DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Mchango wa mbunge wa jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Joelson Mpina (MB) akichangia bajeti ya wizara ya viwanda na biashara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 leo tarehe 14 mei 2025 bungeni Dodoma
Mheshimiwa Spika, Ustawi wa Sekta Binafsi unategemea ulinzi imara wa soko la ndani na udhibiti wa uingizaji holela wa bidhaa kutoka nje ya nchi, uingizaji wa bidhaa zisizo na ubora na usawa katika ufanyaji biashara.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake imeleta maombi ya fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 135.79 ambapo matumizi ya kawaida ni Tsh. Bilioni 93.91 na matumizi ya Maendeleo ni Tsh. Bilioni 41.88 ambapo pendekezo langu la awali, Wizara hii isitengewe fedha kwa kuwa imeshindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu yaliyowekwa kwa mujibu wa Sheria.
Mheshimiwa Spika, Pia niungane na Kamati na Wabunge wenzangu kwa hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Linganga na Mchuchuma ikiwa ni pamoja na kukamilika kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi huo na kuanza mazungumzo na Kampuni ya China ambapo tayari Makubaliano yamefanyika kwenye baadhi ya vipengele muhimu vya mikataba kama mgawanyo wa hisa na muundo wa uwekezaji, kiwango cha mtaji wa uwekezaji na muda wa uwekezaji.
Hii ni hatua nzuri ya kupongezwa.
Changamoto ninayoiona hapa majadiliano yamefanyika hadi kuhitimishwa kwa usiri bila kuuarifu umma kupitia Bunge, Sheria za Maliasili za nchi, Sheria ya The Natural Weath and Resources (Permanent Sovereignty) Act No.5 of 2017 na TEITA Act 2015 ambazo zinakataza usiri wa majadiliano katika miradi ya uziduaji na raslimali zingine za asili.
Taarifa iliyowasilishwa na Serikali haina taarifa muhimu kama tathmini ya mradi na Makubaliano mahususi yaliyofikiwa katika uwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma. Mfano Waziri hakuweka wazi thamani ya Makaa ya Mawe na Chuma yaliyopo, thamani ya uwekezaji na Wajibu wa pande zote mbili, kila upande utapata hisa kiasi gani na namna mapato yatakavyogawanywa, muda wa utekelezaji wa mkataba na kipindi cha mkataba nk.
Hivyo Waziri wa Viwanda na Biashara anapaswa kuliambia Bunge kwa uwazi manufaa ya utekelezaji wa mkataba huo badala ya kutoa taarifa inayoficha mambo muhimu ambayo mara nyingi usiri huu umekuwa ukitumika kama kichaka cha kuzaliwa mikataba Mibovu na isiyo na maslahi kwa Taifa. Pamoja na kusubiri kwa hamu utekelezaji wa Mradi wa Liganga na
Mchuchuma lakini pia hatuweza kukubali kuingizwa kwenye mikataba Mibovu.
Pia katika kipindi cha mwaka 2023/2024 waliopeleka maombi kwenye Tume ya kugawa ardhi kwa ajili ya uwekezaji ni 191 na kati yao maombi hayo 130 sawa 68% ni kampuni ya nje ya nchi na 61 sawa 32% ni makampuni ya Tanzania.
Ushahidi wote unaonyesha kuwa Makampuni na raia wa kigeni wanawekeza zaidi nchini kwa zaidi ya 68% ya uwekezaji unaofanywa kila mwaka. Wizara ya Viwanda na Biashara inapaswa kutoa majibu kwanini tumefikia hapo, nini kinachowafanya watanzania washindwe kuwekeza, kujenga viwanda na kuendesha biashara?
Baadhi ya Wawekezaji wa ndani wanalalamika kunyang’anywa kazi na wageni, hivi karibuni Mfanyabiashara Maarufu nchini na Mbunge Mstaafu wa Igunga, Mheshimiwa Rostam Aziz alinukuliwa na vyombo vya habari akilalamikia wazawa kunyimwa kazi na kazi nyingi kupewa wageni huku akionya kuwa hakuna nchi Duniani iliyowahi kupata maendeleo kwa kutegemea
wawekezaji wa nje pekee. Wizara ya Viwanda na Biashara inapaswa kujibu maswali haya magumu yanayolalamikiwa na wafanyabishara mmoja mmoja na Jumuiya zao za TPSF, TCCIA, CTI, ZNCC, TATOA, TWCC, ACT, TAFOPA, TTMOA ,ATE, TBA, TAMIDA, TSPA, TANEXA, CATA, TASOTA, TASAA, TASSIM, TSA, TWCA, TAA, TUCASA, TEGAMAT, TABOA nk.
Kutoa Misamaha ya kodi kwa bidhaa za nje huku bidhaa za ndani ya nchi zinatozwa kodi. Mfano sukari ya kutoka nje ya nchi imesamehewa kodi ya VAT na Import Duty wakati sukari zinazolishwa nchini zinatozwa VAT. Pia sukari inayozalishwa nchini kulipa ushuru wa Tsh. 50 kwa kilo wakati sukari ya kutoka nje ya nchi inalipa Tsh. 7.8 tu kwa kilo hapa hakuna usawa na kwa vyovyote wazalishaji wa ndani hawawezi kushindana na sukari kutoka nje ya nchi.
