Mzizi wa Mbuyu, mimi ni moja ya mashabiki wakubwa wa muziki wa reggae, na pia ni moja ya mashabiki wa Lucky Dube. Kwa muda mrefu uvumi huo ulinisumbua sana kichwani kwangu, hasa nilivyomjua Lucky Dube kupitia muziki wake. Nilijaribu kutafuta uhusiano wa kimuziki kati ya Dube na Senzo, sikuwahi kuupata, sasa juzi hapa niliporusha hii makala, hilo nalo likaibuka kuwa Dube alimuua Senzo. Hapo ndipo nikapata shauku ya kutafuta tena ukweli wa hilo kwa bahati nzuri ndipo nikakutana na hiyo documentary iliyorushwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015. Kifupi na mimi nimekuja kuujua ukweli juzi tu hapa, ila nyuma ya tarehe 18/10/2017 nilikuwa niko njia panda, na mbaya zaidi hakuna chanzo mfano gazeti ama mtandao wa kuaminika ulioweza kunipa full story ya Senzo. Kitu ambacho nimekuja kugundua ni kuwa uvumi huu ulianzia South Africa kwenyewe. Mbaya zaidi familia yake Senzo haikufanya jitihada kukanusha uvumi huo. Anyway, natafuta namna ya kuuweka ukweli huu zaidi ya hapa ili dunia ijue juu ya hili. Habari mbaya husambaa sana na kuzifuta huwa inachukua muda kidogo.