Ndugu Thesym,
Inaelekea ujui unachokiandika na historia yako umejifunza Wikipedia. Nakushauri usome vitabu, la sivyo giza lililotanda kichwani mwako halitatoweka. Ndio maana mzungu alitutawala na anapenda watu kama nyinyi.
Inawezekena kabisa kwamba bado nina giza kichwani mwangu ndio maana naitaji majibu ya maswali niliyouliza na ningependa kuvijua hivyo vitabu nijifunze zaidi.
Umesema:
Ukitoa lugha za aUkitoa lugha za afrosemitic languages kama vile
Amharic - Wikipedia, the free encyclopedia na
Egyptian language - Wikipedia, the free encyclopedia ambazo kiujumla hizi zipo kwenye kundi moja na lugha kama hebrew, arabic, phonician, aramaic,asyriac nk. lugha karibia zote za kiafrika hazikuwahi kuwa na alphabet zake zenyewe asilia,
Hapa kwanza hujui unachokiandika. Lugha ya kale ya misri ( ancient Egyptian) ambao waliokuwa wanaiongea ni waafrika kama wewe na mimi
Hili mkuu mbona nalifahamu, jaribu kupitia post kwenye thread hii nilivyowajibu baadhi ya watu na nimeadress kabisa kwamba wengi wa wamisri ya sasa ni wageni sio original natives wa hilo eneo, na nimejaribu pia kuelezea maana ya neno moors na sudan, kwa hilo nalifahamu vizuri kabisa.
ndio CHANZO CHA ALPHABET ZOTE ZINAZOTUMIKA SASA HIVI. Kwa hiyo, bila wamisri , tusingeweza kuandika maneno haya. Alphabet ilianzia misri wakakopi waphoenician, baadae wagiriki wakokopi hiyo , romans, wakakopi kwa wagiriki,branch nyingine za maandishi kama kiarabu, Ethiopic, mereoitic( sudan) mpaka saanksrist hizi zote shina lake ni ancient Egypt. kwa kifupi, bila mwafrika, mzungu hajagundua alphabet hata moja.
kwanza kabisa hapa sizungumzii wazungu tu pekee yake, nimejaribu kuadress jamii tofauti mpaka zile za mashariki ya mbali.
rekodi za kale kabisa mpaka sasa ambazo zipo za kimaandishi zinaonyesha vitabu vya kahindi ni miongoni mwa script za kale na dini yao ndo ya kale kabisa zina miaka zaidi ya 5500, sasa mkuu iweje useme egyptian alphabet ambazo manuscript zake zipo zinazoenyesha zina miaka 4500 ndio useme ni chanzo cha alphabet zote tuzionazo sasa mbona hakuna manuscript ya kale kuizidi hao wahindi toka kwa egypt na japokuwa rekodi za wamisri ya kale zipo, mkuu hivi unafahamu jinsi ya korean alphabet zilivyotokea?
ukiangalia watu weusi huku africa huwezi kuta records za kale ambazo zimeandikwa kwa herufi ambazo ni tofauti hizi roman alphabet ama arabic alphabet tofauti tu na michoro ya mapangoni, historia yetu inakuja kuanza moja moja kuja kwa wageni kiasi cha kwamba kama vile afrika haikuwepo, ni ngumu kukuta records zilizoandikwa labda miaka 1500BC kwa sehemu kubwa africa tofauti na zile nchi ambazo ni afro semitic kama ethiopia.
Ujui unaloliandika. Chanzo cha lugha za semitic ni afrika. Semitic ni tawi la lugha zinazoitwa Afroasiatic, lakini chanzo cha lugha hizi zote ni afrika. na hili limethibitishwa na wataalam.Yaani afrika kuna diversity kubwa za lugha za afroasiatic kuliko mashariki ya kati ndio maan wataalamu wakaconclude kwamba hata semitic chanzo chake ni afrika lakini ilikuja kuenea nje ya afrika na kuzaa Arabic. Ukienda Ethiopia utakuta Geez na tigriya ambazo pamoja na lugha nyingine za semitic ambazo zimeshakufa.
