Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, ameibua mjadala mzito bungeni kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma, akisisitiza kuwa eneo la matumizi ndiyo mahali pekee ambapo wabunge wanaweza “kukaa kutwa nzima” kuibana serikali.
Akichangia hoja za serikali katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 8, 2026, Lugola amenukuu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2021/2022, akieleza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 637.5 zilipotea katika mamlaka za serikali za mitaa kutokana na ubadhirifu na vitendo vya rushwa.
Amesema fedha hizo zingekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya wananchi kama zingetumika ipasavyo.
“kwa fedha hizo, Darasa Moja tulalijenga kwa Milioni 25, tuna Majimbo 222 kila mbunge hapa jimboni kwake angekuwa na Madarasa 115 na inawezekana ungekosa hata mahali pa kuyajenga”.... lakini kwa fedha hizo hizo Mwaka mpya kila mtu angepata elfu 10,000”
Amesema Kangi Lugola Mbunge wa Jimbo la Mwibara mkoani Mara wakati akijadili hoja za Seikali kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Apili 8, 2026.