Luis Antonio Valencia Mosquera

Luis Antonio Valencia Mosquera

Messi Lionel

Senior Member
Joined
Jan 11, 2018
Posts
170
Reaction score
159
Kipindi nasoma elimu yangu ya msingi nakumbuka hasa
nilipofika darasa la 5 nilianza kuona ukali wangu katika somo la Maarifa ya jamii na nilitokea kulipenda mno ni kwasababu lilikuwa na mchanganyiko wa historia,jiografia na uraia..

Tukiwa darasa la 7 Mwalimu wangu alitufundisha kuwa Mstari wa Ikweta(equator) unaoigawa dunia katika sehemu mbili zilizo sawa Kaskazini na kusini umepita katika miji miwili mikubwa duniani Entebe(Uganda) na Quito(Ecuador)
Ecuador ndio nchi anayotoka Luis Antonio Valencia Mosquera wengi tumemzoea Antonio Valencia winga na beki wa kulia wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Ecuador..
Jamaa amezaliwa katika mji mmoja mdogo unaitwa Lago uko pembezoni mwa misitu mizito ya mto mkubwa duniani Amazon.Katika ukuaji wake jamaa alipitia katika maisha ambayo leo hii wengi wanalalamika kila siku Magufuli Magufuli..

kazi yake kubwa ilikuwa kumsaidia Mama yake kazi za kuuza maji nje ya uwanja wa timu moja kubwa katika ligi ya Ecuador(Ecuador Serie A) inaitwa El Nacional ni timu ya jeshi ambayo pia baada ya maskauti kumwona alikuja kupata nafasi ya kuichezea timu hiyo hiyo katika ngazi ya wakubwa..
Baada ya kazi za kuuza maji na mama yake katika muda wa ziada unaambiwa jamaa angeendelea kukusanya chupa tupu(empty bottles) kwajili ya kumpelekea baba yake akauze kwenye makampuni ya ukusanyaji chupa tupu kama ilivyo pale maeneo ya mwenge wanavyofanya vijana wengi.

Tangu alipozaliwa Agosti 4,1985 ukiwa ni mwaka mmoja aliozaliwa Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo jamaa amefanikiwa kupita timu nyingi kama El Nacional(Timu ya Jeshi huko Ecuador) baadaye akaenda Villareal Hispania baadaye alipelekwa kwa mkopo Recreativo kabla ya kwenda kwa mkopo wa mwaka mzima Wigan Athletic na baadaye kuuzwa jumla mwaka 2008.
Ujue katika pitapita zangu vibanda umiza siku moja nacheki mechi ya Arsenal na Wigan Athletic nilijikuta muda wote namshangaa winga wa kulia wa wigan wakati huo Antonio Valencia akiwasumbua sana mabeki wa Mzee Wenger hasa Gael Clichy.

Baada ya Cristiano Ronaldo kuuzwa Real Madrid mwaka 2009 ndipo Sir.Alex Ferguson aliponionesha kumbe hata mtu akiwa bongo huwa ana mawazo mara nyingine sawa na mtu wa ulaya kwani niliwaza sana huyu jamaa asingebaki pale wigan kwa miaka mingi,Hatimaye Babu Fergie akambeba katika majira ya joto(summer window) ili kuja kuziba Pengo la Ronaldo..
Ingekuwa ngumu mno kwa mchezaji kama Valencia kuziba Pengo la Ronaldo lakini jamaa alifanikiwa kuongeza jambo kubwa sana katika kikosi cha Man utd.

Kitu kilichokuwa kinambeba sana huyu Unsung Hero wangu wa leo ni hiki.
Kwanza kabisa kabisa ukiacha Ji Sung Park,Darren Fletcher,John O'shea hata Wayne Rooney sijawahi kuona mchezaji mwenye nidhamu ya mchezo kama Antonio Valencia.

Tunaposema nidhamu ya mchezo tuna maana ya kucheza katika majukumu ambayo mwalimu amekupangia ndani ya uwanja ambapo halikuwa tatizo kwa Antonio.
Jamaa katika miaka yake 8 aliyodumu katika jiji la Manchester amefanikiwa kuipa ManUtd Vikombe viwili vya EPL,vitatu vya Kombe la Ligi(EFL),vitatu vya Ngao ya Hisani,Moja la Uefa Europa League na pia amefanya kazi na makocha wanne tofauti kwa usahihi mkubwa sana..

Makocha Kama Sir Alex Ferguson,David Moyes,Louis Van Gaal,na Sasa Jose Felix Mourinho.
Kingine ni kwamba Jamaa ana Juhudi binafsi sana katika kazi yake,mshindani na mpambanaji mkubwa sana.
Ametengeneza zaidi ya magoli 25 katika timu yake tangu ajiunge nayo..

Kuna kipindi ilikuwa ni bora Rooney asiingie uwanjani kama hajamwona mpishi wake wa magoli Antonio..
jamaa kakamilika mno,ana stamina,nguvu(physique),spidi kubwa uwanjani,na mara nyingi sana anafunga yeye mwenyewe na ni mkabaji mzuri sana..

Hata katika Timu ya Taifa jamaa amechangia kuwapeleka katika michuano mikubwa kama world cup 2006,2014,Copa America 2015 na Centenario na katika mechi 80 za Timu ya Taifa amefanikiwa kufunga mabao 10 tangu enzi zile akiwa na Kina Christian Benitez(Chucho) mpaka sasa akiwa na Ener Valencia wa Everton.

Nimeona wachezaji wengi katika timu ya Machester United lakini kwa kipindi hiki huyu ni shujaa wangu asiyeimbwa kwani Mara zote msimu ulioisha na Manchester united kufanikiwa kujikusanyia vikombe vitatu(Ngao ya jamii,EFL Cup na Uefa Europa League) wachezaji kama Ander Herrera,PaulPogba,Antoni Martial,Henrick Mkhitaryan Micky,Zlatan Ibrahimovic,Marcus Rashford,JuanManuel Mata,Eric Baily na David De Gea wamekuwa wakisifiwa sana na Mashabiki lakini ni mara chache walikuwa wakimtaja Valencia katika hatua zao zote za mafanikio.

Lakini leo hii jicho langu limetua moja kwa moja kutambua mchango wa Antonio Valencia katika Timu ya Manchester United na Ecuador

[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]
 
Alivunjika mguu kipindi fulani. Iliniuma sana.
Baada ya kupona kapunguza kasi yake kidogo.
Kwa uwezo wake wa kukaba na kushambulia anampa kocha nafasi ya kubadili mfumo kirahisi
 
Yuko vizuri! Kuna kipindi alivaa jezi namba 7 sijui ikawaje akarudia namba 25!
 
Yuko vizuri! Kuna kipindi alivaa jezi namba 7 sijui ikawaje akarudia namba 25!
Ile number ni kubwa. Aliona haitendei haki ndio maana aliva jezi ya number7 msimu mmjoa tu
 
f39d68667695dd05257326870fc2be97.jpg

Number 25
 
Back
Top Bottom