Ludewa, Njombe: RC asema wasiolima mazao ya biashara kuwekwa rumande

Soko ndio huwa linaamua kuwa wananchi walime au wasilime.Alishawahi ona wananchi wa Uwemba Matola wanalazimishwa kulima viazi?
 
Napenda kilimo lakini siwezi kulima zao ambalo litanifanya niwe mtumwa wa serikali. Kuna watu mwakajana waliwekwa ndani maeneo ya kusini mwa Tanzania, na wengine kuporwa korosho zao kwa kukutwa wakisafirisha kupeleka kwenye masoko waliyoyataka.

Kwa nini uteseke wewe, ugharamie kila kitu wewe, wakati wote, ila wakati wa mauzo, ulichokihangaikia huna uhuru nacho? Kati ya mazao ambao inabidi ufikirie sana kabla ya kuyapanda ni korosho. Mkulima wa korosho awamu amekuwa kama kichwa cha mlevi ambachi hata mwendawazimu hujifunzia kunyoa

Zao la biashara ni zao lolote unaloweza kuuza. Hata mhogo, kama unauuza na unakupa pesa, ni zao la biashara. Sasa huyu DC sijui kama anajua tafsiri hasa ya zao la biashara. Huwezi kumlazimisha mtu alime kahawa wakati humpi shamba, humpi mbegu, hugharimii utunzaji na wala humpi soko.

Mwananchi anaweza kushauriwa mazao ya kulima lakini siyo kulazimishwa. Mkulima anatakiwa kuangalia gharama za uzalishaji, uwepo wa soko na bei ya soko. Kisha anaamua alime zao gani.
 
Hakuna njia mbadala ya kuhamasisha wananchi zaidi ya kuwaweka rumande
Hiyo sisi waalimu tunaita kichocheo hasi na chanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…