Misamaha ya Kodi ya VAT na Kodi ya Mapato kwa wawekezaji mahiri mara nyingi imekuwa ikihusisha Makampuni ya Nje na hivyo kukosesha usawa wa gharama za uzalishaji, Waziri mwenye
dhamana ya Viwanda na Biashara alipaswa kupambania haki na usawa wa biashara nchini.
Nchi yetu, inatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza huduma na bidhaa kutoka nje ya nchi, Mfano kiasi cha Tsh Bilioni 474 zinatumika kuagiza mafuta ya kupikia nje ya nchi kila mwaka, Kiasi cha Tsh. Bilioni 696 kutumika kuagiza ngano nje ya nchi, pia tunatumia zaidi ya Trilioni 1.1 kuagiza mbolea nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Katika Hotuba ya Waziri ameelezea uwekezaji wa Kiwanda cha Mbolea cha Intracom Fertilizer Limited wenye gharama ya Tsh. Bilioni 78.4 kinachozalisha mbolea aina ya FOMI ambapo kikikamilika kitafikisha uzalishaji wa mbolea tani Milioni 1. Pamoja na kiwanda hiki kuanza uzalishaji kwa sehemu kubwa hatununui mbolea katika kiwanda hiki na badala yake tunaendelea kuagiza mbolea nje ya nchi.
Pia ofisi nyingi za umma zimejaa samani za kutoka nje ya nchi mpaka maziwa yanayotumika kwenye ofisi nyingi za umma ni ya kutoka nje ya nchi, ipo mifano mingi ya nchi kugeuzwa soko la bidhaa za nje huku bidhaa za ndani zikikosa soko, kuoza na kuharibika. Katika eneo hili Serikali inatumia fedha nyingi za kigeni bila sababu za msingi na kupoteza mapato ya Serikali.
Hiki kilio ni cha muda mrefu lakini Wizara ya Viwanda na Biashara imeshindwa kutafuta suluhisho la kudumu na kukomesha mambo hayo.
Mfano mwaka 2022/2023 Serikali ilisamehe faini ya 15% ya wafanyabishara ambao hawana vyeti vya CoC na kuondoa ulazima na hivyo kuwa hiari kufanya ukaguzi wa PVoC kitendo ambacho kimeleta madhara makubwa ya kufurika bidhaa feki, bandia na zisizo na ubora katika soko la ndani.
Hali ambayo imeleta madhara makubwa ya kiafya na Kiuchumi. Bidhaa zisizo na ubora kutoka nje ya nchi zimeua ushindani wa haki katika soko la ndani, kufungwa viwanda, ajira kupotea na madhara mengine ya kiafya kwa wananchi. Maamuzi haya yalifanywa bila kuzingatia uwezo wa kitaalamu na kimaabara ya TBS.
Leo tunavyozungumza baadhi ya vifaa vya ujenzi, vipuri na vilainishi vya magari, pikipiki, sukari, mchele, ngano, mbolea, mbegu, viuatilifu, mafuta, vipodozi, vifaa vya umeme, simu, luninga nk vitu hivyo vimeingia nchini vikiwa havina ubora na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi kuhatarisha maisha yao na kuua uchumi na kupoteza mapato ya Serikali.
Taifa na wananchi wanapata hasara kubwa mfano nondo feki ambapo tutakwenda kujenga madaraja na majengo yasiyo na ubora ambayo yataishia kubomoka na kuanguka na kuleta madhara makubwa, vifaa vya umeme ambavyo vimekuwa vikilipuka kila leo na kuunguza mali na kuhatarisha maisha, vipuri vya magari feki vinavyosababisha ajali kila uchao na kusababisha kupoteza maisha kwa wananchi wasio na hatia.
Mheshimiwa Spika, licha ya ukubwa wa tatizo hili sioni dhamira ya dhati ya Wizara ya Viwanda na Biashara kudhibiti uingizaji wa bidhaa zisizo na ubora nchini.
Hivi sasa hali ni mbaya nchi yetu imegeuzwa kuwa dampo la bidhaa feki na bandia na zilizokwisha muda wa matumizi. Na hapa natapa mkanganyiko mkubwa wa fikra kwamba kama Sheria zipo, Mamlaka za udhibiti za TBS, TMDA, FCC, BRELA zipo nini kinachokwamisha?
Kama Sheria zipo na Mamlaka za udhibiti zipo na hali inazidi kuwa mbaya, kuna mambo 2, Moja, kuna Udhaifu mkubwa wa kiutendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi zake, lakini Pili inaweza kuwa biashara hizo ni za kwao na hivyo si rahisi kudhibiti na kujichukulia hatua wao wenyewe.
Hivi majuzi Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliagiza kuundwa Tume ya kuchunguza raia wa kigeni wanaofanya biashara Kariakoo ambapo uchunguzi ulibaini kuwepo kwa raia wengi wa kigeni wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo katika Soko hilo, Jambo la kusikitisha na kushangaza Waziri wa Viwanda na Biashara alikwenda kushughulika na suala hilo moja tu la Kariakoo na kuacha maeneo mengine ya masoko na shughuli nyingine za Kiuchumi kama Uchimbaji mdogo wa madini, uvuvi, viwanda ambako nako kuna raia wengi wa kigeni.
