Luhaga Mpina apiga kura kukataa azimio la Bunge la kufuta kigezo cha JKT kuajiriwa kwenye Majeshi ya Ulinzi na Usalama

Luhaga Mpina apiga kura kukataa azimio la Bunge la kufuta kigezo cha JKT kuajiriwa kwenye Majeshi ya Ulinzi na Usalama

TAYARI ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI YETU, UTAWEKWA UPYA KATIKA MIZANIA YA JE TANZANIA INAPOTEZA UWEZO WA KUJILINDA?

Azimio hili la Bunge tayari taarifa zake zitaingia ktk makabrasha ya intelejensia ya nchi jirani na za mbali kuhusu uimara, idadi ya jeshi la akiba, morali na moyo wa kujitolea kuipigania nchi

1967, National Service was run by the Tanu Youth League and the Afro-Shirazi Youth League and included "political education".

In 1972 National Service came under the responsibility of the Ministry of Defence. From then onwards, National Service was compulsory for students who completed their secondary education and involved military training and vocational training. National Service lasted three years and was carried out in military camps, with agricultural work as the main activity. [4]

In the past the National Service scheme was seriously resisted by students. [3]

6 Annual statistics​



The armed forces comprise about 34,600 troops - 0.11 percent of the population. [8]

The reserve force (Citizens' Militia) is 80,000 strong. [8]

Every year about 280,000 men turn 18. [8]

Sources​





[1] Eide, A., C. Mubanga-Chipoya 1985. Conscientious objection to military service, report prepared in pursuance of resolutions 14 (XXXIV) and 1982/30 of the Sub-Commission of Prevention of Discrimination and Protection of Minorities. United Nations, New York. [2] DIRB, 29 May 1989. [3] Omari, Abillah H. 1993. 'Beyond the civil-military dichotomy in Africa: the case of Tanzania' in: Siddiqui (ed.), Sub-Sahara Africa: A continent in transition. [4] Abecassis, L., P. Duong, S. Perrier, N. Watt, 1994. Conscription Militaire ou Service National a Option Civique, rapport de l'enquête préliminaire effectuée auprès d'une vingtaine d'Etats membres de l'UNESCO. CCIVS - UNESCO, Paris. [5] Gouault, J. 1995. Service National, quelle options? Serie POUR Avec. GREP Editions/UNESCO, Paris. [6] US Immigration and Naturalization Service 1995. Telephone interview with representative of the Tanzanian Embassy, Washington, 20 March 1995. [7] UN Commission on Human Rights 1997. The question of conscientious objection to military service, report of the Secretary-General prepared pursuant to Commission resolution 1995/83. United Nations, Geneva. [8] Institute for Strategic Studies 1997. Military Balance 1997/98. ISS, London, UK.
 
bunge limeona mbali, imekuwa majeshi yote magereza, polisi, wananchi na zimamoto plus uhamiaji na uokoaji lazima umepitia JKT jambo ambalo si la mhimu. JKT ni kitengo tu ama idara chini ya JWTZ sasa kwanini kiwe ndo pass mark ya ajira kwa majeshi takiribani yote. JKT haliwezi kutumika kama standard form ilihali hata uundwaji wake umeweka bayana ni kwa ajiri ya uzalishaji na si vinginevyo. JKT ni paramilitary section kama lilivyo jeshi la mgambo hivyo kulitumia kama standard ya kupata ajira kwa majeshi mengine ni udwanzi! bunge wako sawa.
 
Mmmh...mbona kama hili azimio ni la mchogo wanataka Majeshi nayo watu waanze kuingia kwa memo..? mpina amestukia mapema huu mchongo lakini naamini JWTZ hawatakubali huu ujinga wataendelea na mfumo wao wa namna ya kuwaandaa askari wake... Tulia kama vijana wako wamekosa nafasi waambie waende JKT huwezi kulitumia bunge kufanikisha maslahi binafsi.... Vyombo vya Usalama fuatilieni kwa kina kujua msingi wa azimio hili kama limekidhiri vigezo msiwaruhusu wanasiasa wasiolitakia mema taifa letu wawe waamuzi wa mambo ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.
kwani kabla ya kigezo cha kwenda jkt vimemo havikuwepo...?
 
Japo sijakubaliana sana na hilo azimio ila kumbuka kuna kitu inaitwa shule ya awali ya mafunzo ya kivita (RTS) kwangu mimi hapo hadi kupavuka wewe ni askari kweli. Kuna wana walipiga NS tena ya volunteer kabisa ila pale kihangaiko walidunda.

Vile vile zipo special intake ambazo watu wanapiga na wanamaliza uzuri wa janx ni kwamba ukifika RTS kuna vitu huwi mgeni navyo milele.
Kuna mengi huyajui mkuu. Kuna mengi tunashuhudia kutoka kwa TS na PT ambayo mpaka kuyawaza unaona uvivu.
 
