
It may look so innocent
In your eyes
But let me tell you
It's not a bed of roses
[Chorus: x3]
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don't come to those who wait
I can sit here and teach you
Every trick in the book
But at the end of the day
It is your life
[Chorus: x3]
Good things come to those
Who got out and made them happen
They don't come to those who wait
Dah, embu ngoja niutafute, ujumbe wake umenigusa kwenye kuamua na kutenda.
Hizi lyrics unapata wap man.....nahtaj xnSo far so good, still we are living today.
We don know about our tommorrow please, in this crazy world.
People are dying like flies, everyday.
You read about it in the news, but you don't believe it.
You'll know about it, when the man in a long black coat, knock on your door, cause it is his next victim.
Zipo tu mtandaoni wewe search jina la wimbo ongeza neno lyricHizi lyrics unapata wap man.....nahtaj xn
Hizi lyrics unapata wap man.....nahtaj xn
Bado nipo wakuu, japo sionekaniR I P LUCKY DUBE TUNAKUKUMBUKA SANA
Bado nipo wakuu, japo sionekaniR I P LUCKY DUBE TUNAKUKUMBUKA SANA
Wewe mzee wewe mi bado nipoLucky Dube anatimiza miaka 10 tangu auwawe kwenye eneo la Rosettenville, Johannesburg Gauteng, Afrika Kusini. Hii ilikuwa tarehe 18/10/2007.
Dube aliyeuwawa akiwa na umri wa miaka 43, alizaliwa sehemu iliyojuliakana kama Ermelo, Transvaal (kwa sasa Mpumalanga) mwaka 1964, Augusti, 3. Wazazi wake walitengana kabla ya kuzaliwa kwake na aliishi na mama yake ambaye alimpa jina la LUCKY kwa maana ya bahati, kutokana na mimba kadhaa kabla kuharibika, hivyo kuzaliwa kwa Lucky Dube ilionekana kama ngekewa au bahati.
Pamoja na ndugu zake wawili Thandi na Patrick, Dube alitumia muda wake mwingi wa utotoni na bibi yake, Sarah wakati mama yake alipokwenda kazini. Mwaka 1999 kwenye moja ya interview yake, Dube alimuelezea bibi yake kama 'kipenzi chake kikuu' ambaye alifanya kazi kubwa ya kumlea, na kumkuza Dube.
Kuanza Muziki
Katika umri wa utotoni, Dube alifanya kazi kama mtunza bustani na kadiri alipokuwa akikua, aligundua kuwa kipato alichokuwa akikipata hakikutosheleza kuilisha familia yake, ndipo Dube alianza shule. Katika mazingira ya shule alijiunga na kikundi cha muziki kilichoitwa The Skyway Band. Alijifunza na kufuata imani ya kirasta akiwa shule, na alipofikisha umri wa miaka 18 Dube alijiunga na na kundi la muziki la binamu yake lililojulikana kwa jina la The Love Brothers, ambalo lilipiga muziki wa Kizulu aina ya mbaqanga. Akiwa na kundi hilo, waliweza kuingia mkataba na kampuni ya muziki Gallo Music.
Dube, alivutiwa zaidi na muziki wa Jimmy Cliff na Peter Tosh toka Jamaica, na ndipo safari yake ya kuimba muziki wa reggae ilipoanzia. Mwaka 1984, alirekodi album ndogo ya reggae iliyokwenda kwa jina la Rastas Never Die, hata hivyo album hiyo haikufanya vizuri ambapo iliuza nakala 4000 (elfu nne) tu ukilinganisha na mauzo yaliyofanyika kwenye muziki wa mbaqanga ambapo aliuza hadi nakala 30,000 (elfu thelathini) tu. Akiwa mwenye shauku kubwa ya kupiga vita ubaguzi (ant-apartheid), kupitia muziki na tungo zake mbalimbali, serikali ya kibaguzi ya wakati huo ilipiga marufuku album yake mwaka 1985 kutokana na mashairi ambayo yalionekana kuikosoa serikali ya kibaguzi. Hakukata tamaa, kwani mwaka huo huo wa 1985 aliendelea kuimba muziki wa reggae na aliweza tena kurekodi album yake iliyoitwa Think About The Children iliyompa mafanikio makubwa kwa kuuza nakala na kufikia hadhi ya mauzo ya platinam na kumpaisha na kuwa moja ya mwanamuziki maarufu zaidi huko Afrika Kusini na nje ya Afrika Kusini.
Mafanikio
Dube aliendelea kutoa album za reggae ambapo mwaka 1989 alishinda tuzo ya OKTV kwa album ya Prisoner, tena akashinda tuzo kutokana na album ya Captured Live (iliyotokana na onesho la moja kwa moja). Mwaka uliofuata alitoa album ya House of Exile. Mwaka 1993 album yake ya Victims, iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote. Mwaka 1995 alipata mkataba wa kurekodi na Motown moja ya makampuni makubwa kabisa nchini Amerika, ambapo Trinity ndiyo album ya kwanza kurekoodiwa na kampuni hiyo.
Mwaka 1996, alitoa album mjumuisho iliyokwenda kwa jina la, Serious Reggae Business, ambayo ilifanya awe muuzaji bora au mwenye mafanikio kwenye utoaji wa tuzo za World Music Awards an kama mwanamuziki bora wa kimataifa kwenye tuzo za Ghana Music Awards. album zake tatu zilizofuata zilifanya ashinde kwenye tuzo za South African Music Awards. Album yake ya hivi karibuni, Respect, ilisambazwa na kampuni ya Warner Music. Dube amezunguka dunia aki-perform na wanamuziki kama Sinéad O'Connor, Peter Gabriel, Celine Dion, Ziggy Marley na Sting. Mwaka 1991 aliweza kushirki tamasha kubwa zaidi la reggae sunsplash huko Jamaika ambapo aliombwa arudie tena kutokana na umahiri wake na upekee wa aina yake kama mwanamuziki toka barani Afrika.
Kifo chake
Mnamo tarehe 18/10/2007, Lucky Dube aliuwawa jijini Johannesburg kwenye kitongoji cha Rosettenville muda mfupi baada ya kuwashusha watoto wake wawili. Dube alikuwa akiendesha gari ya kifahari aina ya Chrysler 300C, ambayo waporaji walikuwa wakiitaka. Wauaji hao, katika kujitetea, walidai hawakujua na kugundua kuwa aliyekuwa akiendesha gari hiyo alikuwa Lucky Dube bali walijua alikuwa ni Mnigeria. Watu watano walikamatwa kuhusiana na mauaji hayo na walipatikana na hatia hivyo walihukumiwa kifungo cha maisha tarehe 31 Machi 2009. Wengine wawili walifanya jaribio la kutoroka lakini walikamatwa na wote wanatumikia kifungo cha maisha.
Hadi umauti unamfika, Dube alirekodi album 22, na ni moja ya wanamuziki wenye mafanikio makubwa zaidi toka barani Afrika. Katika uhai wake, pia aliwahi kufanya ziara nchini Tanzania mwaka 1997 na kumtania mtangazaji wa kituo cha CTN Rahma Azizi kuwa alimpenda na angependa amuoe. Dube atakumbukwa zaidi kwa nyimbo zake kama vile, Together As One, Prisoner, Reggae Strong, Different Colours One People, Remember Me, Victims, na nyinginezo nyingi.
Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa: wikipedia Lucky Dube - Wikipedia
picha kwa msaada wa mtandao.
View attachment 611411
uko wapi aiseeBado nipo wakuu, japo sionekani