Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
NIMEMSIKILIZA mtu anayejiita sijui waziri mkuu kivuli.. (vyeo vya kusadikika) ambaye ACT Wazalendo walitaka awe mgombea wao wa urais lakini sijamuelewa kwenye mambo mengi sana
SITAKI kuongelea ujinga wake anaoongea kwenye mambo ya mafuta kwa sababu ni mtu mjinga tu anaweza kupoteza muda kuelewesha jitu zima vile kwa nini mafuta yamepanda bei.. Ni matumizi mabaya ya muda kuanza kuongea na kujadiliana naye kwenye vitu ambavyo viko wazi sana na havihitaji kueleweshwa
DUNIA nzima inapita kwenye shida ya kupanda kwa bei ya mafuta kwa kuwa huko yanakotoka kuna shida na ni principle nyepesi sana ya demand and suppy.. Supply imekuwa ndogo maana yake demand imekuwa kubwa na price ambayo ni factor ya demand na supply lazima inabadilika interchangeably..
KWA hiyo kuona mtu anaongelea mambo ya sijui mafuta nini na anajua kuwa ni shida ya dunia nzima ni mtu mjinga na hahitaji kujibiwa kwa lolote yaani..
LAKINI Mpina amezungumzia eti nchi za Malawi na Zambia zimeacha kutumia babdari ya Dar Es Salaam na sasa wanatumia babdari ya Beira kule Msumbiji.. Sina uhakika kama Mpina huwa anajipa muda kutafiti mambo au anapayuka tu ..
TUTAMSAIDIA kuelewa mambo mepesi sana hapa halafu yeye kama mkulima wa mpunga na mfanyabishara wa mpunga angefanyaje!
ZAMBIA
💡 umbali wa kutoka Beira Port mpaka Lusaka ni 1,050km
💡Roli inasafiri kwa masaa 13
💡Muda wa meli kusubiri kushusha mizigo kule beira ni siku 13
💡Muda wa kuclear mizigo na kuitoa bandarini ni kati ya siku 3-5
DAR ES SALAAM
💡umbali wa kutoka Dar Es Salaam mpaka Lusaka ni 1948km
💡Roli linasafiri kwa masaa 35
💡Muda wa meli kusubiri kushusha mizigo ni siku 1-2
💡Muda wa ku clear mizigo na kuitoa bandarini ni aiku 1-2
SASA huyu mkulima wa mpunga anayejifanya anajua mambo ya uchumi anaelewa jinsi wafanyabiashara wanavyofanya maamuzi wapi wapitishe bidhaa zao?
TUNA wanasiasa wapumbavu sana kwenye mifumo yetu na wanatumia kutokuelewa kwa watanzania kwenye haya mambo na kuanza kuwajaza uongo na porojo..
MPINA ashauriwe ajikite kwenye kilimo cha mpunga maana huko ni eneo ambako anafanya vizuri sana na amekuwa anafanya vizuri sana kwenye kulima siyo kwenye siasa anakokuja na kuleta blah blah kwenye mambo ya maana