Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mkoani Njombe, na hasa wilayani Ludewa, uchaguzi umevurugika kwa kiwango cha kutisha.
Awali, katibu wa CHADEMA mkoani Njombe, alieleza kuwa wilaya ya Ludewa ilikuwa ya pili kitaifa kwa idadi kubwa kuenguliwa wagombea wa CHADEMA, ambapo kati ya wagombea 198 wa vitongoji, walienguliwa wote, kati ya wagombea 44 wa nafasi za wenyeviti wa vijiji, walienguliwa 42, na kati ya wagombea 450 wa nafasi za wajumbe, walienguliwa 440. Baada ya rufaa, majina karibia yote yalirudishwa, kasoro wagombea 6.
Kumbe urudishwaji huo wa majina, ambao unatajwa kupewa nguvu na mkuu wa mkoa bwana Mtaka, inaonekana ulikuwa na hila za mbeleni. Mkurugenzi kwa kupitia kamati yake ya rufaa, baada ya kuzikubalia rufaa na kuwatangazia kuwa wagombea wa CHADEMA wamerudishwa, hakuipeleka hiyo orodha kwa wazimamizi wasaidizi, kitendo kilichofanya baadhi ya maeneo kama vile kata ya Luilo, wagombea wa CHADEMA, kuzuiwa hata kufanya mikutano ya kampeni.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Ludewa, Bwana Mapunda, ameeleza kuwa, karibia maeneo yote ambayo CHADEMA ilikuwa ina uhakika wa kushinda kama vile Manda, Ngelenge, Lifua, Ludende na Luilo, majina ya wagombea wote wa CHADEMA, hayapo kwenye karatasi ya kupigia kura.
Kwenye maeneo ambayo wapiga kura wamekuwa wakali kama vile Ludende, msimamizi msaidizi wa uchaguzi amewatangazia wapiga kura kuwa amepewa maelekezo ya kuahirisha uchaguzi.
Kata ya Makonde, mwenyekiti huyo ameeleza kuwa, karatasi za kupigia kura zimeisha, walikuwa wanasuburi kuletewa nyingine, na tayari ilikuwa saa 9 alasiri.
Lifua wapiga kura baada ya kufanikiwa kuzuia uchaguzi kwa kutumia karatasi zenye wagomvea wa CCM pekee, wapiga kura wamegoma kuondoka vituoni kwa hofu kuwa wakiondoka CCM wanaweza kuingiza kura za wizi, wanasema watakuwepo vituoni mpaka saa 12 jioni, na asubuhi saa 12 tena watakuwepo kwenye vituo vya kupigia kura ili kuzuia uchafuzi wa uchaguzi.