Hapana hilo nalifahamu kabisa ninachokiandika, semitic languages zote ni tawi la afro asiatic(hapo kwenye mada yangu niliandika kimakosa kama afro semitic)., kuhusu hilo ambalo umedai linawezekana likawa hivyo lakini naomba nikuulize
hizo ni dokument za sumerian za mesopotamia language ambazo ziliandikwa 3rd millenium BC ambazo kimakadirio ni kama miaka 5000 za wamisri ni kama miaka 4500, hizo nazo zina root zake misri ya kale? hapa sijagusia wachina.
Umesema:
mi natoa challenge kama kuna mtu anaweza weka records za tanzania hata 100BC aweke. hii inamanisha ni kwamba afrika ustaarabu umechelewa kufika lakini cha kushangaza kuna watu wanasema watu weusi(waafrika) walishawahi tawala dunia nzima na hata ulaya kwamba mababu zetu ndo walifundisha sasa cha kushangaza hata kabla ya european renaissance karne ya 15 sikuwahi kubahatika kumsoma ama great thinker yeyote ambaye ni mweusi au mwafrika, lakini utakuta wachina, wagiriki, waarabu, wakorea, wahindi,wayahudi wapo na rekodi zao zipo na wanajulikana hizo lugha zote na nyingi ya nchi za asia lugha zao zina alphabet zake
Najibu:
Naomba uende library utafute kitabu cha historia ya Afrika, halafu urudi hapa.
Ungenipa jina la mwandishi ili nijaribu kukitafuta hiko kitabu
Umesema:
….asilia na rekod zao zimeandikwa na wao wenyewe na si mtu baki kwa kutumia herufi za lugha zao wenyewe. kwa mfano tunasoma mwaka 2500BC wanajimu wa kichina walirekodi tukio la kupatwa kwa mwenzi hili ndilo tukio la mwanzo la kupatwa kwa…
Nasema:
Tatizo wewe ukiona kitu chochote cha maana Afrika unakitoa, na kusema sio afrika. Egypt, Ethiopia na sudan kwa mfano ni Afrika, kwanini unazichomoa hizi nchi kuzitoa afrika?
Mimi ninachorabu kusema na kujiuliza kwa nini sehemu kubwa ya afrika tofauti na egypt, ethiopia hapakuwa na namba na alphabet zao wenyewe ambazo wangetumia kuweka rekodi zao wenyewe, yaani historia yetu ni kama tumeandikiwa. Hivi mkuu kwa mawazo yako unadhani tofauti na hizo tawala mbili hapakuwahi kuwa na great thinker hata hapa tawala za kale tanzania? lakini kwa nini huwezi kukuta maandishi ya kale kama kielelezo?
Ukiangalia kitabu cha zamani cha medicine na mathematics( Kahun papyrus), kwa mfano kiliandikwa kabla hata chinese civilisation haijaanza.
Sina tatizo kabisa kuhusu uwezo wa misri ya kale ila kusema iliizidi umri chinese civilization sina uhakiaka nalo maana hapa vyanzo vilivyopo nilivyoviona text za hizo rekodi zinaonyesha ni 1800 BC, labda unipe chanzo kingine cha uhakika nipitie.
Ndugu, soma kwanza vitabu vya linguistics, archeology and historia ya afrika, unaweza kuanzia na kitabu cha ‘The African origin of Civilisation’ cha Cheik anta Diop, hiki kinaelezea vizuri historia ya Afrika na jinsi wazungu waliipindisha ili wapatikane watu wa kuwadanganya kama wewe.
Ok, nitatafuta hiko kitabu, kuhusu hilo swala la wazungu kuiharibu historia hapo ndo huwa nachoka hivi kwa nini wahindi mbona historia yao na ustaarabu wao mbona haukuwai kuharibiwa, wametawaliwa na waarabu miaka zaidi 1000 na wakaaribu temple zao za mda mrefu na masanamu yao baadae wakaja wakatawaliwa na waingeleza lakini historia yao ipo pale pale na ancient rekodi zao zipo na wale scientist wao wa kale rekodi zao zipo kama kawaida sasa iweje waafrika tu ndio wenyewe historia yao, ustaarabu wao na vitu vingine viharibiwe kiasi cha kwamba tukaletewa utamaduni mwingine kabisa na kujikuta ghafla tuwe na ignorance?.