Luhaga Mpina Hana Vigezo vya Kugombea Urais Hii Ndiyo Sababu kiundani na ningeshanga sana kukubaliwa

Luhaga Mpina Hana Vigezo vya Kugombea Urais Hii Ndiyo Sababu kiundani na ningeshanga sana kukubaliwa

Lastborn Wa Taifa

New Member
Joined
Aug 22, 2025
Posts
3
Reaction score
0
Thread: Luhaga Mpina Hana Vigezo vya Kugombea Urais Hii Ndiyo Sababu kiundani na ningeshanga sana kukubaliwa

1.Muda wa Uanachama Ulikosekana
Kanuni za ACT WAZALENDO zinahitaji mwanachama awe na siku 30 kabla ya uteuzi. Mpina alijiunga tarehe 5 Agosti, akateuliwa siku moja baadaye tarehe 6 Agosti. Alikosa hata siku 7

2.Fomu Zilichukuliwa Baada ya Mwisho Wake
Mwisho wa kuchukua fomu za urais ulikuwa tarehe 25 Mei. Mpina alijiunga na kuchukua fomu mwezi Agosti mwezi 3 uliopita! Hakuna marekebisho yaliyopitishwa kikatiba.

3.Hajatangaza Mali yake
Kanuni inamlazimisha mgombea kutangaza mali na vyama vyake kabla ya kuteuliwa. Mpina hakufanya hivyo

5.Hatukuiona Itikadi yake
Hakuthibitisha uelewa wa falsafa,misingi, na sera za ACT WAZALENDO hata kidogo.

6.Sheria Ya Vyama Vya Siasa Inakataza Hii
Kifungu cha 6A(2) cha Sheria ya Vyama Vya Siasa kinasema,chama kiendeshwe kwa kanuni zake.Hii haikufanyika.

Mpina hana vigezo, na uteuzi wake ni ukiukwaji wa wazi wa kanuni na sheria.ACT WAZALENDO imejikwaa mwenyewe.
 
Attachments

  • IMG-20250826-WA0400.jpg
    IMG-20250826-WA0400.jpg
    46.9 KB · Views: 26
Kwa hiyo Mpina anaweza kuwa mgombea urais September 5?
Mwenye wivu ajinyonge.
Mpina anaweza kuwa mgombea urais wiki ijayo.
 
Huyo ni project ya chams chawala hivyo hakuna jipya
 
Back
Top Bottom