Mfano eneo la wachimbaji wadogo la Bushimangila Msalala, Mwakitolyo Namba 5 Shinyanga, Mavota Ushirombo, Ntambarare Namba 2 Segese, Shilalo Misungwi, Nyamahuna Geita, Iramba Singida, Bugaka Msalala nk maeneo yameuzwa kwa wawekezaji wa Kichina na kusababisha adha kubwa kwa wachimbaji wa wadogo kwa kukosa maeneo ya kuchimba waliyokuwa wanajitafutia riziki huku wakiwa hawana njia Mbadala, na wengine kufukuzwa bila hata kulipwa fidia ya uwekezaji waliofanya na hivyo kupata hasara na kufilisika na kuikosesha mapato Serikali.
Pia kuwepo na migogoro na Malalamiko yasiyoisha katika maeneo ya wachimbaji wadogo ambapo shughuli za uchimbaji zimekuwa
zikisimamishwa mara kwa mara kwa visingizio mbalimbali mfano eneo la Ifugandi Nyang’hwale Geita wachimbaji hao wamepaza sauti bila kusikilizwa.
Maeneo ya wachimbaji wadogo yaliyokuwa yakiajiri watu 10,000 hadi 20,000 na kuzalisha takribani kilo 20 za madini kila mwezi na kuchangia mapato ya Serikali anakabidhiwa mchina mmoja (Raia wa Kigeni) ambaye hamna masharti ya uzalishaji kwa mwezi ni yeye anavyoona inafaa na wakati mwingine hata akaunti zake hazipo hapa nchini na hivyo kupoteza ajira nyingi, kudumaza uchumi na kupoteza mapato ya Serikali.
Wazabuni na wakandarasi kupewa wa kutoka nje ambao wengine hawana sifa, upendeleo, kuvunja Sheria na kuacha njia ya ununuzi ya ushindani ili kufanikisha kupendelea Makampuni ya kigeni.
Zabuni, kandarasi na ushauri elekezi kwenye miradi mingi kwa sehemu kubwa wapewa wageni hata kwa zile ambazo zinaweza kufanywa na wazawa katika sekta mbalimbali na miundombinu ya Kiuchumi.
Mfano sekta ya ujenzi ina makandarasi 14,550 ambapo kati yao 550 ni makandarasi wa nje na 14,000 ni makandarasi wazawa lakini katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wazawa wanapata 46% na makandarasi wa nje wanapata 54% ya thamani ya miradi
hii ina maana kuwa 54% ya bajeti ya Ujenzi inalipa wageni na kwamba miradi yote mikubwa wanapewa wageni na miradi midogo midogo wanapewa wazawa ambao pia wanakopwa miaka nenda rudi hadi kufilisika.
Katika uchambuzi uliofanywa na The CHANZO Initiative Machi 31, 2024 unaonyesha kuwa TANROADS imekuwa ikilipa 95% ya bajeti ya ujenzi kwa Makampuni ya nje katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2024 ambapo imelipa kwa Makampuni ya nje Tsh. Trilioni 11.72 sawa na 95% ya fedha zilizolipwa wakati Makampuni za ndani zikiambulia Tsh. Bilioni 633 tu sawa na 5% tu ya fedha zilizolipwa. Huku Makampuni ya Kichina yakipata fedha nyingi zaidi yakiongozwa na Kampuni ya CCECC iliyopata Tsh. Trilioni 4.9 na Kampuni ya CHICO iliyopata Tsh. Bilioni 920.
Kampuni za Kichina za CCECC, CHICO, CRJE na Synohidro karibu kila mradi wanapewa wao hapa nchini katika miradi ya Barabara, Bandari,Nishati, Maji, Reli, viwanja vya ndege, Madaraja Nk hii inatia uchungu sana kwa wakandarasi wazawa na vijana wa kitanzania wanaotaabika kwa kukosa ajira.
Changamoto hii kwa sehemu kubwa ni kwa Makampuni ya Ndani kwani Makampuni ya nje yamekuwa yakilipwa pamoja na riba kufidia ucheleweshaji wa malipo.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Viwanda na Biashara imeshindwa kudhibiti uingiaji wa madeni holela katika Wizara na Taasisi za Serikali na kuua biashara, ajira, kodi na uwekezaji nchini.
Licha ya kuwepo Sera na Sheria ya ushiriki wa wazawa (Local Content) katika uwekezaji na miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini kuna maandalizi hafifu ya watanzania kushiriki utekelezaji wa miradi hiyo na hivyo watanzania kutokujua fursa zilizozipo kwenye miradi hiyo kama LNG, JNHPP- 2115, SGR, Bomba la Mafuta (EACOP), Kabanga Nickel, Liganga na Mchuchuma nk. Hakuna mkakati wazi ulioandaliwa kuwezesha watanzania wote kuyajua mahitaji ya chakula, vifaa na utaalamu ili waweze kujiandaa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi hiyo na hata baadhi ya mikataba haiweki masharti ya ushiriki wa wazawa.
