Wakuu,
Inaonekana mambo yameendelea kuchemka huko CCM.
Imefikia hatua hata viongozi wa CCM wameanza kukosoa jinsi mchakato wa Uchaguzi Wa Serikali unavyoenda.
Soma pia:
Luhaga Mpina kufungua Kesi zote ndani ya masaa 24
Nimejiuliza tu, hivi kwa post hii, Luhaga Mpina atakuwa salama kweli au ndo watamfukuza uanachama na automatically kumvua Ubunge.
Simulizi za zamani zina visa vyenye muktadha na mafundisho mazuri pamoja na kusheheni mantiki na maudhui mazuri sana ndani yake.
Mathalani ni kile kisa kimoja maarufu cha mfalme mpenda sifa pamoja na wapambe wake uchwara, alijikuta akingizwa mkenge na wapambe zake, akajikuta akikaa uchi wa mnyama mbele za watu huku akiwa ameaminishwa kuwa kavaa mavazi ya kifahari na pia yenye thamani kubwa.
Ijapokuwa yeye binafsi hakuweza kuyaona, bali aliiamini hivyo kutokana ujinga wake mwenyewe.
Hali akijijua yeye yupo uchi, na wala hakuweza kuyaona, bali alizuga tu na kujifanya anayaona kwa kuwa aliaminishwa hivyo.
Ijapokuwa wapambe wake pia walijitambua kwa uovu wao, na pia wala hawakuyaona, mavazi hayo bali walilazimika kumsifia tu huku wakimsanifu kwa kuona utupu wake.
Hali kadhalika ilikuwa pia kwa wananchi wote, walipigwa na butwaa pale walipouona utupu wake akiuanika hadharani, lakini kwa unafiki wao walilazimika kusifia uzuri wa mavazi/mavuzi yake
Dogo asiye kuwa na hili wala lile ndiye pekee ambaye aliweza kuuanika upuuzi huo hadharani. Dogo huyo bila ya hiyani alilazimika kuropoka kwa sauti ya juu na kumuuluza mama yake, "mbona mfalme yupo uchi"
CCM na viongozi wake (mama) wapo uchi, na kuuweka hadharani na kila mtu anatambua ukweli huo. Hata vyombo vya ulinzi na usalama navyo vipo hivyo hivyo, ijapokuwa huuona kwa wazi utupu huo wa mfalme vimeamua kuuchuna, na kusifia ili kutimiza tu wajibu, husifia ufahari wa mavazi yake ambayo kiuhalisia haupo. Mtoto (Mpina) kauona utupu huo wa mfalme naye sasa anaropoka hadharani.
Mficha maradhi kilio humuumbua.