Mafwi Munda
JF-Expert Member
- Nov 30, 2017
- 1,750
- 1,603
Habari zenu wana bodi.
Huwa najiuliza maswali lakini sipati majibu lakini leo naomba nanyi mnisaidie.
Tanzania tuna makabila mengi na haya makabila yanaongea lugha tofauti. Lakini pia tunaongea kiswahili. Swali langu ni hili ilikuwaje tuweze kuongea lugha tofauti lakini tukashindwa kuwa au kuweza kuandika hizi lugha zetu kwa HERUFI zetu?! Yani makabila yote tulijua kuongea lakini hakuna hata kabila moja liliweza kuwa na herufi za maandishi yake?! Angalia Ethiopia wana herufi zao,wahindi wana herufi zao,wachina wana herufi zao, warusi wana herufi zao,sweden wana herufi zao waingereza wana herufi zao. Sisi Tanzania tulishindwa au tulitegemea ugunduzi wa wazungu kutuwekea vitu vyetu kwenye kumbukumbu na kwakuwa hawakuziweka kumbukumbu inamaana hatukuwa na herufi zetu kweli?!
Je, tunaweza kutengeneza herufi zetu leo au ugunduzi uliishafungwa?! Ikiwa tunaweza kugundua leo, je kumeshawahi kufanyika utafiti wa kuanza kutengeneza herufi zetu au ugunduzi ni wa kiteknelogia tu lakini sio maandishi(herufi)?!. Kwa wataalam wa tafiti za lugha kumewahi au wamewahi kuona herufi zozote za kuwakilisha maandishi ya kabila lolote Tanzania?! Je kuna wataalam wale wanaoitwa ma anthropologist wa lugha?! Je wamewahi kutafiti herufi za kuwakilisha mawasiliano ya kimaandishi ya lugha yoyote ya makabila yetu Tanzania?!
Kwa BAKITA kiswahili tunaweza kukiundia herufi zetu mbali ya hizi A to Z?! Je kuna juhudi hizo au mnakuza lugha tu herufi zina mamlaka yake?!
Ni mjadala wa wote kwa yeyote anayejua chochote kuhusiana na hili. Karibuni kwa mjadala.