Luís Miquissone nini kimekukuta?

Huo uchawi wanarogwa na watu wa nje au wanarogana?
Mi nikimuona mtu anazungumsha uchawi ktk soka namuona kama mwehu, na mashabiki wa Simba hii kitu imewakaa sana damuni.

Huko nje ambako tunaamini hakuna uchawi kuna mifano mingi sana ya wachezaji ambao pancha kwao ni mara kwa mara, unakuta msimu mzima mtu kacheza miezi miwili tu.
 
Mtu akiongelea uchawi ktk mpira namuona hajielewi kabisa. Na sijui kwanini mashabiki wa Simba wanaamini sana ktk uchawi.
 
Miquissone ni yuleyule.... Jamaa alihitaji mechi nyingi Ili awe fit, sababu muda mrefu hakuwa na timu baada ya kutoka arabuni. Ilibidi apate gemu tatu full. Kiufupi soka la bongo Lina figisu sana, unakumbuka ishu ya Okra, viongozi walidai jamaa ni majeruhi huku mwenyewe akidai alikua fit na hakua majeruhi
 
Sasa Kama ndio hivyo inabidi lifanyike Jambo vingenevyo wachezaji wetu wataendelea kupigwa MIBA....Kama yule aubin kramo wanampiga kweliKweli....kipindi kile kapona kurudi uwanja wa mazoezi kaumia Tena hii inanipa mashaka sanaa

Na wewe unaamini ni kweli ?
 
Fedha zimemlevya ,kipindi cha mwanzo alikuwa na njaa...Arab money ni hatari...he was getting arab money.
 
Hii karne bado kuna mijitu inaamini ktk ulozi.
Ama kweli ninaona aibu mimi ninatamani kukuona unafananaje
 
Class is permanent and form is temporary naamini Luis miquisoni bado ni mchezaji mzuri ila ni kipindi tu anapitia mpira ni kama baiskeli ukijua umejua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…