Matokeo yake hata kwa kazi ambazo zingeweza kufanywa na watanzania hufanywa na wageni na mahitaji kuagizwa kutoka nje ya nchi na watanzania kubaki kuwa watazamaji. Hali hii inawakosesha ajira watanzania, Serikali kukosa mapato na kuua uchumi wa nchi.
Makadirio yanapokuwa ya juu wafanyabiashara hushindwa hata kulipa ile theluthi 1 ya kiwango cha kodi kinachobishaniwa na pale mashauri yanapochukua muda mrefu kuamualiwa na mamlaka za rufani za kodi, Serikali inapoteza mapato mengi.
Muda wa wiki 2 haitoi nafasi kwa wafanyabiashara na wadau wengine kusoma na kuelewa msingi wa mabadiliko ya kodi yaliyowasilishwa na Serikali hali inayopelekea kushindwa kutoa Maoni na ushauri na kushuka kwa viwango vya uzingatiaji wa ulipaji kodi (low Compliance rate)
Changamoto nilizozitaja ni za siku nyingi lakini zimefumbiwa macho licha ya kuwepo Sheria madhubuti na Taasisi za Udhibiti. Huu si wakati wa kuikumbusha Wizara hii Wajibu wa Majukumu yao kwani wanajua na walishashauriwa mara nyingi, lakini pia sio wakati wa kubebana katika matatizo makubwa haya kwa gharama za wananchi kama wawakilishi ni lazima tuonyeshe hasira zetu dhidi ya Wizara hii kwa utaratibu wa “Carrot and Stick approaches”. Ili kutoa fundisho na kuleta mageuzi makubwa yatakayokuza biashara na uwekezaji nchini na hivyo kukuza uchumi na mapato ya Serikali kwani “Calibration and Adjustments are the Natural Course of Action for Building Excellence”
Mwisho, kwa kuwa Wizara hii imeshindwa kuwajibika kikamilifu kwa sababu wanazozijua wao nalishawishi Bunge kiushauri Serikali kufanya yafuatayo:
- UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, Ustawi wa Sekta Binafsi unategemea ulinzi imara wa soko la ndani na udhibiti wa uingizaji holela wa bidhaa kutoka nje ya nchi, uingizaji wa bidhaa zisizo na ubora na usawa katika ufanyaji biashara.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake imeleta maombi ya fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 135.79 ambapo matumizi ya kawaida ni Tsh. Bilioni 93.91 na matumizi ya Maendeleo ni Tsh. Bilioni 41.88 ambapo pendekezo langu la awali, Wizara hii isitengewe fedha kwa kuwa imeshindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu yaliyowekwa kwa mujibu wa Sheria.
UTEKELEZAJI WA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA
Mheshimiwa Spika, Pia niungane na Kamati na Wabunge wenzangu kwa hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Linganga na Mchuchuma ikiwa ni pamoja na kukamilika kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi huo na kuanza mazungumzo na Kampuni ya China ambapo tayari Makubaliano yamefanyika kwenye baadhi ya vipengele muhimu vya mikataba kama mgawanyo wa hisa na muundo wa uwekezaji, kiwango cha mtaji wa uwekezaji na muda wa uwekezaji.
Hii ni hatua nzuri ya kupongezwa.
Changamoto ninayoiona hapa majadiliano yamefanyika hadi kuhitimishwa kwa usiri bila kuuarifu umma kupitia Bunge, Sheria za Maliasili za nchi, Sheria ya The Natural Weath and Resources (Permanent Sovereignty) Act No.5 of 2017 na TEITA Act 2015 ambazo zinakataza usiri wa majadiliano katika miradi ya uziduaji na raslimali zingine za asili.
Taarifa iliyowasilishwa na Serikali haina taarifa muhimu kama tathmini ya mradi na Makubaliano mahususi yaliyofikiwa katika uwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma. Mfano Waziri hakuweka wazi thamani ya Makaa ya Mawe na Chuma yaliyopo, thamani ya uwekezaji na Wajibu wa pande zote mbili, kila upande utapata hisa kiasi gani na namna mapato yatakavyogawanywa, muda wa utekelezaji wa mkataba na kipindi cha mkataba nk.
Hivyo Waziri wa Viwanda na Biashara anapaswa kuliambia Bunge kwa uwazi manufaa ya utekelezaji wa mkataba huo badala ya kutoa taarifa inayoficha mambo muhimu ambayo mara nyingi usiri huu umekuwa ukitumika kama kichaka cha kuzaliwa mikataba Mibovu na isiyo na maslahi kwa Taifa. Pamoja na kusubiri kwa hamu utekelezaji wa Mradi wa Liganga na
Mchuchuma lakini pia hatuweza kukubali kuingizwa kwenye mikataba Mibovu.
