Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, mkoani Simiyu, Luhaga Mpina, ameiomba Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia na kupitisha sheria kali, ikiwemo adhabu ya kunyongwa kwa mtu yeyote atakayebainika kufanya ubadhilifu wa mali za umma.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Nyakafuru, Halmashauri ya Mbogwe, mkoani Geita, Mpina alisisitiza kuwa matumizi mabaya ya kodi za wananchi yanawakosesha haki ya kupata huduma bora za kijamii, jambo linalosababisha madhara makubwa kwa jamii.
"Kutokana na mafisadi hawa wachache, bado tunashuhudia vifo vya wajawazito na watoto, wagonjwa wakikosa huduma muhimu hospitalini, elimu duni kutokana na ukosefu wa miundombinu bora ya kujifunzia na kufundishia, huku baadhi ya watu wachache wakigawana na kutafuna fedha hizo kwa tamaa," alisema Mpina.
Aidha, alibainisha kuwa alipowasilishwa kwa mara ya kwanza hoja hiyo bungeni, alikuwa Mbunge wa 121 kujiorodhesha kuunga mkono na hadi sasa wabunge 168 tayari wameunga mkono pendekezo hilo.
"Ninaamini katika Bunge lijalo la bajeti, hoja hii itajadiliwa kwa kina. Rais wetu aliunda tume ya maboresho ya kodi, nami nilichangia kwa kuandika ripoti yenye kurasa 235 kuhusu masuala ya kodi. Ripoti yangu ilibaini kuwa kila mwaka, takribani trilioni 42 zinapotea kutokana na ubadhilifu wa fedha za umma," aliongeza.
"Fedha za umma zikitumiwa vibaya, matokeo yake ni kwamba hospitali hazitakuwa na dawa wala madaktari wa kutosha. Watu wangapi wamepoteza maisha kwa kukosa huduma hizo muhimu? Watoto wangapi wamefariki kwa kukosa damu kwa sababu fedha zinaliwa na mafisadi?" alihoji Mpina.
Mbali na hayo, aliwataka wawakilishi wa wananchi kuepuka kuwa "machawa" wa viongozi wakubwa na badala yake wazingatie kusimamia maslahi ya wapiga kura wao.
Source: Nipashe