Mfano mzizi wa neno "Como" unapatikana katika lugha hizi mbili zote.
Ila Spanish ni tamu kuliko Portuguese!
Português unaijua? Português iko poa kabisa maneno mengi hayakupi shida ya Português ukifahamishwa kutoka kwenye English
Mfano WA maneno ya English yaliomalizia na
tion mfano communication kwa kwenye português unatoa
tionunaweka
ção na kuwa
communicação kwahiyo viirabu vyenye cento yaani zenye alama mfano ç,ã,á n.k kama hujaskiliza mtu anaeongea kwa kuandikiwa tu ukasoma hujui inavyotamkwa.
Ukiamua kuifuatilia lugha hii lazima ujipinde maana ni ngumu kiasi fulani.
Pia kwa kwenye português neno
COMO lina maana ifuatayo:
COMO kwa maana ya kwanza inamaana ya kuuliza jambo mfano como está?= how are you=Hali yako? Kwenye English kwa neno hili ni
How.
Maana ya pili ya neno
COMO hapa inatokana na kitendo
KULA kwahiyo neno hili linatumika kwa nafs ya kwanza umoja tu yaani Mimi ndio inayoniuhusu na si nafsi nyengine mfano
Eu como arroz com carne de cabrito na minha casa =Mimi huwa nakula wali na nyama ya Mbuzi nyumbani kwangu. Kwa kwenye English hapo tunasema ni tense ya simple present.
Pia kwenye hiyo sentensi hapo juu neno
minha likiwa na maana ya
-angu hayo maneno yapo mawili moja ni hilo minha likiwa na sifa ya uke na jengine ni
Meu likiwa na sifa ya uume yote yana maana sawa ila yana sifa zake kwenye utumiaji.
Kwa hayo machache samahanini.