Luhaga Mpina: Katiba inataka mikataba yote ya rasilimali iwekwe wazi lakini hawafanyi hivyo

Luhaga Mpina: Katiba inataka mikataba yote ya rasilimali iwekwe wazi lakini hawafanyi hivyo

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
268

Na kwa ujumla serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka mitano, katika miaka mitano, imeingia mikataba ya rasilimali 43 ya rasilimali, na mikataba ya ubia 74 yote kwa siri. Hakuna mkataba ulioletwa kwa wananchi.

Na mikataba hiyo mingi ni mikataba ya rasilimali, uhakika na usalama wa nchi yetu uko wapi? Ukiambiwa mikataba ya rasilimali 43 alafu huijui, sheria ya rasilimali yetu inasema mikataba yote ya rasilimali lazima itangazwe hadharani Watanzania wote wajue. Hawa viongozi wetu wameenda kuingia hiyo mikataba kwa ridhaa ya nani na kwa sababu gani? Na kwa nini hawataki iwe wazi?

Na kukataa uwazi maana yake ni kwamba wewe umetuiibia. Kukataa uwazi kwa sababu unajua tukiuwajuwa ukweli tutakuwajibisha. Sasa kama mikataba 43 imeingiwa, maana yake mnaweza kujikuta rasilimali za nchi zote zimeshauzwa.

Soma katiba, ibara ya tisa, ibara ya 27 (1) na (2), dhamana ya Watanzania katika kulinda rasilimali zao. Na hairuhusiwi mtu mmoja kufanya maamuzi ya rasilimali za Watanzania peke yake. Kitendo cha serikali kutokuweka wazi mikataba hiyo, wameamua kufanya maamuzi kwa niaba ya Watanzania peke yao, hao watendaji wa serikali, kwa maana ya kutuibia tu.

Sasa hiyo mikataba ya hivyo inaingiwa kwa usiri, haiwekwi wazi, hata mkisemaje, katiba ya nchi inakataa, sheria za nchi zinakataa lakini bado hiyo mikataba imeingiwa.

Sheria ya rasilimali inatutaka kwamba mikataba yote ya rasilimali lazima iingie kwa umma. Yaani kwanza kutangaza tenda yake au zabuni yake lazima muwe wazi. Mnapoingia mkataba, vipengele vya mkataba lazima mviweke wazi.

Sasa leo serikali watoke hadharani waseme sababu iliyowafanya kuingia mikataba ya uendeshaji wa bandari kwa siri ni nini? Bandari ni mali ya Watanzania, hiyo siri maana yake ni nini kwenye taifa ambalo linasimamiwa na nguzo kuu ya utawala bora ya uwazi na uwajibikaji? Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba bandari hii ya Dar es Salaam imekabidhiwa, imemilikiwa... ni mkakati ule wa kuhamisha mali ya umma kuzipeleka kwenye umiliki wa watu binafsi kwa manufaa binafsi, ndio maana yake.

Kwa sababu kama sheria inakutaka uweke wazi, mkataba unakutaka uweke wazi, katiba ya nchi inakutaka uweke wazi, wewe unaenda kuweka mikataba ya siri. Na tuméhoji na kuhoji, Watanzania wote wamehoji na kuhoji, HGAs mpaka leo mkataba huo umefichwa na serikali. Na hata ule wa IGA haukuwekwa wazi na serikali mpaka ulipovuja.

Sasa leo serikali watoke hadharani watueleze Watanzania, huo mkataba wa IGA, huo mkataba wa HGAs, hiyo mikataba yote mitatu inatunzwa kwa siri na imeingiwa kwa siri.
 
Back
Top Bottom