Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 10, leo Aprili 19, 2024.
Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina amesema Serikali haiwezi kuendelea kuvumilia Wizi, Ufisadi, Rushwa na Mateso kwa watanzania yanayokea kwenye baadhi ya Sekta nchini.
Mpina amesema hakuna mgawanyiko wa madaraka ulio wazi miongoni mwa watumishi hivyo kuendelea malumbano yasiyo na tija kwa kuwa kila mtumishi hujiona mkubwa kuliko mwingine. Aidha, teuzi na baadhi ya ajira kutolewa bila kuzingatia ushindani imefanya nchi ipate viongozi dhaifu ambao hushindwa kutekeleza majukumu yao pamoja na kumpa kazi kubwa Rais ya kuteua na kutengua kila mara.
Amehoji kwanini waziri ateuliwe na siyo kushindana kwenye Interview? Hali kadhalika kwa Makatibu wakuu, wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa, pia mfumo wa vetting hautoi hakikisho la kupata viongozi sahihi, unapendekeza huyu awe DC umempata wapi? Nani ameanzisha huo mchakato wa maombi? Yamepatikanaje kwa Rais maombi hayo?