Lucky or NOT...??

Lucky or NOT...??

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Hi guys!!

Najua kwamba wote tuliomo hapa tumeshaishi na kujifunza mambo mawili matatu kuhusu maisha.
Katika maisha yako so far ni lazima umeshapata mafanikio makubwa au madogo ...umeshashindwa
kwenye mambo makubwa au madogo nk.Yani kwa kifupi umeshaonja matamu na machungu ya maisha
iwe sana au kidogo.

Swali langu ni je mpaka hapo ulipofikia je unajiona/jichukulia kwamba wewe ni mtu mwenye bahati au
mtu asie na bahati???
unlucky-lotto-winners.jpg
Kwanini unajichukulia hivyo??

Nimejisikia kuuliza kwasababu wapo watu ambao hua wanajiona wasio na bahati kabisa mpaka pale
wanaposikia/shuhudia ugumu waliopitia wengine na kugundua kwamba wao hawana haki ya kulalamika m
bele ya hao wengine. Kwahiyo nataka tuweze kushirikishana uzoefu wetu maana nna hakika kila mmoja a
tajifunza toka kwa mwenzake.

C'est la vie
 
nna bahati sana mimi. Nadhani Mungu ananipendelea kabisa.
Nkianza kutaja hapa ntaonekana naringa buree.[/QUOTE]

Nani atakuona bana??

We share kidogo....

Mungu ni mwema kwangu kila wakati, amenipigania mambo mengi, na ni kwa neema zake tu nafanikiwa.
Nadhani kila mtu amepewa neema zake za mafanikio.
Yote kwa yote Mungu ndo mpaji. Tumshuruku kwa kila jambo.
 
Maisha ni kupambana bila kuchoka,mi mwenyewe nimepitia kwenye magumu kiasi kwamba unaona hufanikiwi lakini kutoka na uvumilivu unajikuta unafanikiwa,uvumilivu ukikushinda unatafuta njia mbadala bila na ukiwa na nia utafanikiwa,usikimbie changamoto za kimaisha,ukizikimbia hata utakapoenda utakutana nazo pia.Kwahiyo bila kukata tamaakwenye maisha unaweza ukawa mwenye bahati.
 
Maisha ni kupambana bila kuchoka,mi mwenyewe nimepitia kwenye magumu kiasi kwamba unaona hufanikiwi lakini kutoka na uvumilivu unajikuta unafanikiwa,uvumilivu ukikushinda unatafuta njia mbadala bila na ukiwa na nia utafanikiwa,usikimbie changamoto za kimaisha,ukizikimbia hata utakapoenda utakutana nazo pia.Kwahiyobila kukata tamaakwenye maisha unaweza ukawa mwenye bahati.

Nimependa mtazamo kuhusu maisha ila nadhani unachangiwa na ukweli kwamba umeweza kupigana mpaka ukafika sehemu unayoona umeweza. Ila kwa mtu ambae bado anapigana na mpaka sasa bado hajaona mwanga unadhani anaweza kuchukulia maisha kama ufanyavyo wewe??Maana wewe tayari unajua kwako inawezekana....ila kwa yule asiyejua je?
 
Umeongea kitu cha muhimu sana, usipojilinganisha ama kusikia magumu ya wenzio unaweza ukadhani uimefanikiwa/umefeli. Kama ni mtu wa kuangalia walichotenda wenzio ama walipo unaweza kujipima mwenyewe. Kwangu mie the fact I am in good health,walking in two and with a straight back to date;I feel lucky enough. Its abt the small things that makes up the whole puzzle and I thank god for all that I have. Na kwa ambavyo bado sijavipata,sidhani kama I'm unlucky,ila naamini mungu atanipa timely coz kuna vitu vikivipata hapa huenda vikaniua kabisa! So I strive and wait upon the lord
 
Nimependa mtazamo kuhusu maisha ila nadhani unachangiwa na ukweli kwamba umeweza kupigana mpaka ukafika sehemu unayoona umeweza. Ila kwa mtu ambae bado anapigana na mpaka sasa bado hajaona mwanga unadhani anaweza kuchukulia maisha kama ufanyavyo wewe??Maana wewe tayari unajua kwako inawezekana....ila kwa yule asiyejua je?
Inategemeana na moyo wa mtu jinsi ulivyo,mwingine anaweza akakutana na sitution ngumu na sio mrahisi wa kukata tamaa hata kama haoni mwanga,mwingine ana moyo mwepesi na mlaini kwahiyo hawezi kuchukuliana na ugumu unaomkabili,hapo ndo athari kubwa inapompata.
 
