figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu,
Hapa chini ni maelezo kwa Ufupi ya Mbunge Luhaga Mpina aliyo yatoa kwenye mahojiano na Waandishi wa habari wiki hii Jijini Dar Es Salaam alipokuwa akitoka Mahakamani.
Pia alitoa maagizo kwa mawakili wake waiombe Mahakama Kuu ya Tanzania itoe maelekezo kwa Waziri wa Kilimo Mh. Hussen Bashe, Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Prof. Kennedy Bengesi kusimamishwa kazi. Yaani Mawakili wake 100 waandae barua ya kisheria kuiomba Mahakama itoe amri ya viongozi hawa kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi na mwenendo wa kesi uendelee kwa haki.
Tiririka....
=======
Tarehe 24 Juni, 2024, zililetwa kesi tatu Mahakamani, kama ambavyo mawakili wameeleza. Kesi ya kwanza ililetwa na wakulima wa Kirombero, wakipinga marekebisho ya sheria yaliyofanywa kupitia Finance Bill ya mwaka 2024, hususani katika sekta ya tasnia ya sukari. Wakulima hao wamelalamika Mahakamani, na kesi inaendelea vizuri.
Kesi ya pili ilikuwa yangu mimi, nikimpinga Spika kwa kuniondoa Bungeni, nikiamini kwamba nilionewa na sikutendewa haki.
Kesi ya tatu ilikuwa yangu mimi, Mpina, dhidi ya Waziri wa Kilimo Mh. Hussen Bashe, Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, Bodi ya Sukari, Kamishna wa TRA, makampuni binafsi matatu, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kesi hii ilikuwa inapingwa kuhusu utaratibu wa uingizaji wa sukari nchini, ambao ulisababisha changamoto nyingi.
Kwa ujumla, napenda kusema kwamba Mahakama Kuu mpaka sasa imesikiliza kesi zetu kwa hatua tofauti tofauti. Natoa shukrani kwa majaji wetu wa Mahakama Kuu kwa kutusikiliza vizuri sana, hata kesi nyingine zimechukua muda mrefu, hadi saa tatu usiku. Huu ni mfano mkubwa wa uwajibikaji wa majaji wetu katika kuhakikisha haki inatendeka.
Pia, natoa agizo kwa mawakili wangu waiombe Mahakama Kuu ya Tanzania itoe maelekezo kwa Waziri wa Kilimo Mh. Hussen Bashe, Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Prof. Kennedy Bengesi, kuandaa barua ya kisheria kuiomba Mahakama itoe amri ya viongozi hawa kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi na mwenendo wa kesi uendelee kwa haki.
Nina sababu za kuamini kuwa wao kubaki madarakani kunaweza kuathiri mwenendo wa kesi. Kwa mfano, Waziri wa Kilimo na Bodi ya Sukari bado wanaendelea kutoa vibali vya kuingiza sukari nchini, jambo ambalo naona ni mwendelezo wa kuwakomoa wakulima au viwanda vya ndani. Hivi karibuni, Kiwanda cha Kilombero Sugar kimeshusha bei ya miwa kwa tani kutoka shilingi 108,000 hadi 93,000, likieleza kuwa sukari inayozalishwa nchini haina mahala pa kuuzwa kwa sababu sukari kutoka nje imejaa sokoni.
Vilevile, Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba bado anashikilia nafasi yake licha ya malalamiko yaliyopo Mahakamani. Naona kuwa kuendelea kwake katika nafasi hiyo kunaweza kuleta hasara kubwa kwa taifa, hivyo ni vyema akae pembeni hadi Mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho.
Natoa wito kwa viongozi wenzangu, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Kilimo Mh. Hussen Bashe, Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Prof. Kennedy Bengesi, pamoja na Kamishna wa TRA na makampuni binafsi, wafike Mahakamani wao wenyewe ili kushuhudia mwenendo wa kesi badala ya kuwaachia mawakili wao pekee.