Luís Miquissone nini kimekukuta?

Luís Miquissone nini kimekukuta?

Katka maisha kuna kitu kinaitwa kulizika ikifika hio stage kila kitu unaona normal nahutamani kufanya kitu kingine zaidi na huna shauku kufikia kitu kingine kwakua umelizika,kwangu mm he need to do what he was doing before go back to basics train hard and wait for the opportunity

Kulizika kuna raha na ubaya wake. Kuridhika kwenye kazi result moja wapo ndio hii. Kukosa hari, stop kuwa creative, hujitumi tena.
Huyu anahitaj coach wa saikolojia but kile alichonwcho pia kipunguzwe ili akili iamke
 
Ametoka kukaa nje ya uwanja zaidi ya miezi 6+ alipokuwa Aly Ahly alikuwa anacheza kwa manati dk 10-15 tu...!!, Amekuja kwenye timu inayohitaji matokeo ya mchezaji moja kwa moja bila kujua hali yake aliyonayo yakutokuwa na match fitness, mazoezi yakutosha.
 
Watu wanapiga sana ulozi. Mnamsema Miquisson tu ni kumuonea. Wachezaji wote wa Simba ukiwatizama kwa sasa ni kama vile akili na mwili vinaongea lugha mbili tofauti. Hata wachezaji wa ile timu nyingine ya Kariakoo mnafikiri wanachodeliver ni kiwango chao halisi. Pale Simba kwa sasa hata wakiwachukua wachezaji nguli wa timu zote za Afrika wakawasajili wataonesha kiwango kwa mwezi mmoja hadi mitatu baada ya hapo ni uvundo mtupu. Kosa kubwa Simba wamelifanya ni kumfukuza bwana yule aliyeondoka na mtu wake ambaye kwa sasa anafanya kazi upande wa pili.

Ulozi ni theory tu , kujituma,politics na viwango vibovu.
EPL, spain na french league, perfoming team kwenye hizo league wanawezaje kukaa top miaka mingi?

Investiment,masilahi, na ushindani wa hali ya juu ndani na nje ya club.
Simba imeingiliwa na mdudu ambae amewarudisha nyuma walipotoka
 
Ametoka kukaa nje ya uwanja zaidi ya miezi 6+ alipokuwa Aly Ahly alikuwa anacheza kwa manati dk 10-15 tu...!!, Amekuja kwenye timu inayohitaji matokeo ya mchezaji moja kwa moja bila kujua hali yake aliyonayo yakutokuwa na match fitness, mazoezi yakutosha.
Kama ndio hivyo tukiri Basi viongozi wa Simba wamerudia SAME mistake Kama ilivyokuwa kwa sawadogo right???? (Kutokana na maelezo YAKo )
 
Kwa hii fans pressure aliyopo Simba viongozi wanaweza kumvumilia kweli mpk ajipate???
Tatizo sio fans pressure... Inshu ngumu nayoina kwake n kama vile kocha hatampa nafasi na wala hatasumbuka Naye hapo natumia tu saikolojia ndogo kumsoma Benchika kile alichosema wakati anakuja...

"Sitaangalia Nani ni star, wachezaji wote wako Sawa Yule atayenifit ndo ntampanga..."

Simba fans hakuna asiyeujua uwezo wa Miquesson na ndani ya mioyo Yao wanampenda sana ndo maana alitambulishwa siku ya mwananchi ili kuwatisha wapinzani wao hivo kuhusu mashabiki asilimia kubwa wapo upande wake hiyo sio shida tatizo ni kua sioni akipewa nafasi na kocha...

Kocha anataka kutengeneza wachezaji wake thus y unaona umeibuka mgogoro wa Chama hii yote ni kuwazima Kwanza ma-star waliokuepo ili atengeneze wa kwake ni kitu cha kawaida Tu ndo maana hata Tinho alimuunda Kibu kua mchezaji muhimu Sana...

My take
Miquesson bado ni winger Bora hapa bongo kama akipewa nafasi hata game mbili tu acheze dakika 90... Vuta picha Onana kaaminiwa kidogo watu wanamuona "dili" vipi Kwa Miq??
 
Mmakonde anavyomsifia mmakonde mwenzake, eti akiitwa Konde boy sababu ya Harmonize. Eddo Kumwembe aache uongo, akiitwa Konde boy sababu alitokea Msumbiji ambako kabila la wamakonde linapatikana
 
Ndio uhalisia hakuna timu kubwa yoyote inayoweza kumsajiri mchezaji ambaye amekaa Zaid ya miezi 6 bila timu na kucheza!!, Sawadogo na MIQUISONE ni mifano hai. Wote wamefeli....!.
Morrison kabla hajaja hapa bongo kucheza Dar Young Africans unajua alikua amekaa nje ya uwanja Kwa muda gani?
Hata huyu Max zingeli alikua nje ya uwanja Kwa muda gani? hebu fatilia...
 
Morrison kabla hajaja hapa bongo kucheza Dar Young Africans unajua alikua amekaa nje ya uwanja Kwa muda gani?
Hata huyu Max zingeli alikua nje ya uwanja Kwa muda gani? hebu fatilia...
Yanga ni timu kubwa Hapa Tz sio kwenye ulimwwngu wa mpira wa professional!. Nilitegemea uniambie Madrid,Man City au Bayern... Tz hakuna professionalism kwenye suala la usajiri. Pia Max ametoka Maniema akicheza acha kudanganya
 
Braza amini nakwambia isingekuwa silaha aliyoipeleka kule wasingekuwa tayari kumpokea. Sawa ameenda kula pesa sikatai. Jamaa alileta mtaalamu wa mambo ya utamaduni pale mtaa wa Msimbazi, kama unafuatilia Simba kipindi cha nyuma walikuwa wanafanya kinachofanywa na nyuma mwiko sasa hivi (kutoa misaada kwa watoto yatima, wazee na makundi maaalum mengine). Ndio maana alikuwa anasemaga Simba itachukua ubingwa 10 years back to back.
Taifa likiwa na watu wa hivi usitalajie shida ya umeme kuisha.
 
Kiwango chake ndio kishaenda alijojo hivyo, mambo ya kawaida kwa wachezaji, akili inakuwa inataka lakini mwili ndio ishagoma...
 
Braza amini nakwambia isingekuwa silaha aliyoipeleka kule wasingekuwa tayari kumpokea. Sawa ameenda kula pesa sikatai. Jamaa alileta mtaalamu wa mambo ya utamaduni pale mtaa wa Msimbazi, kama unafuatilia Simba kipindi cha nyuma walikuwa wanafanya kinachofanywa na nyuma mwiko sasa hivi (kutoa misaada kwa watoto yatima, wazee na makundi maaalum mengine). Ndio maana alikuwa anasemaga Simba itachukua ubingwa 10 years back to back.
Kwani simba wamekatazwa kwenda kutoa misaada
Nchi hii kuna ujinga mwingi
 
Ametoka kukaa nje ya uwanja zaidi ya miezi 6+ alipokuwa Aly Ahly alikuwa anacheza kwa manati dk 10-15 tu...!!, Amekuja kwenye timu inayohitaji matokeo ya mchezaji moja kwa moja bila kujua hali yake aliyonayo yakutokuwa na match fitness, mazoezi yakutosha.
Ana Assists nyingi kwenye ligi kuliko Ntibazonkiza
 
Back
Top Bottom