Hi guys!!

Najua kwamba wote tuliomo hapa tumeshaishi na kujifunza mambo mawili matatu kuhusu maisha.
Katika maisha yako so far ni lazima umeshapata mafanikio makubwa au madogo ...umeshashindwa
kwenye mambo makubwa au madogo nk.Yani kwa kifupi umeshaonja matamu na machungu ya maisha
iwe sana au kidogo.

Swali langu ni je mpaka hapo ulipofikia je unajiona/jichukulia kwamba wewe ni mtu mwenye bahati au
mtu asie na bahati???
unlucky-lotto-winners.jpg
Kwanini unajichukulia hivyo??

Nimejisikia kuuliza kwasababu wapo watu ambao hua wanajiona wasio na bahati kabisa mpaka pale
wanaposikia/shuhudia ugumu waliopitia wengine na kugundua kwamba wao hawana haki ya kulalamika m
bele ya hao wengine. Kwahiyo nataka tuweze kushirikishana uzoefu wetu maana nna hakika kila mmoja a
tajifunza toka kwa mwenzake.

C'est la vie

Pamoja na kuwa naweza kujiweka katika kundi la watu wanaojituma sana pia naweza kusema Mungu amenipa bahati kubwa sana na ndio maana namshukuru kila siku iendayo kwake. Kila jambo ambalo nililidhamiria mpaka sasa Mungu kwa uwezo wake ameniwezesha kulifanikisha jambo hilo. Yes, life is GOOD and I can't complain.

Last edited by a moderator:
Nimejisikia kuuliza kwasababu wapo watu ambao hua wanajiona wasio na bahati kabisa mpaka pale
wanaposikia/shuhudia ugumu waliopitia wengine na kugundua kwamba wao hawana haki ya kulalamika m
bele ya hao wengine. Kwahiyo nataka tuweze kushirikishana uzoefu wetu maana nna hakika kila mmoja a
tajifunza toka kwa mwenzake.

C'est la vie

kipimo ni matarajio.......................na kulinganisha na ulichonacho.......................matokeo ni mafanikio au kuyakosa mafanikio...........nionavyo sisi hudhani ya kuwa tuna sauti juu ya maisha yetu.............................lakini ukweli ni kuwa safari zetu zilipangwa na Muumba kabla dunia hii haijaumbwa.......Daniel 4:32-37 na Ephesians 2:10
 
kuna mtu kila kukicha anapenda kusema "lucky is when opportunity meets preparation.." kwa mantiki hiyo nimejikuta nikiamini kuwa siyo kwamba ni bahati bali jitihada pamoja na maandalizi ndo yanayotufanya tuwe pale tulipo, tofauti na hapo tutatumia kauli "sina/huna/hana bahati" kufunika uvivu wetu!
 
bahati... kwan ni sawa na kubarikiwa am totaly confused
unajua bahati zinatofautiana baina ya mtu na mtu mwingine anaweza ona ni bahati ila mwingine kwake ni jambo la kawaida sana
mi nadhani hay mambo yana invisible force anayeya control and we have nothing to speak abt it ..

maana unawezakuta mtu kamwambia mwenzake kuwa una bahati wewe hujafa kwenye ile ajali ... je kifo ni kitu ambacho twaweza kuki control? hapana sasa bahati ipo wapi hapo
infact sijaelewa
 
Wee desh desh haujambo......

In response to your question i don't believe in LUCK, blessings aren't luck, they are blessings. Are there such things as bad blessings? No. Always it is God's will for my life when things go right and when things go wrong it might be because I have made a wrong move, but even then

All things work together for good for those who love God and for those who are the called according to His purpose......... (Romans 8:28) so I would be a fool to believe in luck when I have the Lord at my side. I would be denying the faith and insulting God's Holy Spirit of grace.