HALI YA VIWANDA NA UWEKEZAJI NCHINI
Mheshimiwa Spika, Mwenendo wa uwekezaji nchini, Katika kipindi cha mwaka 2022/2023 kupitia dirisha la huduma za uwekezaji mahala pamoja (One Stop Facilitation Centre- OSC) ambapo ilisajiliwa miradi 240 yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,387.17 sawa na Tsh. Trilioni 11.4 kati ya miradi hiyo miradi 94 ya wageni, 89 ya watanzania na 57 ya ubia kati ya wageni na watanzania. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa kampuni za kigeni na raia wa kigeni wanaongoza kwa uwekezaji nchini.Pia katika kipindi cha mwaka 2023/2024 waliopeleka maombi kwenye Tume ya kugawa ardhi kwa ajili ya uwekezaji ni 191 na kati yao maombi hayo 130 sawa 68% ni kampuni ya nje ya nchi na 61 sawa 32% ni makampuni ya Tanzania.
Ushahidi wote unaonyesha kuwa Makampuni na raia wa kigeni wanawekeza zaidi nchini kwa zaidi ya 68% ya uwekezaji unaofanywa kila mwaka. Wizara ya Viwanda na Biashara inapaswa kutoa majibu kwanini tumefikia hapo, nini kinachowafanya watanzania washindwe kuwekeza, kujenga viwanda na kuendesha biashara?
Baadhi ya Wawekezaji wa ndani wanalalamika kunyang’anywa kazi na wageni, hivi karibuni Mfanyabiashara Maarufu nchini na Mbunge Mstaafu wa Igunga, Mheshimiwa Rostam Aziz alinukuliwa na vyombo vya habari akilalamikia wazawa kunyimwa kazi na kazi nyingi kupewa wageni huku akionya kuwa hakuna nchi Duniani iliyowahi kupata maendeleo kwa kutegemea
wawekezaji wa nje pekee. Wizara ya Viwanda na Biashara inapaswa kujibu maswali haya magumu yanayolalamikiwa na wafanyabishara mmoja mmoja na Jumuiya zao za TPSF, TCCIA, CTI, ZNCC, TATOA, TWCC, ACT, TAFOPA, TTMOA ,ATE, TBA, TAMIDA, TSPA, TANEXA, CATA, TASOTA, TASAA, TASSIM, TSA, TWCA, TAA, TUCASA, TEGAMAT, TABOA nk.
CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAFANYABIASHARA NCHINI
Sera za Kodi zisizotabirika na Misamaha holela ya kodi kwa bidhaa za kutoka nje ya nchi
Mheshimiwa Spika, Kuwa na Sera, Sheria, Kanuni, Mikakati na Miongozo ya Kodi isiyotabirika na kusababisha mazingira magumu ya uwekezaji na biashara nchini. Mabadiliko ya kodi ya mara kwa mara yasiyo na utafiti na tathmini ya kutosha yanasababisha kusuasua kwa uwekezaji na kufungwa kwa biashara na kuikosesha serikali mapato.Kutoa Misamaha ya kodi kwa bidhaa za nje huku bidhaa za ndani ya nchi zinatozwa kodi. Mfano sukari ya kutoka nje ya nchi imesamehewa kodi ya VAT na Import Duty wakati sukari zinazolishwa nchini zinatozwa VAT. Pia sukari inayozalishwa nchini kulipa ushuru wa Tsh. 50 kwa kilo wakati sukari ya kutoka nje ya nchi inalipa Tsh. 7.8 tu kwa kilo hapa hakuna usawa na kwa vyovyote wazalishaji wa ndani hawawezi kushindana na sukari kutoka nje ya nchi.
Misamaha ya Kodi ya VAT na Kodi ya Mapato kwa wawekezaji mahiri mara nyingi imekuwa ikihusisha Makampuni ya Nje na hivyo kukosesha usawa wa gharama za uzalishaji, Waziri mwenye
dhamana ya Viwanda na Biashara alipaswa kupambania haki na usawa wa biashara nchini.
Uingizaji holela wa bidhaa kutoka nje ya nchi
Mheshimiwa Spika, Soko la ndani limejaa chakula, mazao, vifaa vya ujenzi, vipuri vya magari, vifaa vya umeme, vifaa vya TEHAMA hata vile ambavyo vinaweza kupatikana nchini.Nchi yetu, inatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza huduma na bidhaa kutoka nje ya nchi, Mfano kiasi cha Tsh Bilioni 474 zinatumika kuagiza mafuta ya kupikia nje ya nchi kila mwaka, Kiasi cha Tsh. Bilioni 696 kutumika kuagiza ngano nje ya nchi, pia tunatumia zaidi ya Trilioni 1.1 kuagiza mbolea nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, Katika Hotuba ya Waziri ameelezea uwekezaji wa Kiwanda cha Mbolea cha Intracom Fertilizer Limited wenye gharama ya Tsh. Bilioni 78.4 kinachozalisha mbolea aina ya FOMI ambapo kikikamilika kitafikisha uzalishaji wa mbolea tani Milioni 1. Pamoja na kiwanda hiki kuanza uzalishaji kwa sehemu kubwa hatununui mbolea katika kiwanda hiki na badala yake tunaendelea kuagiza mbolea nje ya nchi.
