#COVID19 Luhaga Mpina: Corona isiwe kwa wazembe kukusanya mapato ya Serikali

#COVID19 Luhaga Mpina: Corona isiwe kwa wazembe kukusanya mapato ya Serikali

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge Luhaga Mpina ametahadharisha mlipuko wa COVID19 usiwe kinga kwa watu waliozembea kukusanya mapato ya Serikali kwa kisingizio cha Ugonjwa huo.

Katika mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha, Mbunge huyo amehoji namna Wizara hiyo inafuatilia ili kujiridhisha pale inapoambiwa sababu ni Virusi vya Corona.

 
Akiwa Bungeni Dodoma, Luhaga Mpina amempongeza Rais Samia Suluhu kwa jinsi anavyoendelea ambapo amesema hadi sasa hamna mradi unaosuasua na miradi yote ya kimkakati inaendelea vyema.

Pia Mpina ameongelea zimepokelewa changamoto nyingi kwa wizara na taasisi nyingi kushindwa kufikia malengo wakieleza sababu ni Corona, Mpina amesema pengine ni kweli lakini haiwezi kulingana na maeneo mengine ambayo waliweka 'lockdown' na kwa hilo anampongeza kwa dhati Hayati John Magufuli kwa kusimamia vizuri hilo eneo.

Mpina ametahadharisha Corona isiwe kinga uzembe wa kukusanya mapato ya serikali.
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya.

Tunaanza kampeni rasmi ya kumchangia na kumuwekea wakili Sabaya kwenye kesi yake. Kama msaliti wa nchi mzee wa MIGA aliweza kuchangiwa ,sisi kama watanzania wazalendo hatuwezi kushindwa kumchangia Sabaya ambaye kwa uzalendo wake aliitoa wilaya ya Hai kutoka ya 63 kwenye ulipaji kodi hadi ikawa ya 4 kitaifa.

Hatuwezi kuhukumu watu kwa kusikiliza upande mmoja wa wanafiki chadema ambao hawana jema kwa nchi yetu.

Chadema kila kitu wanapinga na kuponda, walipinga ndege, bwawa la umeme, elimu bure, ujenzi wa viwanda kila kitu wao ni kupinga tu, Ndege zilipokamatwa walishangilia.
Ndiyo tuwasikilize? Hapana.

#Justice for SABAYA
#Free SABAYA
 
Hatuko tayari kuona wazalendo wa nchi yetu wakinyanyaswa na wauza madawa ya kulevya...
Hilo suala sio la siasa ni la haki za binaadamu, muache Sabaye asimame mbele ya haki ajitetee, muache ushabiki usio kua na tija Tz nikubwa kuliko mtu yoyote.
 
Back
Top Bottom