Luís Miquissone nini kimekukuta?

Luís Miquissone nini kimekukuta?

Huo uchawi wanarogwa na watu wa nje au wanarogana?
Mi nikimuona mtu anazungumsha uchawi ktk soka namuona kama mwehu, na mashabiki wa Simba hii kitu imewakaa sana damuni.

Huko nje ambako tunaamini hakuna uchawi kuna mifano mingi sana ya wachezaji ambao pancha kwao ni mara kwa mara, unakuta msimu mzima mtu kacheza miezi miwili tu.
 
Ulozi ni theory tu , kujituma,politics na viwango vibovu.
EPL, spain na french league, perfoming team kwenye hizo league wanawezaje kukaa top miaka mingi?

Investiment,masilahi, na ushindani wa hali ya juu ndani na nje ya club.
Simba imeingiliwa na mdudu ambae amewarudisha nyuma walipotoka
Mtu akiongelea uchawi ktk mpira namuona hajielewi kabisa. Na sijui kwanini mashabiki wa Simba wanaamini sana ktk uchawi.
 
Miquissone ni yuleyule.... Jamaa alihitaji mechi nyingi Ili awe fit, sababu muda mrefu hakuwa na timu baada ya kutoka arabuni. Ilibidi apate gemu tatu full. Kiufupi soka la bongo Lina figisu sana, unakumbuka ishu ya Okra, viongozi walidai jamaa ni majeruhi huku mwenyewe akidai alikua fit na hakua majeruhi
 
Sasa Kama ndio hivyo inabidi lifanyike Jambo vingenevyo wachezaji wetu wataendelea kupigwa MIBA....Kama yule aubin kramo wanampiga kweliKweli....kipindi kile kapona kurudi uwanja wa mazoezi kaumia Tena hii inanipa mashaka sanaa

Na wewe unaamini ni kweli ?
 
Fedha zimemlevya ,kipindi cha mwanzo alikuwa na njaa...Arab money ni hatari...he was getting arab money.
 
Braza amini nakwambia isingekuwa silaha aliyoipeleka kule wasingekuwa tayari kumpokea. Sawa ameenda kula pesa sikatai. Jamaa alileta mtaalamu wa mambo ya utamaduni pale mtaa wa Msimbazi, kama unafuatilia Simba kipindi cha nyuma walikuwa wanafanya kinachofanywa na nyuma mwiko sasa hivi (kutoa misaada kwa watoto yatima, wazee na makundi maaalum mengine). Ndio maana alikuwa anasemaga Simba itachukua ubingwa 10 years back to back.
Hii karne bado kuna mijitu inaamini ktk ulozi.
Ama kweli ninaona aibu mimi ninatamani kukuona unafananaje
 
Class is permanent and form is temporary naamini Luis miquisoni bado ni mchezaji mzuri ila ni kipindi tu anapitia mpira ni kama baiskeli ukijua umejua.
 
Back
Top Bottom