Pia ofisi nyingi za umma zimejaa samani za kutoka nje ya nchi mpaka maziwa yanayotumika kwenye ofisi nyingi za umma ni ya kutoka nje ya nchi, ipo mifano mingi ya nchi kugeuzwa soko la bidhaa za nje huku bidhaa za ndani zikikosa soko, kuoza na kuharibika. Katika eneo hili Serikali inatumia fedha nyingi za kigeni bila sababu za msingi na kupoteza mapato ya Serikali.
Hiki kilio ni cha muda mrefu lakini Wizara ya Viwanda na Biashara imeshindwa kutafuta suluhisho la kudumu na kukomesha mambo hayo.
Uingizaji wa bidhaa zisizo na ubora
Kushamiri kwa Biashara Haramu, Biashara za magendo na matumizi ya bandari bubu, kumepelekea bidhaa nyingi kuingizwa nchini bila kulipa kodi. Pia uingizwaji bidhaa feki na bandia na zisizo na ubora umekuwa ukiuwa ushindani na soko la bidha za ndani ya nchi, Vile vile viwanda bubu ambavyo hutengeneza bidhaa kama vinywaji vikali, wine, vifaa vya ujenzi, umeme nk na kuuzwa bila kulipa kodi..Mfano mwaka 2022/2023 Serikali ilisamehe faini ya 15% ya wafanyabishara ambao hawana vyeti vya CoC na kuondoa ulazima na hivyo kuwa hiari kufanya ukaguzi wa PVoC kitendo ambacho kimeleta madhara makubwa ya kufurika bidhaa feki, bandia na zisizo na ubora katika soko la ndani.
Hali ambayo imeleta madhara makubwa ya kiafya na Kiuchumi. Bidhaa zisizo na ubora kutoka nje ya nchi zimeua ushindani wa haki katika soko la ndani, kufungwa viwanda, ajira kupotea na madhara mengine ya kiafya kwa wananchi. Maamuzi haya yalifanywa bila kuzingatia uwezo wa kitaalamu na kimaabara ya TBS.
Leo tunavyozungumza baadhi ya vifaa vya ujenzi, vipuri na vilainishi vya magari, pikipiki, sukari, mchele, ngano, mbolea, mbegu, viuatilifu, mafuta, vipodozi, vifaa vya umeme, simu, luninga nk vitu hivyo vimeingia nchini vikiwa havina ubora na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi kuhatarisha maisha yao na kuua uchumi na kupoteza mapato ya Serikali.
Taifa na wananchi wanapata hasara kubwa mfano nondo feki ambapo tutakwenda kujenga madaraja na majengo yasiyo na ubora ambayo yataishia kubomoka na kuanguka na kuleta madhara makubwa, vifaa vya umeme ambavyo vimekuwa vikilipuka kila leo na kuunguza mali na kuhatarisha maisha, vipuri vya magari feki vinavyosababisha ajali kila uchao na kusababisha kupoteza maisha kwa wananchi wasio na hatia.
Mheshimiwa Spika, licha ya ukubwa wa tatizo hili sioni dhamira ya dhati ya Wizara ya Viwanda na Biashara kudhibiti uingizaji wa bidhaa zisizo na ubora nchini.
Hivi sasa hali ni mbaya nchi yetu imegeuzwa kuwa dampo la bidhaa feki na bandia na zilizokwisha muda wa matumizi. Na hapa natapa mkanganyiko mkubwa wa fikra kwamba kama Sheria zipo, Mamlaka za udhibiti za TBS, TMDA, FCC, BRELA zipo nini kinachokwamisha?
Kama Sheria zipo na Mamlaka za udhibiti zipo na hali inazidi kuwa mbaya, kuna mambo 2, Moja, kuna Udhaifu mkubwa wa kiutendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi zake, lakini Pili inaweza kuwa biashara hizo ni za kwao na hivyo si rahisi kudhibiti na kujichukulia hatua wao wenyewe.
Raia wa kigeni kuruhusiwa kufanya biashara ndogondogo kinyume cha Sheria za nchi
Kuruhusu raia kutoka nje ya nchi kufanya biashara ndogondogo kinyume cha Sheria kama umachinga, kuchoma mahindi, uchimbaji mdogo wa madini, uvuvi na kushamiri kwa uanzishwaji wa viwanda bubu.Hivi majuzi Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliagiza kuundwa Tume ya kuchunguza raia wa kigeni wanaofanya biashara Kariakoo ambapo uchunguzi ulibaini kuwepo kwa raia wengi wa kigeni wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo katika Soko hilo, Jambo la kusikitisha na kushangaza Waziri wa Viwanda na Biashara alikwenda kushughulika na suala hilo moja tu la Kariakoo na kuacha maeneo mengine ya masoko na shughuli nyingine za Kiuchumi kama Uchimbaji mdogo wa madini, uvuvi, viwanda ambako nako kuna raia wengi wa kigeni.
Maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini kupewa raia wa kigeni
Maeneo mengi ya wachimbaji wadogo yamekuwa yakiuzwa kwa raia wa kigeni na hivyo wazawa kufukuzwa na kukosa maeneo ya kuchimba na kuikosesha mapato Serikali.Mfano eneo la wachimbaji wadogo la Bushimangila Msalala, Mwakitolyo Namba 5 Shinyanga, Mavota Ushirombo, Ntambarare Namba 2 Segese, Shilalo Misungwi, Nyamahuna Geita, Iramba Singida, Bugaka Msalala nk maeneo yameuzwa kwa wawekezaji wa Kichina na kusababisha adha kubwa kwa wachimbaji wa wadogo kwa kukosa maeneo ya kuchimba waliyokuwa wanajitafutia riziki huku wakiwa hawana njia Mbadala, na wengine kufukuzwa bila hata kulipwa fidia ya uwekezaji waliofanya na hivyo kupata hasara na kufilisika na kuikosesha mapato Serikali.
Pia kuwepo na migogoro na Malalamiko yasiyoisha katika maeneo ya wachimbaji wadogo ambapo shughuli za uchimbaji zimekuwa
zikisimamishwa mara kwa mara kwa visingizio mbalimbali mfano eneo la Ifugandi Nyang’hwale Geita wachimbaji hao wamepaza sauti bila kusikilizwa.
Maeneo ya wachimbaji wadogo yaliyokuwa yakiajiri watu 10,000 hadi 20,000 na kuzalisha takribani kilo 20 za madini kila mwezi na kuchangia mapato ya Serikali anakabidhiwa mchina mmoja (Raia wa Kigeni) ambaye hamna masharti ya uzalishaji kwa mwezi ni yeye anavyoona inafaa na wakati mwingine hata akaunti zake hazipo hapa nchini na hivyo kupoteza ajira nyingi, kudumaza uchumi na kupoteza mapato ya Serikali.
Kazi kupewa Makampuni ya Kigeni
Mheshimiwa Spika, Zabuni na kandarasi nyingi kupewa wageni, umeme, barabara, madaraja, Majengo ya Serikali, Maji nk.Wazabuni na wakandarasi kupewa wa kutoka nje ambao wengine hawana sifa, upendeleo, kuvunja Sheria na kuacha njia ya ununuzi ya ushindani ili kufanikisha kupendelea Makampuni ya kigeni.
Zabuni, kandarasi na ushauri elekezi kwenye miradi mingi kwa sehemu kubwa wapewa wageni hata kwa zile ambazo zinaweza kufanywa na wazawa katika sekta mbalimbali na miundombinu ya Kiuchumi.
Mfano sekta ya ujenzi ina makandarasi 14,550 ambapo kati yao 550 ni makandarasi wa nje na 14,000 ni makandarasi wazawa lakini katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wazawa wanapata 46% na makandarasi wa nje wanapata 54% ya thamani ya miradi
hii ina maana kuwa 54% ya bajeti ya Ujenzi inalipa wageni na kwamba miradi yote mikubwa wanapewa wageni na miradi midogo midogo wanapewa wazawa ambao pia wanakopwa miaka nenda rudi hadi kufilisika.
Katika uchambuzi uliofanywa na The CHANZO Initiative Machi 31, 2024 unaonyesha kuwa TANROADS imekuwa ikilipa 95% ya bajeti ya ujenzi kwa Makampuni ya nje katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2024 ambapo imelipa kwa Makampuni ya nje Tsh. Trilioni 11.72 sawa na 95% ya fedha zilizolipwa wakati Makampuni za ndani zikiambulia Tsh. Bilioni 633 tu sawa na 5% tu ya fedha zilizolipwa. Huku Makampuni ya Kichina yakipata fedha nyingi zaidi yakiongozwa na Kampuni ya CCECC iliyopata Tsh. Trilioni 4.9 na Kampuni ya CHICO iliyopata Tsh. Bilioni 920.
Kampuni za Kichina za CCECC, CHICO, CRJE na Synohidro karibu kila mradi wanapewa wao hapa nchini katika miradi ya Barabara, Bandari,Nishati, Maji, Reli, viwanja vya ndege, Madaraja Nk hii inatia uchungu sana kwa wakandarasi wazawa na vijana wa kitanzania wanaotaabika kwa kukosa ajira.
Malimbikizo na Madeni ya Wazabuni na Wakandarasi
Serikali kudaiwa malimbikizo ya madeni ya wazabuni na wakandarasi kupitia Wizara, LGAs, Mashirika na Taasisi za Serikali ambayo yamefikia kiasi cha Tsh. Trilioni 3.5. Madeni haya ni ya muda mrefu na baadhi ya Makampuni yamefilisika na kufunga biashara, kuua ajira na mapato ya Serikali kupotea ambapo Makampuni hayo yalikuwa yakilipa kodi kila mwaka.Changamoto hii kwa sehemu kubwa ni kwa Makampuni ya Ndani kwani Makampuni ya nje yamekuwa yakilipwa pamoja na riba kufidia ucheleweshaji wa malipo.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Viwanda na Biashara imeshindwa kudhibiti uingiaji wa madeni holela katika Wizara na Taasisi za Serikali na kuua biashara, ajira, kodi na uwekezaji nchini.