There's no luck or chance in my life. It is all of God
 
mimi ninamshukuru mumgu na ninajivunia nina bahati sana
toka asubuhi hadi ninapolala huwa namshukuru mungu kwa yale mema aliyonitendea na anaendelea kunitendea katika maisha yangu
kweli nimemuona mungu akitenda katika maisha yangu tena kwa mambo magumu na mazito ambayo kwangu mimi nilishaona hayawezekaniki kabisa.so kwa kifupi niseme nina bahati sana kupitia yeye anitiae nguvu na kuniwezesha MUNGU
 
Kwa upande wangu namshukuru sn mungu maishan mwangu,japo siamin sn ktk bahati badala yake naamini ktk kujibidisha kukitafuta na kukifanyia kazi nikimshirikisha mungu bila kukata tamaa na siku zote huwa nafanikiwa,japo nimeshapitia magumu mengi namshukuru mungu amekuwa akinionyesha njia ya kutokea na kusonga mbele,siku zote naamin hakuna mafanikio ya kudumu yanayokuja kwa kubahatisha,zaidi ya kujituma kwa bidii na kumwomba mungu.
 
Swali langu ni je mpaka hapo ulipofikia je unajiona/jichukulia kwamba wewe ni mtu mwenye bahati au
mtu asie na bahati???
unlucky-lotto-winners.jpg
Kwanini unajichukulia hivyo??

Nimejisikia kuuliza kwasababu wapo watu ambao hua wanajiona wasio na bahati kabisa mpaka pale
wanaposikia/shuhudia ugumu waliopitia wengine na kugundua kwamba wao hawana haki ya kulalamika m
bele ya hao wengine. Kwahiyo nataka tuweze kushirikishana uzoefu wetu maana nna hakika kila mmoja a
tajifunza toka kwa mwenzake.

C'est la vie

...aisee Lizzy, kwa mtazamo wangu naamini bahati kila mmoja wetu anayake bana....tunatofautiana maamuzi tu.
binafsi naamini, bahati inatokana na uamuzi utaokufanya uwe mahala muafaka, kwa wakati muafaka (the choice of being at the right place at the right time)...na unavyoitumia bahati hiyo...iwe ni tangible, au intangible i.e mapenzi, kazini, biashara nk...

...wengi wetu ni waoga, wazito wa kufanya maamuzi magumu...ikiwamo kujiandaa...!

kuna mtu kila kukicha anapenda kusema "lucky is when opportunity meets preparation.." kwa mantiki hiyo nimejikuta nikiamini kuwa siyo kwamba ni bahati bali jitihada pamoja na maandalizi ndo yanayotufanya tuwe pale tulipo, tofauti na hapo tutatumia kauli "sina/huna/hana bahati" kufunika uvivu wetu!

...spot on!

haya ndiyo niliyoyaelezea awali...

mfano; ....umeshawishika kwa chenji ulizokuwa nazo kununua tiketi yabahati nasibu,
(being at the right place, at the right time)...mungu si athumani matokeo umejishindia zawadi hii;

DSC08088%2B[800x600].JPG

Mkurugenzi wa Lena Event inayoandaa Miss East Africa Lena Calist akionyesha gari aina ya Range Vogue Sport lenye thamani ya dola za Kimarekani 165.000 litakaloshindaniwa katika bahati nasibu ya Miss East Africa...​

...nini yatakuwa maamuzi yako ya mwanzo....
wengi tu weshajishindia bahati nasibu lakini wamefilisika...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
apolo1.jpg
...hawa 'nyoka' wanakamata 'mawe' ya mamilioni ya fedha...ila ndio hivyo tena...wanasafisha jina kwa kununua makreti ya bia kukoshea magari yao wanayoyanunua hapo kwa papo... pesa zikiisha wanarudi migodini kuanza upya kusaka bahati zao..!

waulize vijana wa mererani, mbuguni na kwingineko...ni wangapi wanaobahatika...
kisha jifikirie na tanzania yetu hii tuliojaaliwa 'bahati' ya kila maliasili...taifa bado li masikini.
 
Back
Top Bottom