GE2025 Luhaga Mpina awajia juu wanaosema kuwa ACT Wazalendo inafanya maigizo

GE2025 Luhaga Mpina awajia juu wanaosema kuwa ACT Wazalendo inafanya maigizo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mgombea urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, ameapa kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi nchini, akisisitiza kuwa hatapumzika hadi Watanzania wote wanufaike na rasilimali za taifa, na chama hicho kipo makini katika kutatua changamoto za Watanzania.

Akizungumza Agosti 9, 2025 akiwa Zanzibar alipokwenda kutambulishwa kwa Wazanzibar, Mpina amesema: "Hatuna mchezo na taifa letu. Hatutapumzika kulipigania mpaka maendeleo yaliyokusudiwa yafikie wananchi. Watanzania hawawezi kuwa wanyonge kwenye taifa lao, hawawezi kugeuzwa manamba na kikundi kidogo cha watu kinachonyonya fedha za nchi hii."

Ameongeza kuwa, kufanikisha mabadiliko hayo, ni muhimu Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla kumpa ushirikiano na kumuunga mkono kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.


 
Alikoenda hawana malengo hayo na Chama chenyewe agenda zao si za kihivyo. Wanauma kidogo, wanapuliza kwa sanaaaaa!!!
 
Back
Top Bottom