(Viii) Ushiriki mdogo wa Watanzania katika miradi mikubwa ya kimkakati
Mheshimiwa Spika, Ushiriki mdogo wa watanzania na Makampuni ya ndani katika miradi ya kimkakati, hakuna taarifa wala kanzidata ya watoa huduma iliyoandaliwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati na uwekezaji kwa sekta binafsi nchini. Pia mifumo ya kanzidata za BRELA, TIC, TRA na NIDA haijahuishwa kuwezesha upatikaji wa taarifa muhimu.Licha ya kuwepo Sera na Sheria ya ushiriki wa wazawa (Local Content) katika uwekezaji na miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini kuna maandalizi hafifu ya watanzania kushiriki utekelezaji wa miradi hiyo na hivyo watanzania kutokujua fursa zilizozipo kwenye miradi hiyo kama LNG, JNHPP- 2115, SGR, Bomba la Mafuta (EACOP), Kabanga Nickel, Liganga na Mchuchuma nk. Hakuna mkakati wazi ulioandaliwa kuwezesha watanzania wote kuyajua mahitaji ya chakula, vifaa na utaalamu ili waweze kujiandaa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi hiyo na hata baadhi ya mikataba haiweki masharti ya ushiriki wa wazawa.
Matokeo yake hata kwa kazi ambazo zingeweza kufanywa na watanzania hufanywa na wageni na mahitaji kuagizwa kutoka nje ya nchi na watanzania kubaki kuwa watazamaji. Hali hii inawakosesha ajira watanzania, Serikali kukosa mapato na kuua uchumi wa nchi.
Malalamiko ya ukadiriaji wa kodi
Mheshimiwa Spika, Kuwepo na Malalamiko makubwa ya ukadiriaji wa kodi (Tax Assesment and Disputes), kumekuwepo na Malalamiko makubwa ya wafanyabiashara kwa TRA kutoa makadirio makubwa kuliko ukubwa wa biashara na kuwafanya washindwe kulipa kodi kwa wakati lakini pia kuwalazimu kwenda katika Mamlaka za Rufaa za Kodi za TRAB, TRAT na CAT ambapo pia mashauri hukaa muda mrefu bila kuamuliwa.Makadirio yanapokuwa ya juu wafanyabiashara hushindwa hata kulipa ile theluthi 1 ya kiwango cha kodi kinachobishaniwa na pale mashauri yanapochukua muda mrefu kuamualiwa na mamlaka za rufani za kodi, Serikali inapoteza mapato mengi.
Ushiriki wa Sekta Binafsi katika Muswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill)
Ushirikishwaji mdogo wa Sekta Binafsi wakati wa maandalizi ya Bajeti na Sheria za Bajeti ambapo hutolewa siku 15 tu au wiki 2 tu wadau na Bunge kujadili na kuamua Muswada wa Sheria ya Fedha (Finance Bill), muda huu ni mfupi sana na hata wenzetu wa nchi jirani wa Kenya na Uganda Muswada wa Sheria ya Fedha huwasilishwa na kujadiliwa kwa miezi 2.Muda wa wiki 2 haitoi nafasi kwa wafanyabiashara na wadau wengine kusoma na kuelewa msingi wa mabadiliko ya kodi yaliyowasilishwa na Serikali hali inayopelekea kushindwa kutoa Maoni na ushauri na kushuka kwa viwango vya uzingatiaji wa ulipaji kodi (low Compliance rate)
5 HITIMISHO
Mheshimiwa Spika, Kama nilivyosema hapo awali kwamba nimepata mgongano mkubwa sana wa kifikra kwa Wizara inayotegemewa kuwa Rufaa ya huzuni na mateso ya Wafanyabiashara kuwa kinyume chake, kuwa Wizara ya kuua biashara, wawekezaji, ajira na kodi nchini, kuwa Wizara ya kufanikisha biashara za raia wa kigeni na kuua biashara za wazawa.Changamoto nilizozitaja ni za siku nyingi lakini zimefumbiwa macho licha ya kuwepo Sheria madhubuti na Taasisi za Udhibiti. Huu si wakati wa kuikumbusha Wizara hii Wajibu wa Majukumu yao kwani wanajua na walishashauriwa mara nyingi, lakini pia sio wakati wa kubebana katika matatizo makubwa haya kwa gharama za wananchi kama wawakilishi ni lazima tuonyeshe hasira zetu dhidi ya Wizara hii kwa utaratibu wa “Carrot and Stick approaches”. Ili kutoa fundisho na kuleta mageuzi makubwa yatakayokuza biashara na uwekezaji nchini na hivyo kukuza uchumi na mapato ya Serikali kwani “Calibration and Adjustments are the Natural Course of Action for Building Excellence”
Mwisho, kwa kuwa Wizara hii imeshindwa kuwajibika kikamilifu kwa sababu wanazozijua wao nalishawishi Bunge kiushauri Serikali kufanya yafuatayo:
- Kuwaondoa Watumishi wote wa Wizara ya Viwanda na Biashara kuanzia Waziri hadi mfagizi wa Ofisi na kuweka watumishi watakaowajibika kikamilifu kwa mujibu wa viapo na Sheria za Nchi.
- Kuifuta Wizara ya Viwanda na Biashara