Lucy Kombani: Watumishi wapya wanaripoti kazini, posho na mishahara vinachelewa, Wizara tatizo ni nini?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Lucy Kombani, amehoji ucheleweshaji wa fedha za kujikimu kwa watumishi wapya, Aprili 17, 2026 Bungeni, kwa Wiara ya Ridhiwani Kikwete ya Wizara wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini Tanzania.

Akichangia hoja hiyo, alieleza kuwepo kwa changamoto kwa watumishi wanaoanza kazi, ikiwemo kukosa fedha za kujikimu pamoja na ucheleweshaji wa mishahara.

"Hili zoezi la kuajiri ni zoezi ambalo linaanza kwa hatua mbalimbali, kwamba tunaangalia sehemu ambayo ina uhitaji wa watumishi, tunatangaza hizi kazi, wanafanya interview na wanaenda kwenye vituo vyao."

"Lakini kumetokea na sintofahamu moja, kwamba mtumishi anaenda kituo chake cha kazi, hela za kujikimu hamna na kuna wengine mishahara wanalalamika inakuwa inachelewa. Wizara iangalie tatizo ni nini kwa sababu mchakato wa kuajiri ni mrefu na unachukua miezi mingi, kwanini linapofika swala la watu kupata hizo hela iwe tatizo?"

"Siku zote jamani hizi ajira hasa za utumishi wa umma kitu cha kwanza mtumishi wa umma ni kumtengeneza mindset yake. Sasa anafika eneo kwa mfano kijijini kama kwetu Malinyi kule Ulanga kule, hela ya kujikimu hana na majibu anayopewa kule atafute namna ya kusurvive. Jamani, mtumishi huyu anakuja na nia nzuri ya kutenda kazi, kufanya kazi, kuhudumia jamii, lakini kwa kitendo tunachomtendea sisi waajiri wake mwisho wake anakuja kukengeuka."

Soma zaidi kuhusu kero za watumishi wapya;
 
malimbikizo ya posho na mishahara ya watumishi wa kada zote nchini yatalipwa kwa wakati muafaka baada ya uhakiki na kuidhinishwa na mamlaka au idara zao.

ni vizuri watumishi kote nchini, wapya na wazamani kua wastahimilivu na wenye subra wakati madai yao yakishughulikiwa na mamala walipoajiriwa.
Kila mtumishi atapata stahili zake bila wasiwasai wowote, na ni muhimu sana waendelee kuchapa kazi bila kuchoka wala kukata tamaa.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Lucy Kombani, amehoji ucheleweshaji wa fedha za kujikimu kwa watumishi wapya, Aprili 17, 2026 Bungeni, kwa Wiara ya Ridhiwani Kikwete ya Wizara wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini Tanzania.

Akichangia hoja hiyo, alieleza kuwepo kwa changamoto kwa watumishi wanaoanza kazi, ikiwemo kukosa fedha za kujikimu pamoja na ucheleweshaji wa mishahara.

"Hili zoezi la kuajiri ni zoezi ambalo linaanza kwa hatua mbalimbali, kwamba tunaangalia sehemu ambayo ina uhitaji wa watumishi, tunatangaza hizi kazi, wanafanya interview na wanaenda kwenye vituo vyao."

"Lakini kumetokea na sintofahamu moja, kwamba mtumishi anaenda kituo chake cha kazi, hela za kujikimu hamna na kuna wengine mishahara wanalalamika inakuwa inachelewa. Wizara iangalie tatizo ni nini kwa sababu mchakato wa kuajiri ni mrefu na unachukua miezi mingi, kwanini linapofika swala la watu kupata hizo hela iwe tatizo?"

"Siku zote jamani hizi ajira hasa za utumishi wa umma kitu cha kwanza mtumishi wa umma ni kumtengeneza mindset yake. Sasa anafika eneo kwa mfano kijijini kama kwetu Malinyi kule Ulanga kule, hela ya kujikimu hana na majibu anayopewa kule atafute namna ya kusurvive. Jamani, mtumishi huyu anakuja na nia nzuri ya kutenda kazi, kufanya kazi, kuhudumia jamii, lakini kwa kitendo tunachomtendea sisi waajiri wake mwisho wake anakuja kukengeuka."

Angalau pamoja na kwamba ni wa vitu maalumu ndani ya lichama la kiuaji lakini anagalau Katoa hoja inayo takiwa kutolewa bungeni tena kwa utulivu mkubwa kabisa na kaeleweka kabisa , hongera mbunge , sio hao vinuka mkojo wengine

Swali: kwani huyu ni mtoto wa celina kombani? ( marehemu)
 
Back
Top Bottom