Lugha ya kiswahili itakufa? Nasikia watoto wa english medium hawakijui

Lugha ya kiswahili itakufa? Nasikia watoto wa english medium hawakijui

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Juzi nimeona mtandaoni mama mmija akilalamika kuwa mwanae wa miaka 8 hajui vizuri kiswahili. Mwingine anasema mwanae anaongea kiswahili kama cha wahindi.

Hili ni jambo zuri au ni tatizo? Hii ipo kwa kiasi gani? Kiswahili kinaenda kufa?
 
Haiwezekani, uwiano/ratio inagoma kabisa.
 
Wakati anampeleka huko shule yeye alijua anaenda kujifunza nini ?

Na huko mitandaoni anamlalamikia nani ?
 
Akija anaongea kiswahili tupu utamuelewa kweli wakati umelipa kamilioni kako akasome english medium?
 
Hata wasukuma hawajui vizuri kiswahili, nimesoma nao mpaka form iv, wanachapia sana.
So ajabu mtoto anaeshikiwa fimbo asiongee kiswahili kutwa nzima asijue kiswahili.
Binafsi huwa nikitembelea zile shule huwa navihurumia sana vile vitoto, uhuru wao umetekwa na wazazi,walimu na ajira.Masikini! watoto wanakuwa watumwa katika nchi yao.
Wazungu walipowafikisha watumwa Marekani, waliwakataza wasiongee lugha zao na kuwapa majina mapya ya mabwana.
 
Kama lugha za asili zimekufa kwa hivi vitoto vinavyozaliwa na kukulia mjini, tukiendekeza uzwazwa na kiswahili kitakufwa kabisa...
 
Wazazi wenyewe wanaona fahari vitoto vyao vikiongea kizungu,shule kutwa nzima vinabonga kizungu vikirudi nyumbani wazazi badala wawaongeleshe kiswahili wanawaongelesha kizungu,huyu mtoto lini ataongea lugha mama?:siku kitoto kikipelekwe kwa bibi nanjilinji ni full lugha gongana tu!
 
Tatizo kiswahili kina walimu wawili, mmoja shuleni mwingine mtaani ,

Mwl: washuleni amefundisha neo Lakini
Mwl: wamtaani anafundisha neno Rakini

Necta ikifika ni 0 tu
 
Juzi nimeona mtandaoni mama mmija akilalamika kuwa mwanae wa miaka 8 hajui vizuri kiswahili. Mwingine anasema mwanae anaongea kiswahili kama cha wahindi.

Hili ni jambo zuri au ni tatizo? Hii ipo kwa kiasi gani? Kiswahili kinaenda kufa?
Hata marehemu jiwe alikuwa hajui kiswahili vizurii,Ni kisukuma tu, hakuna jipya hapo.
 
Juzi nimeona mtandaoni mama mmija akilalamika kuwa mwanae wa miaka 8 hajui vizuri kiswahili. Mwingine anasema mwanae anaongea kiswahili kama cha wahindi.

Hili ni jambo zuri au ni tatizo? Hii ipo kwa kiasi gani? Kiswahili kinaenda kufa?
Wenye kiswahili tupo busy kukitupa na wenzetu huko Uganda wana taman sasa kuongea kiswahili 😀😀😀😀
Tbc 1 wamerusha kipindi jana na leo cha kiswahili wakiungana na UBC
 
Wenye kiswahili tupo busy kukitupa na wenzetu huko Uganda wana taman sasa kuongea kiswahili [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Tbc 1 wamerusha kipindi jana na leo cha kiswahili wakiungana na UBC

Kiswahili sanifu kipo Pwani na sio Bara, nikisema pwani kama vile Mombasa, Zanzibar, Lamu na kwengineko. Ama Bara kama vile Mwanza, Chato na kwengine. Watu wa Bara hawajui lugha ya Kiswahili na ndio wanaochafua lugha yetu. Kila siku maneno ya kiajabu ajabu, “kifirio” ndio nini kama si tusi.
 
Haiwezekani, uwiano/ratio inagoma kabisa.
Ni kweli hata bila ya kufanya utafiti bado hesabu zinagoma kabisa maana kuna maeneo hakuna shule za English medium.
Labda nyumbani kwake au kwa jirani yake Kiswahili ndiyo kinaenda kufa.
 
Back
Top Bottom