Wamasai katika mazungumzo ya lugha yao wanaambatanisha pia na gestures au alama inayotambulisha namba (nafikiri zote). Hizo namba nina uhakika ni ya kwao pekee waliobuni wao pekee tangu enzi na enzi.
Kwanini nimesema hivyo? Ni kwasababu sio Wazungu, Wahindi, Wachina ama Makabila yooote ya kibantu yanatumia hizo gestures zao.
Kwahiyo tayari wao wana asili yao ya Ubunifu wa ishara za mawasiliano zaidi ya sauti pekee ila si Kiuandishi.
Kuhusu lugha ya kimasai pia nikitrace origin yao sioni zikifanana saaana na kiaramaic ila najua zina asili moja kabisa, hivyo tayari sina ushahidi kuwa kimasai kimekopa maneno kokote kama kilivyo kiswahili na kiingereza.
Hiyo inanifanya nikubali na kuamini kuwa Wamasai tangu enzi na enzi walikuwa wakijisimamia na kuenzi asili yao katika:-
-Lugha
-Mavazi
-Chakula
-Organization / mfumo wa utawala wa kirika (Age-set)
- Style ya maisha kwa ujumla wake.
2) Wabantu ni akina nani?
Ni watu wa Afrika (zamani ikiitwa Ethiopia) ambao wana asili ya kutokea eneo la milima ya Cameroon kwa miaka mingi iliyopita.
Kimuonekano wanaelezewa kuwa weusi, wenye asili ya kunenepa, wenye uso mpana, pua na lips pana, tofauti na wakush, wanilotes etc.
Hawa wabantu walikuja kusambaa katika Afrika yote (kasoro sehemu zilizokaliwa tayari na waarabu, wanilotes, wakush etc.)
Wabantu walioenda upande wa kusini ndio hawa ambao babu zao waliwaza kina Shaka wa Zulu etc
Wabantu wengine waliishi ktkt ya Africa ambao babu zao ndio walioianzisha Zimbabwe ya kina mugabe
Wabantu wengine walibaki cameroon, Ghana, Mali etc
Wengine walienda zaire / congo
Wabantu wengine wakaja mashariki ya Africa na ndio waliozaa makabila ya huku.
Ubantu ulikuja kusababisha aina nyingi sana za Makabila ya asili kama kihaya, kigogo, kipare n.k... ILA historia inakumbusha neno "NTU" kama ndio lugha ya kibantu ikimaanisha Mtu au Binadamu.
Wabantu wa mashariki ya Afrika walipokuja kuungana na Waarabu na Wareno kwasababu ya Dini, Ukoloni au Biashara walizalisha lugha nyingine inayoitwa KISWAHILI lakini uandishi wake si wa kiarabu ila ni wa wazungu waliokuja kufunza watu weusi namna ya kuandika.
● Hivyo kwa mtazamo wangu na uelewa wangu, UBANTU na MAKABILA YAKE haujawahi kugundua namna yake ya mawasiliano (ya kimaandishi au kiishara) zaidi ya SAUTI TU.
Aina za maandishi iliambatana na Formal Education ambayo wabantu waliletewa na Wageni (Wazungu) na aina nyingine ni kiarabu, na hata kirumi katika namba ambazo zinafundishwa katika shule za msingi.
Mfano baada ya kusoma One, two, three mpaka a thousands and Millions tukaambiwa tena ni vizuri tujue haya:
X ni 10
C ni 100
M ni 1000
V ni 5
Hahahaha [emoji23]
Kuna maneno nitakayoyaamini siku zote kuwa:
"Mtu akishaweza kutawala UTAMADUNI WAKO basi amekutawala kila kitu"
Hiki ndicho wakichokifanya watu weupe kwa Wabantu tangu enzi na enzi.
....x.....x......x.....x.....x......x......x.....