Wanataka kigezo cha jkt kiondolewe ili waendelee kuingiza watoto wao kirahisi moja kwa moja mwenye ajira
Hii ni Moja ya sababu nyingine ya kuonyesha udhaifu wa Bunge katika kuisimamia serikali kwenye mambo ya msingi...kibaya ni kama Bunge linaipotosha Serikali... Hii haikubaliki kwa vipimo vyote....!!!
 
Maneno haya hapa chini ya mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC kuwa viongozi wengi wenye mamlaka, waongozaji taasisi n.k wameweza kupatiwa mafunzo ya kimkakati ya ulinzi na usalama.

Leo tunaona bunge letu lenye watu wenye mamlaka kuhusu mustakhabali wa ulinzi na usalama wameshindwa kuelewa masomo waliyopewa, huku wengine majina yaao yanaanza na Dr. X ndcmbunge wa CCM au katibu wa bunge Bi. Nenelwa Mwihambi, ndc. Ndc ikionesha ni muhitimu wa mafunzo ya Chuo Cha Ulinzi wa Taifa-NDC

MIAKA 60 YA UHURU, Mkuu wa Chuo Cha Ulinzi wa Taifa-NDC Meja Jenerali Ibrahim Mhona Aeleza Mafanikio


View: https://m.youtube.com/watch?v=YGH4z19yylk
 
Nchi iliyokosa Misingi imara huyumba mara nyingi katika mipango. Nadhani kuna haja baadhi ya maamuzi yanayogusa Usalama wa nchi ni vema yakajadiliwa na kuamuliwa na vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama.

Kama kigezo ni kwa vile sio vijana wote wanaopata furusa za kupita jkt/jku ni bora basi ingeamuliwa vijana wanaochaguliwa kuingia kwenye majeshi husika wapitie kwanza jkt/jku halafu wapikwe na kuchujwa huko kisha watakaofaa ndio waendelee na hatua ya huko walipokusudiwa.

Lakini kama.uzito ni suala la AJIRA na sio USALAMA WA NCHI/TAIFA basi na iwe hivyo kama WALIVYOONA INAFAA.

NINA IMANI HUKO MBELENI WATAKUJA WATAKAOFIKIRIA ZAIDI YA HAYO MAAMUZI
 
hawezi kuhamia kwenye chama kutwa kucha kiko kwenye maridhiano huku wananchi wanateseka na matatizo yao ya umeme, sukari, kupanda kwa maisha wao mda wote wako Ikulu kwenye maridhiano ambayo haiwelezwi wanariadhiana nini wanasahau kufanya kazi yao ya upinzani kama Jicho la kuisahihisha serikali wao wanasaka maslahi binafsi...Mpina hawezi kwenda Chadema hawana mfumo wa kitaasisi ataendelea kuwa mwana CCM muumini wa Katiba ya CCM, aZIMIO LA ARUSHA..
Leo wametoka saa? Ikulu
 
Wanataka kigezo cha jkt kiondolewe ili waendelee kuingiza watoto wao kirahisi moja kwa moja mwenye ajira
Na hii ndiyo sababu kuu ya kupitisha hilo azimio. Baada ya hapo utaona watakavyo jazana kwenye hizo ajira. Hawa jamaa hawana hata chembe ya aibu.

Vijana walioenda kulimishwa kama punda huko JKT ndiyo imekula kwao.
 
JKT hawaendi wahitimu wote wa kidato Cha sita,huchaguliwa baadhi kutokana na ufinyu wa bajeti,Sasa uwanyime wengine wengi fursa ya kuajiriwa wakati wewe ndiye uliyeshindwa kuwapeleka JKT!?
Sheikh umechanganya madesa. Vijana tunao watetea hapa siyo hao wanaokwenda JKT kwa miezi 3 baada ya kumaliza kidato cha sita!

Hawa ni wale vijana wahitimu ambao wapo mtaani. Kwa muda sasa wamekuwa wakijitolea huko JKT kwa matarajio ya kupewa kipaumbele kwenye ajira zinazohusiana na majeshi yetu yote nchini. Kwa hiyo Bunge ndiyo limeondoa hicho kigezo.
 
Sheikh umechanganya madesa. Vijana tunao watetea hapa siyo hao wanaokwenda JKT kwa miezi 3 baada ya kumaliza kidato cha sita!

Hawa ni wale vijana wahitimu ambao wapo mtaani. Kwa muda sasa wamekuwa wakijitolea huko JKT kwa matarajio ya kupewa kipaumbele kwenye ajira zinazohusiana na majeshi yetu yote nchini. Kwa hiyo Bunge ndiyo limeondoa hicho kigezo.
Ok!!
 
