GE2025 Luhaga Mpina: CCM ina wenyewe na hao wenyewe ndio mliowaona juzi kwenye harambee yao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Luhaga Mpina Mgombea urais kupitia chama Cha ACT-Wazalendo akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini leo tarehe 14 Agost, 2025 katika Jengo la Maalim Seif, Dar es Salaam.

​

"Nimezaliwa katika familia ya CCM akiwemo baba yangu ambaye ni mwanzilishi wa Chama Cha TANU,lakini licha ya kuzaliwa katika chama hicho chama Cha mapinduzi kimepoteza mwelekeo na kukiuka misingi iliyowekwa na waasisi wake.

CCM imesaliti adhima na misingi iliyowekwa na waasisi wa Chama hicho, CCM imekuwa na misingi ya kujisahihisha. CCM ilijisahihisha mwaka 2015 baada ya Mwalimu Nyerere. Hii ya sasa imechoka, haina wazee wa kuisahihisha. Hii ya sasa ni kama vyuma chakavu.

Upendeleo umehalalishwa, vitabu viko sawasawa ila genge linaloiendesha sasa hamna kitu. Pia vitendo vya wizi wafedha za wavuja jasho. Watu wamekula hela kutokana na urefu wa kamba zao. Watu wamekuwa wakihangaika kulipia hospitali kutokana na CCM kushindwa kuwajibika na kuruhusu watu wacheche kula kutokana na urefu wa kamba yake.

Pia upotevu wa mali za umma na hakuna aliyewajibishwa. Mchakato wa uchujaji wa mwaka huu 2025 umevunja katiba ukiwa na upendeleo. Tumeshuhudia kikao Cha kuwaengua watia nia wakikikesha usiku kucha kuwaondoa wakina Mpina,lakini kukaa hata kikao kimoja kujadili ripoti ya CAG juu ya upotevu na wizi wa fedha hakuwahi kujadiliwa hata siku moja?"
 
Mbona nyie Chadomo huwanawaita ni CCM B?
Mimi ni mwanachama wa ccm, mwenye kadi! Shida iliyopo kwangu ni kutokupenda kuunga mkono wizi, ufisadi, upigaji dili, ubadhirifu, ujinga, upumbavu, uchawa, ujangili, uonevu, dhuluma, nk. Hata sishangai mara nyingi mnapo nihusisha na CHADEMA.
 
Toka umezaliwa umewahi sikia SSH akitajwa kwenye ufisadi?
 
Kuna maneno maarafu sana yanasema hivi "nioneshe marafiki zako, ili nikuambie tabia yako"
Sasa uniambie hapa marafiki wa SSH ni akina nani, ili nikutajie tabia yake.
 
Maneno vs uhalisia
Dhamira ya mtu inaanzia kwenye maneno yake kabla ya kuhamia kwenye moyo wake. Kama wewe ni kiongozi halafu unashindwa kudhibiti, kukemea na kukomesha vitendo vya rushwa vilivyokithiri! Tukuweke kwenye kundi gani? Ni dhaifu, au ni sehemu ya hao rushwa?

Kama kiongozi unatangaza hadharani watoa taarifa za uhujumu uchumi, wizi, ubadhirifu, nk. washughulikiwe/wadhibitiwe! Tukuweke kwenye kundi gani?

Kama kiongozi unaruhusu kufungamana na watu walioshtakiwa na mtangulizi wako kwa makosa ya ufisadi! Tukuweke kwenye kindi gani?

Kama kiongozi unashindwa kushughulikia kwa vitendo wabadhirifu waliotajwa kwenye ripoti ya mdhibiti wa hesabu za serikali! Na badala yake hao watu unawapandisha cheo! Tukuweke kwenye kundi gani?
 
Luhaga Mpina Mgombea urais kupitia chama Cha ACT-Wazalendo akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini leo tarehe 14 Agost, 2025 katika Jengo la Maalim Seif, Dar es Salaam.

"Nimezaliwa katika familia ya CCM akiwemo baba yangu ambaye ni mwanzilishi wa Chama Cha TANU,lakini licha ya kuzaliwa katika chama hicho chama Cha mapinduzi kimepoteza mwelekeo na kukiuka misingi iliyowekwa na waasisi wake.

CCM imesaliti adhima na misingi iliyowekwa na waasisi wa Chama hicho, CCM imekuwa na misingi ya kujisahihisha. CCM ilijisahihisha mwaka 2015 baada ya Mwalimu Nyerere. Hii ya sasa imechoka, haina wazee wa kuisahihisha. Hii ya sasa ni kama vyuma chakavu.

Upendeleo umehalalishwa, vitabu viko sawasawa ila genge linaloiendesha sasa hamna kitu. Pia vitendo vya wizi wafedha za wavuja jasho. Watu wamekula hela kutokana na urefu wa kamba zao. Watu wamekuwa wakihangaika kulipia hospitali kutokana na CCM kushindwa kuwajibika na kuruhusu watu wacheche kula kutokana na urefu wa kamba yake.

Pia upotevu wa mali za umma na hakuna aliyewajibishwa. Mchakato wa uchujaji wa mwaka huu 2025 umevunja katiba ukiwa na upendeleo. Tumeshuhudia kikao Cha kuwaengua watia nia wakikikesha usiku kucha kuwaondoa wakina Mpina,lakini kukaa hata kikao kimoja kujadili ripoti ya CAG juu ya upotevu na wizi wa fedha hakuwahi kujadiliwa hata siku moja?"
Kama ni kweli Mpina kampigia Pambalu wa Chadema kumshawishi ahamie ACT na kumuahidi kitita Cha milioni 100 zimsaidie kugombea ubunge Mwanza,basi nchi hii Wazalendo ni wachache.
 
Back
Top Bottom