Lugha ya Kichina na utamaduni wa Kichina vyapata umaarufu miongoni mwa wanafunzi wa Ghana

Lugha ya Kichina na utamaduni wa Kichina vyapata umaarufu miongoni mwa wanafunzi wa Ghana

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1784166742625.png


Bertha Asiedua Boadu, mwanafunzi kijana wa Ghana, alianza kupenda kutazama filamu za Kichina mwaka 2020. Ili kuelewa hadithi za filamu bila kutegemea (subtitle) yaani tafsiri zinazopita chini ya filamu, mwanafunzi huyo alianza kutumia programu za kujifunza lugha ya Kichina mtandaoni ili kujifunza Kichina cha msingi.

Kitu alichoanza kama udadisi tu wa kutaka kujua haraka kikageuka kuwa cha kuvutia, na kumfanya aanze kujifunza kuzungumza Kichina peke yake huku akivutiwa zaidi na lugha na utamaduni wake.

"Nilikuwa nikifanya mazoezi ya kuzungumza peke yangu. Kidogo kidogo nikaanza kugundua jinsi lugha hiyo inavyovutia," Boadu alisema.

Kuvutiwa na utamaduni wa Kichina pia kulimfanya mwanafunzi huyo kutafuta fasihi kuhusu utamaduni wa Kichina mtandaoni, akizingatia aina za vitabu ambavyo Wachina walisoma tangu utotoni, ikiwa ni pamoja na The Analects of Confucius, vinavyojumuisha maneno ya mwanafalsafa wa Kichina Confucius.

Kutokana na hatua hiyo ya ujasiri, Boadu sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Cape Coast.

"Wakati mwingine huwa naandika hati moja ya Kichina mara 10 au 15 na bado siwezi kuipatia, jambo ambalo hunikasirisha sana. Lakini walimu wangu wanakuja kunitia moyo. Jambo hilo limenifundisha kuwa mvumilivu," alisema.

Mnamo Mei 22, Boadu alishinda tuzo ya mshindani bora katika kipengele cha chuo kikuu kwenye Shindano la Daraja la Kichina la mwaka huu linaloandaliwa na Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah, akipata tiketi ya kuiwakilisha Ghana katika shindano la kimataifa baadaye mwaka huu nchini China.

Hadithi ya Boadu ilionesha lugha ya Kichina inazidi kuongeza furaha miongoni mwa wanafunzi wa Ghana.

Prince Amissah, mtoto wa miaka 12 katika Shule ya Ubunifu ya Winged huko Cape Coast, ambaye aliibuka kama mshindi bora wa jumla katika ngazi ya shule ya msingi katika shindano hilo, alisema kwamba namna ya kuandika hati za kichina na jinsi ya kutamka maneno na kuunda sentensi yote ni mambo yanayomvutia sana.

Kadri wanafunzi wengi wanavyotaka kujifunza Kichina katika nchi ya Afrika Magharibi, Taasisi tatu za Confucius nchini Ghana zimekuwa zikianzisha njia bunifu za kushughulikia usambazaji duni wa walimu wa Kichina.

Mapema mwezi Mei, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana ilizindua mradi wa darasa la mtandaoni na washirika wa ndani ili kupanua ufikiaji wa elimu ya lugha ya Kichina nchini.

Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Cape Coast (CIUCC) inasimamia ukuzaji wa mtaala wa kitaifa wa lugha ya Kichina ili kuhakikisha kwamba lugha hiyo inafundishwa kote nchini Ghana katika siku za usoni, alisema Emmanuel Amo Ofori, mkurugenzi wa CIUCC kutoka Ghana.

"Kupitia hilo, pia tunawafunza walimu wengi wenyeji lugha ya Kichina ili kwenda kufundisha ndani ya shule mbalimbali nchini Ghana. Tunatumai kwamba ndani ya miaka mitano hadi kumi ijayo, tutawafunza walimu wengi zaidi wa Kichina kuchukua jukumu la kufundisha na kufunza wanafunzi wa Kichina," Ofori alisema.


Source: China Daily
 
Huenda pia ukawa ni mkakati wa chinese soft power kuiteka kifikra elimu ya Afrika ili kuirahisishia China kupata upendeleo wa kibiashara, mikataba, na kuungwa mkono kisiasa katika majukwaa ya kimataifa, huku ikipunguza ushawishi wa nchi za Magharibi Afrika.
 
Malcom Little x aliwahi kusema kwamba "if you dont stand for something, you gonna fall for anything" na hao ndiyo waafrika kila siku kudandia kesho watahamia vietnam, baada ya hapo utasikia wanajifunza hindi au arab ...
 
Back
Top Bottom