Mmmh...mbona kama hili azimio ni la mchogo wanataka Majeshi nayo watu waanze kuingia kwa memo..? mpina amestukia mapema huu mchongo lakini naamini JWTZ hawatakubali huu ujinga wataendelea na mfumo wao wa namna ya kuwaandaa askari wake... Tulia kama vijana wako wamekosa nafasi waambie waende JKT huwezi kulitumia bunge kufanikisha maslahi binafsi.... Vyombo vya Usalama fuatilieni kwa kina kujua msingi wa azimio hili kama limekidhiri vigezo msiwaruhusu wanasiasa wasiolitakia mema taifa letu wawe waamuzi wa mambo ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.
Haya ndiyo matatizo ya vyombo vya usalama kuingiziwa siasa
 
Tujiandae kupata JWTZ legelege zaidi ya sasa
Kwani JWTZ wenyewe watu wao hawawapeleki Depo? Naamini JWTZ, PT, Magereza, Usalama wa Taifa nk huwa kabla hujaanza kazi kuna mafunzo lazima uyafanye kwanza.
 
Bunge limepitisha azimio la kuondoa kigezo cha kupitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa vijana wanaoomba nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama huku Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akipiga kura ya hapana kutounga mkono azimio hilo.

Azimio hilo limekuja kufuatia hoja ya dharura iliyotolewa jana Alhamis Februari 15, 2024 na Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole na kisha Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kutaka kujiridhisha ikiwa Bunge limeshawahi kutoa maelekezo juu ya jambi hilo.

Hata hivyo baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwahi kuwa na maelekezo juu ya jambo hilo alimruhusu Mbunge huyo kutoa hoja ambayo iliungwa mkono na kisha ikajadiliwa na azimio likatoka.

Hata hivyo wakati akitoa hoja ya kuahirisha Bunge Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilitaja azimio kupitishwa na Bunge kama moja ya maazimio yaliyopitishwa kwenye mkutano huu wa Bunge.


JKT, Enzi za mwalimu ilianzishwa kwa lengo la:
1. Kuwajengea vijana uwezo wa kuzalisha Mali kwa kuwapa mafunzo stadi na ujuzi maridhawa.
2.kuwapa vijana mafunzo ya uzalendo na kuwandaa kuwa raia wema wenye kupenda nchi Yao.
3. Kuwa na jeshi la akiba lenye vijana wenye utayari wa kuilinda na kuitetea nchi wakati wa vita.
4. Kulijengea uwezo jeshi la wananchi kwa kuwa na kikosi cha uzalishaji Mali.

Sasa alipoingia Rais Magufuli aliamua kufufua na kuboresha uwezo wa jeshi la kujenga taifa hasa baada ya kubaini kwamba uzalendo umepungua nchini. Ukatengenezwa utaratibu na mkakati na Kisha masuala ya bajeti.
Nini faida yake kwa vikosi vya ulinzi na usalama.
1. Katika mafunzo ya awali na mhimu( basic trainings) inakuwa rahisi kwa wao kuelewa kwa uharaka mafunzo kwani tayari Wana msingi. Hivyo kwa wakufunzi na vikosi huwa vinafaida kwa kuwa na mwendelezo Bora wa kuruta(recruits) hivyo kuwa na urahisi wa kupenyeza mafunzo.
2. Lakini pia vijana Hawa huwa na moyo wa kujituma na wenye nidhamu ya kiaskari( naomba nisisitize hapo nidhamu ya kiaskari kwani kuna tofauti kati ya nidhamu ya mtoto wako na nidhamu ya kiaskari) .
Kwanini wameondoa kigezo hiki?
Nionavyo Mimi siasa imewaingia na mob psychology. Yaani wabunge kama wawakilishi wa wananchi wamesikiliza malalamiko ya wananchi na kuyaleta katika maazimio bila kuangalia umhimu wa JKT.
Lakini pia suala la bajeti inawezekana limeanza kuwashinda kwani yapo malalamiko mno ya vijana Hawa.
Nini nikionacho hapa? Kama ilivyokawaida kwa nchi yetu kuwa kila kitabu na zama zake.
Atakapokuja Rais mzalendo huu utaratibu utarudishwa Tena. Na hii miaka mitano bila kigezo hiki madhara yataonekana kwa wananchi kuanzia barabarani Hadi uhamiaji. Simanishi kwamba sasa hivi hakuna madhara. Yapo lakini yataongezeka zaidi.
Asante Mpina
 
JKT hawaendi wahitimu wote wa kidato Cha sita,huchaguliwa baadhi kutokana na ufinyu wa bajeti,Sasa uwanyime wengine wengi fursa ya kuajiriwa wakati wewe ndiye uliyeshindwa kuwapeleka JKT!?
Naunga mkono hoja hii
 
Back
Top Bottom