Kesi (ya kupitia uhalali wa kisheria kuhusu utolewaji wa vibali vya kuagiza sukari) imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam ambapo mdai ni ndugu Luhaga Mpina, ambao anawashtaki ni Waziri wa Kilimo, Bodi ya Sukari, viwanda vya ITEL, Zenji Industries, Waziri wa Fedha ambaye yeye anashtakiwa kwa kutoa misahama ya kodi ya VAT (Kodi ya Ongezeko la Thamani) ambapo Mpina anadai hata taarifa ya msamaha wa kodi haikuchapishwa katika gazeti la serikali, lakini pia Mpina amemshtaki Kamishina Mkuu wa TRA kwa kutokudai na kukusanya kodi kwa watu waliopewa vibali vya kuagiza sukari lakini wa mwisho kushtakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, shauri hilo liko mahakamani tayari.