Lugha ya kichaga kupotea miaka kadhaa ijayo wachaga hawafunzi watoto wao hii lugha adhimu

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Katika sehemu ambayo lugha ya asili zitapotea kwa kasi ni moshi

Yaani tofauti na jamii nyingine ni nadra sana kumkuta mzazi wa kichaga akibonga na mwanae kilugha hapa nazumgumzia wazazi wa sasa hivi na watoto waliozaliwa kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa

Tamaduni nyingi africa zinakufa ila walau zingebaki lugha za asili basi lakini kwa wachaga imekua tofauti

Nizipongeze jamii nyingi za tz kwa kuendelea na utamaduni mwema wa kurithisha watoto wenu lugha za asili kama nyenzo mbadala za mawasiliano

Pia wachaga wengi wakiwa mjini wanajifanya waswahili na kwamba hawajui kichaga (wanaona aibu, wanavunga kuzungumza kichaga) watakwambia hawajui hususani wasichana

Ee mungu wa israel tuhurumie watoto wetu na vizazi vyetu
 
Kuna mkakati ulikuwa wa kufunza watoto Mila na kujenga makumbusho kila mtaa ndani ya wilaya ya hai pamoja nakuandika vitabu vya mila
 
Mie ningependekeza wachaga watengeneze dictionary yao kidogo ingesaidia watu wafahamu baadhi ya maneno yao
 
Mie mama ni mchaga...lakini na ukubwa huu hata kukiongea sijui nakiskia tuu. Nadhani shule inachangia sana kukipoteza kichaga.
 
Katika sehemu ambayo lugha ya asili zitapotea kwa kasi ni moshi

Yaani tofauti na jamii nyingine ni nadra sana kumkuta mzazi wa kichaga akibonga na mwanae kilugha hapa nazumgumzia wazazi wa sasa hivi na watoto waliozaliwa kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa

Tamaduni nyingi africa zinakufa ila walau zingebaki lugha za asili basi lakini kwa wachaga imekua tofauti

Nizipongeze jamii nyingi za tz kwa kuendelea na utamaduni mwema wa kurithisha watoto wenu lugha za asili kama nyenzo mbadala za mawasiliano

Pia wachaga wengi wakiwa mjini wanajifanya waswahili na kwamba hawajui kichaga (wanaona aibu, wanavunga kuzungumza kichaga) watakwambia hawajui hususani wasichana

Ee mungu wa israel tuhurumie watoto wetu na vizazi vyetu

Hakuna kitu kama Lugha ya Kichaga Dunia hii, acheni kujidanganya!
 
Huwa najiuliza nchi kama USA sio kila mtu alienda na lugha yake lakini baada ya intermarriage watoto wanazaliwa watajua tu lugha ya taifa, ndio huko tunakoelekea mimi natokea Mbeya na mke wangu anatokea Arusha hapa mtoto ataishia kujua Kiswahili tu
 
Back
Top Bottom