Lugha kupindishwa kiaina kulikoni?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,753
Reaction score
9,575
Habari zenu

Nimejitokeza hapa kujua jambo moja ambalo watanzania wengi wanalo
kuna dhana moja ambayo imejengeka kwa watanzania kuhusu lugha yetu
ya kiswahili na misemo, nahau na sentensi zake kiujumla,
imekuwepo tabia ambayo watanzania wengi wanayo ya kupindishia misemo,
nahau, na dhima nzima ya lugha yetu na isiweze kuleta maana mahali pale
panapostahili maana hiyo kutumika zaidi, wengi wao huwa hawaelewi ni
mahali gani naweza kutumia lugha fasaha kwa matumizi ya eneo hilo
kwa mfano: Mtu anataka kitu benki, au dukani au mahali popote badala ya
kutumia neno fasaha mahali hapo yeye atatumia neno la mtaani mahali hapo
na kuondoa dhana na heshima ya mahali hapo:

matamshi au misemo inayotumiwa mitaani inaingizwa hadi sehemu stahiki
ambazo aghalabu huwezi tumia lugha hiyo mfano (oya! lete hapa kitu kamili,)
nitwangie baadaye, sasa hivi niko benki) opoa sasa kitu kipya hicho chajileta,
Haya ni maneno au misemo ya mtaani hayapaswi kuwepo maeneo stahiki
kama hapo. Vijana wengie wameharibikiwa siku hizi kwa misemo ya kiajabu
ajabu ambayo haina radha hata kuisikia masikioni kwani masikio yanawasha
mara mtu atamkapotamka maneno hayo. Hivyo wapendwa marafiki zangu hebu
jifunzeni kuwa wastaharabu kwenye matumizi ya misemo, lugha na maneno
yetu yalete munyu mahali stahiki panapotakiwa.
Nawapenda nawatakia jioni njema.


copy: Mamndenyi, Lady doctor, watu8, Bujibuji, Mtambuzi, Mentor, amu, Erickb52, Bishanga, Mr Rocky, Filipo, Ruttashobolwa, The secretary, Jiwe Linaloishi, monaco, Preta, marejesho, Heaven on earth, Passion Lady, FirstLady, Fixed Point, Paloma, Excellent, Dancani, Asprin, Kipaji Halisi, Mwita Maranya, Bakulutu, mwaJ, Arushaone na marafiki wengine
niliowasahau
 
Last edited by a moderator:
Mtazamo wangu ni kuwa ukitaka kujua ustaarabu au niseme Tabia za mwanzo za mtu,hutumia haya maneno ya kijiweni sehemu isiyohusika.....hapo utajua huyu ni mstaarabu kiasi gani,na hata upendo pia utaupima kwa kuona matamshi yake yasivyo na staha/sahihi.....hii huonyesha pia Mtu wa kutamka maneno hayo huonyesha kukosa msimamo ujasiri,kwa hiyo anatafuta ujasiri kwa kuonekana/eti aonekane mjanja kumbe kichwani ustaarabu F.Kitokakcho nje kimeanzia kuumbwa ndani.....
 
ladyfurahia hivyo vinaitwa ni vijimisemo, au maneno ya msimu ona hivi nimevidesea mahali:
[h=3]Tutafakari haya....Misemo ya Kiswahili[/h]


  • Waninunia mie.....umekosa mwenyewe magoli ya penati utayaweza ya kona.......

  • Japo chungu we meza tu....

  • Kufika utafika hata kama ukitembea....

  • Mola nipe jicho la tatu linijaze ufahamu....

  • Aliyekuonjesha kaweke kambi kwake.....

  • Eti kuku wa kuchora....hawiki, hatagi yai wala hadonoi.....
  • Unaacha nyama nyumbani unaenda kula mishikaki baa....
  • Umezoea cheko la nyundo hebu tupe la msumari sie nginjha nginjha....

  • Uko busy airport unasubiri meli na hata passport hujabeba.......

  • Umeumbwa u-kanga unataka u-kuku.....

  • Uko busy kama unapiga deki bahari.....

  • Japo chungu we meza tu......

  • Donda la maskini hupona kwa umande.....


  • Kobe hufika aendako hata akienda taratibu......

  • Usijifanye unachagua wakati bado unachaguliwa......

  • Hata tausi mrembo lakini haliwi nyama....

  • Mbwa mzee hafundishwi sheria mpya.....

  • Ingekuwa rahisi hata samaki angetafuta perfume......

  • Aaahhh papai kubwa ka-apple kadogoo...bei ya apple sasa, papai halina maana....

  • Uniniletea perege mie, hicho kidagaa....niletee yule papa ndio saizi yangu

  • Hukushiba kwa tonge, utashiba kwa kulamba....

  • Ukimuona kobe juu ya mti ujue kapandishwa......

  • Madogo madogo yakupite na makubwa yakusakame....

  • Huwezi kuwa mkwezi ukashindwa kusuka pakacha......

  • Mchele kisoda, nazi sita.....

  • Usipaki fuso kwenye gereji ya bajaji...

  • Usipite kimyakimya uliza njia usije ukajigonga buree...

  • Muwasho wa ulimi, haukunwi na kidole....

  • Kama bahari.....ukiweka lindo kaskazini wenzio kusini wanavua....

  • Mzoea punda, hapandi farasi.....


  • Bora kandambili kuliko mdundo mbovu....

  • Unavua samaki kwa mikono, utamaliza kesho.....


  • Ukibipu tu, mi nakupigia.....

  • Una maswali mengi, kwani we ni polisi.....

  • Unaniongelesha kizungu, umenisomesha wewe......


  • Mchuma janga, hula na wa kwao.....

  • Zege halilali.....

  • Ukimjua adui yako unamshinda kirahisi.....


  • Unapanda basi la bagamoyo wakati unaenda ikwiriri.......

  • Uko kama majani ya chai, hujulikani kama dawa ya ngiri au ya kichwa.......

  • Ameshakuwa kuku wa kwenye jokofu, kapoteza radha..........
 
Last edited by a moderator:

Ukimaliza hilo, tafadhali lizungumzie hili la watu wazima kutokujua matumizi ya vituo.

Nini hii, aya nzima kubwa hivi kukosa kituo kikubwa hata kimoja?
 
Huwezi kuamini kwamba haya maneno yanatoka kinywani mwa MCHAGA...
Kweli kinyonga huakisi mazingira aliomo...
 

  • Muungwana hasafiri na maiti bila kutoa chozi......
  • Hukupendeza harusini utapendeza msibani?.....

 
Yani hapa umenena mwana kile kimtokacho mtu ndicho kilivyo kwa uhalisia wa nje
 
MM NIMEIPENDA HII KITU HAPA NIMEPASTE
  • Uko busy kama unapiga deki bahari.....
 
mhm! ngoja nimwachie Mtambuzi hapo
Ukimaliza hilo, tafadhali lizungumzie hili la watu wazima kutokujua matumizi ya vituo.

Nini hii, aya nzima kubwa hivi kukosa kituo kikubwa hata kimoja?
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi si umeona eeh,
tunabadilika badilika kulingana na mazingira,
.... Mtambuzi nakupa huu hapa ............Uko kama majani ya chai, hujulikani kama dawa ya ngiri au ya kichwa.......

Huwezi kuamini kwamba haya maneno yanatoka kinywani mwa MCHAGA...
Kweli kinyonga huakisi mazingira aliomo...
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…