Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kivumbi tu! Kutoka kwa Mpina, anaendelea kutapika nyongo haswa
Ila huyu jamaa ni tofauti sana na wanaCCM wengine yani aogopi kupiga panapo stahili
================
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, amesema Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya utakatishaji wa fedha haramu, hali inayoiweka nchi kwenye hatari ya kuingizwa katika orodha ya uangalizi maalum wa Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha (FATF).
Akizungumza na wanahabari kuhusu maoni yake kwa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi, Mpina amebainisha kuwa Tanzania inapoteza takriban dola bilioni 1.5 za Kimarekani (sawa na shilingi trilioni 3.3) kwa mwaka kutokana na utoroshaji wa fedha kwenda nje ya nchi.
Soma Pia: Luhaga Mpina: Wanaomsifia Rais Samia ndio hao wanaoongoza kwa kumhujumu na kufanya uovu
Ameeleza kuwa hivi karibuni kumekuwa na madai ya utoroshaji mkubwa wa fedha unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali, akisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti ili kudhibiti tatizo hilo na kulinda uchumi wa taifa.