Ili lugha ife, sharti ipitie haya...
Kwanza...Language Attrition, hii hutokana na wazungumzaji wa lugha ya asili, au lugha mama (mother tongue language) kuanza kuchanganya misamiati toka lugha ya pili (L2).
Pili......Language Shift, hii ni hatua ambayo wazungumzaji huamua kuipa kisogo lugha yao na kuanza kuzungumza lugha ya pili (L2) kwa kasumba ya kuwa lugha hiyo ya pili (l2) ni lugha ya wenye hadhi.
Tatu.....Language death, hapa ndipo lugha hufikia ukomo wake kwa sababu kunakuwa hakuna mzungumzaji tena wa lugha husika. Lakini haya yote hayaji tu kama mvua, bali ni mchakato wa muda mrefu sana.
Mwandishi umesema kuwa, wazazi wa Kichaga hawaongei na watoto wao lugha hiyo, sijajua hao wazazi wakiwa wapi. Je, ni huku mijini au huko kwao Moshi? Kama ni mjini, inatakiwa uelewe kuwa, mjini alikozaliwa mtoto, si rahisi kwa mzazi kuzungumza naye (mtoto) Kichaga kwa sababu lugha ambayo mtoto amekuwa exposed ni Kiswahili na Kiswahili kwa mazingira haya nndiyo first language ya mtoto. Kama ni huko Uchagani wazazi hawazungumzi lugha hiyo na watoto wao, I'm skeptical about that, kwa sababu Wachaga walio wengi ambao mimi nimekuwa nikiwashuhudia huzungumza sana lugha yao wakiwa hapa hapa mjini. Kadhalika umesema Wachaga hawapendi kuzungumza lugha yao hapa mjini, nadhani huzungumzii Wachaga naowajua mimi. Wachaga naweza kusema ni moja ya makabila yanayotukuza lugha yao sana, hawaoni aibu kuitumia lugha yao.
Ningeshauri ufanye utafiti kwanza ndipo uje na andiko lako. Maana andiko lako limepwaya sana.