ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,753
- 9,575
Habari zenu
Nimejitokeza hapa kujua jambo moja ambalo watanzania wengi wanalo
kuna dhana moja ambayo imejengeka kwa watanzania kuhusu lugha yetu
ya kiswahili na misemo, nahau na sentensi zake kiujumla,
imekuwepo tabia ambayo watanzania wengi wanayo ya kupindishia misemo,
nahau, na dhima nzima ya lugha yetu na isiweze kuleta maana mahali pale
panapostahili maana hiyo kutumika zaidi, wengi wao huwa hawaelewi ni
mahali gani naweza kutumia lugha fasaha kwa matumizi ya eneo hilo
kwa mfano: Mtu anataka kitu benki, au dukani au mahali popote badala ya
kutumia neno fasaha mahali hapo yeye atatumia neno la mtaani mahali hapo
na kuondoa dhana na heshima ya mahali hapo:
matamshi au misemo inayotumiwa mitaani inaingizwa hadi sehemu stahiki
ambazo aghalabu huwezi tumia lugha hiyo mfano (oya! lete hapa kitu kamili,)
nitwangie baadaye, sasa hivi niko benki) opoa sasa kitu kipya hicho chajileta,
Haya ni maneno au misemo ya mtaani hayapaswi kuwepo maeneo stahiki
kama hapo. Vijana wengie wameharibikiwa siku hizi kwa misemo ya kiajabu
ajabu ambayo haina radha hata kuisikia masikioni kwani masikio yanawasha
mara mtu atamkapotamka maneno hayo. Hivyo wapendwa marafiki zangu hebu
jifunzeni kuwa wastaharabu kwenye matumizi ya misemo, lugha na maneno
yetu yalete munyu mahali stahiki panapotakiwa.
Nawapenda nawatakia jioni njema.
copy: Mamndenyi, Lady doctor, watu8, Bujibuji, Mtambuzi, Mentor, amu, Erickb52, Bishanga, Mr Rocky, Filipo, Ruttashobolwa, The secretary, Jiwe Linaloishi, monaco, Preta, marejesho, Heaven on earth, Passion Lady, FirstLady, Fixed Point, Paloma, Excellent, Dancani, Asprin, Kipaji Halisi, Mwita Maranya, Bakulutu, mwaJ, Arushaone na marafiki wengine
niliowasahau

Last edited by a moderator: