SI KWELI Luhaga Mpina alikataa kurudisha fomu baada ya kushinda kesi

SI KWELI Luhaga Mpina alikataa kurudisha fomu baada ya kushinda kesi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu hii imekaaje huko?
Mpina Millard.jpg
Mpina jambo.jpg
 
Tunachokijua
Luhaga Mpina ni mwanachama wa chama cha siasa cha ACT Wazalendo ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, kabla ya hapo Mpina amekuwa mbunge wa jimbo la Kisesa kwa vipindi tofauti.

Mpina alikumbana na kadhia ya kuondolewa na msajili wa vyama vya siasa kuwania Urais kwa kile kilichoitwa ni kwenda kinyume na kanuni za chama chao kwa mujibu wa pingamizi lililowekwa na mmoja wa wananchama wa ACT wazalendo.

Madai

Kuanzia Septemba 12, 2025 baadhi ya taarifa zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Luhaga Mpina akataa kurudisha fomu ya Urais. Taarifa hiyo imeambatanishwa pia na grafiki ya baadhi ya vyombo vya habari.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo kama ilivyowasilishwa na mdau wa Jukwaa hili aliyekuwa akitaka kupata uhalisia wake na kujiridhisha, Si ya kweli.

Kupitia utafutaji kwa njia ya maneno muhimu, JamiiCheck imebaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa wala kutolewa na vyanzo rasmi wala vya kuaminika.

Aidha ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa Luhaga Mpina na mgombea mwenza walirudisha fomu ya Urais, Septemba 13 na kuteuliwa kuendelea na mchakato wa kampeni. Licha ya hilo Mpina pia alikataa kuchukua gari linalotolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa wagombea wa Urais.

Chama cha ACT Wazalendo pia walichapisha taarifa iliyoambatana na grafiki siku ya Septemba 13, 2025 na kueleza kuwa haki imeshinda hii ni kuashirira kuwa mchakato wa kampeni kwa wagombea wake wa ngazi ya Urais utaanza mara moja.

Grafiki ya Millard Ayo na Jambo TV zilizotumika kusambaza taarifa hiyo pia zilikuwa za kughushi kwani hazikutolewa wala kuchapishwa na vyanzo hivyo kama inavyoonekana.
Back
Top Bottom