The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Huu ni mchango wa mbunge wa jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 tarehe 30 Mei 2024 bungeni Dodoma.
“....Serikali tarehe 16 Juni 2023 kupitia Wizara ya Ujenzi ikiongozwa na Prof. Makame Mbarawa by then, ilisaini mikataba saba ya ujenzi wa miradi saba ya barabara zenye urefu wa jumla ya kilomita 2,035 kwa gharama ya Tsh. Tril. 3.75 kwa kiwango cha lami kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F) na kama pia ilivyoelezwa katika Hotuba ya Waziri (Wizara ya Ujenzi).
Miradi ya ujenzi wa barabara hizo nchi nzima ni hii ifuatavyo hapa👇👇 chini;
1. Mafinga-Mtwango-Mgolololo (Km 81)
2. Igawa-Songwe-Tunduma (Km 218)
3. Uyole-Songwe (Km 48.9), Masasi-Nachingwea-Liwale (Km 175)
4. Arusha-Kibaya-Kongwa JCT (Km 453.42),
5. Ifakara-Lupiro-Malinyi-Kilosa, Kwampepo-Londo Lumecha/ Songea (Km 435)
6. Karatu- Mbulu- Haydom- Sibiti River- Lalago - Maswa - Bariadi Simiyu (Km 339) na;
7. Handeni- Kibirashi- Kijungu- Kibaya- Njoro- OlborotiMrijochini- Chambalo- Chemba- Kwa Mtoro- Singida (Km 374.24).
Tangu kusainiwa kwa mikataba hii leo ni takribani mwaka mzima umepita ujenzi haujaanza. Na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Waziri wa Ujenzi wa sasa, Innocent Bashungwa walikuwa wakieleza kuwa wakandarasi bado wanafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na baadaye maelezo yakabadilika kuwa serikali inatafuta fedha za kuwalipa wakandarasi ikiwemo malipo ya awali ya 10% ya thamani ya mradi kiasi cha Tsh. Bilioni 375.51 ndiyo kazi iweze kuanza.
Awali siku ya kusaini mkataba huu ambapo baadhi ya waheshimiwa wabunge tulishiriki tukio hilo nilipinga wasilisho la Waziri la kuitambulisha miradi hiyo kwa kuwa hapakuwa na maelezo ya kina kuonesha miradi hiyo inatekelezwa kwa utaratibu upi kwani masharti na vigezo vya mikataba hiyo havikuwekwa wazi ilikuwa ni siri kati ya Waziri na Wakandarasi”
“Nilihoji siku ya kusaini Mikataba na ndani ya Bunge nini faida ya kutumia EPC+F badala ya utaratibu wa kawaida wa Serikali kuajiri na kulipa wakandarasi yenyewe.
Nilihoji pia wakandarasi wa EPC+F watalipwa kwa utaratibu gani baada ya miradi kukamilika au kwa kipindi gani.
Na kwa kuwa huu ni mkopo kwanini tunapanua dirisha ukopaji fedha nje ya utaratibu uliowekwa.
Ulinzi wa ajira za vijana nchini utalindwaje katika miradi ya aina hii.
Na kwa kuwa miradi hii wakandarasi watatumia fedha zao (kwa kukopa ktk taasisi za fedha za kimataifa kwa dhamana ya serikali) na baadaye serikali kulipa mikopo, nikataka kujua nafasi ya CAG na Bunge kusimamia matumizi ya fedha hiyo miradi hiyo inapokuwa inakelezwa.
Maswali haya yote hayakupata majawabu hadi leo.
Hapa ni wazi kuwa, serikali imetumia gharama kubwa kuandaa miradi hewa na kupeleka ahadi hewa kwa wananchi wa maeneo yaliyotajwa na mbaya zaidi wananchi wa mikoa inayopitiwa na miradi hii 7 ya Ujenzi ya barabara hizi wameondolewa kwenye mipango na bajeti ya mwaka 2023/2024 na 2024/2025 kwa kuwa barabara zao zitajengwa kupitia utaratibu wa EPC+F.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inakiri kwamba hakuna kinachoendelea katika miradi ya EPC+F, Hotuba ya Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa katika Ibara ya 40 ukurasa wa 36 anakiri kuwa miradi hiyo haina chanzo cha fedha na bado haijaanza na kwamba Serikali inaendelea na mazungumzo na wafadhili ili kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo.
Miradi tuliyoambiwa ina ufadhili wa moja kwa moja yaani mkandarasi anayejenga atatumia fedha zake na baadaye kuidai Serikali, leo tunaambiwa anatafutwa mfadhili wa kugharamia miradi hiyo. Hii inaleta mashaka, wasiwasi, sintofahamu na mkanganyiko mkubwa kiasi cha kutilia shaka credibility......”
Luhaga Mpina.