Luhaga Mpina ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu Kivuli

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kwa hatua inayotajwa kuimarisha kambi ya upinzani nchini, kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, ametangaza baraza jipya la mawaziri kivuli na kumteua Luhaga Mpina kuwa Naibu Waziri Mkuu Kivuli pamoja na Waziri wa Nishati na Madini.

Uzinduzi wa baraza hilo umefanyika leo Mei 18, 2026 katika makao makuu ya chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mpina ni mwanasiasa aliyewahi kulitumikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu na pia kushika nafasi ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Kujiunga kwake ACT-Wazalendo kulivuta mjadala mkubwa wa kisiasa kutokana na uzoefu wake serikalini na bungeni.
Mwaka 2025, ACT-Wazalendo ilimteua Mpina kuwa mgombea wake wa urais kupitia mchakato wa ndani wa chama hicho.

Pamoja na uteuzi huo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) haikumuidhinisha kugombea katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
 
Uwaziri kivuli bila kiti bungeni is purely theatrical!
 
Ndio maana hawa madalali nilisema siwaamini watu wako kutafuta haki za waliouwawa October 29 wao wako busy na masuala ya vyeo.
 
Eti ndugu zangu wa ACT Wazalendo mnapoteua watu kuwa Mawaziri vivuli, huwa kunakuwa na posho! Au kila kitu kinakuwa kwenye hali ya ukivuli!
 
Kwani azam tv ni channel namba ngapi
 
Back
Top Bottom